Chenge, StarTV na Utaalam wa kisasa

Chenge, StarTV na Utaalam wa kisasa

Kuhani.. nchi zilizoendelea zinalinda sources pia... si kweli kwamba watu wakiandika habari basi hadi majina yao yajulikane. Umesahau skendo ya Watergate? Na zipo nyingi kila kukicha ambapo vyanzo vya habari vinalindwa sana... au umesahamu mambo ya Valerie Plamer..?

Ukiona watu tunaandika kwa uhakika ni kwa sababu sources hizo ni impeccable... tatizo ni kwamba wakati mwingine u kiitaja source ni rahisi sana kwa wajanja kufanya elimination na kujua source ni nani...

Mwnkjj,

Nimeelezea kwa mifano jinsi anonymous sources zilivyo na nafasi na zinavyotumika katika Uandishi uliopevuka.

Ndugu, unatetea fani yako, lakini na mimi kama mpokea habari napigania ubora wa habari nitazokubali uniletee!

Ahsante.
 
KK,

unajaribu kuleta analysis ya kimagharibi uliko katika jamii yetu ambayo watu tunayoishi tunifahamu fika.Wewe na Pundit mmekaa huko ng'ambo na kujifunza dunia kupitia jicho la kimagharibi,kumbuka this is African politics conducted in an African way...
 
Mwnkjj,

Nimeelezea kwa mifano jinsi anonymous sources zilivyo na nafasi na zinavyotumika katika Uandishi uliopevuka.

Ndugu, unatetea fani yako, lakini na mimi kama mpokea habari napigania ubora wa habari nitazokubali uniletee!

Ahsante.


Mzee hii ni forum na si gazeti, TV, au Radio.. ni modern media ambapo sheria za uandishi ziko very gray.. msingi mkubwa wa haya mambo ni anonymity. Sasa ukianza kuiangalia JF kama classic media unafanya makosa makubwa sana kwani JF, Blogs.. etc siyo classical media.. ni modern media ambazo kwa hakika kiini chake cha habari ni tetesi, uvumi, na uzushi.

Kutoka hapa ndio regular media zinatakiwa kuingia kati kwa vile wana resources, manpower na wanalipwa kufuatilia habari hizo au tetesi hizo. Ndio maana itakuwa makosa makubwa sana kwa regular media kuandika habari nzito zinazotoka kwenye mtandao pasipo wao wenyewe kuzihakikisha. Kama kile kisa cha Facebook ambapo media zilidai mtoto wa Waziri Mkuu aliyeuliwa wa Pakistan Benazir Bhutto alikuwa na ukurasa waka n.k Hilo pia lilitokea kwa kijana mwingine wa Morocco hivyo hivyo.

Sasa unapotaka quality ya habari ni sawa kabisa lakini quality ya habari katika mtandao huwezi kuwekea kiwango kile cha regular media kwa sababu kwenye mtandao news is raw and undiluted.. inakuja jinsi ilivyo. HIvyo utakuta porojo, tetesi, uvumi, habari za kweli, n.k n.k Ni jukumu lako kama msomaji kuamua na kuzipa uzito unaostahili.

Lakini kwa kadiri mambo yanavyokwenda habari zenye uhakika zinaletwa hapa. Ndio maana tulikuwa wa kwanza kuelezea kilichotokea kuhusu ndege iliyoanguka kwa kutoa muda, mahali, na idadi halisi ya waliofariki.. na kuna habari nyingine nyingi ambazo zinapoletwa hapa lengo lake siyo kuhabarisha bali kusababisha mabadiliko.

Suala la Mkullo kwa mfano, kwa wengine wanafikiri ni habari kwao, lakini kwa wanaojua ni ujumbe uliotumwa kwa Mkullo kuwa "tunajua" na atengeneze mambo yake. Siyo kwa yeye tu bali hata kwa watu wengine wanaotajwa hapa au taasisi zinazotajwa hapa.

So, ombi langu ni kuwa na leeway ya watoa habari hapa, tusije kuanza kujifanya sisi CNN au FNC kiasi kwamba mtu akiwa na nyeti aanze kusita kwa kuogopa kuambiwa aoneshe video, picha n.k vikiwepo vitaletwa visipokuwepo tuvipime...
 
Mwnkjj,

Nimeelezea kwa mifano jinsi anonymous sources zilivyo na nafasi na zinavyotumika katika Uandishi uliopevuka.

Ndugu, unatetea fani yako, lakini na mimi kama mpokea habari napigania ubora wa habari nitazokubali uniletee!

Ahsante.

KK na ubora wa habari lazima source ijulikane?Kipi cha msingi:content au source?

Je kila habari source yake huwa credible?Ni kwa vipi wewe kama mpokea habari unaiamini source iliyotajwa na mwandishi?

Kwa hiyo habari isiyokuwa na source (inayokwenda sambamba na imani yako) kwako si habari (I mean contentwise)?
 
Mwnkjj,

Nimeelezea kwa mifano jinsi anonymous sources zilivyo na nafasi na zinavyotumika katika Uandishi uliopevuka.

Ndugu, unatetea fani yako, lakini na mimi kama mpokea habari napigania ubora wa habari nitazokubali uniletee!

Ahsante.

Kwa nini nawewe usilete habari zako kama unazo? makelele mengi tu na hakuna kitu unafanya. Wewe unasema kuwa Chenge ni fisadi? una hakika na hili?
 
sema weye mzee wa kijiji nikisema miye inzi watasema ni mzushi na mchafu!
 
"Ni kweli, Matatizo ya Ufisadi yamemwingiza Chenge kwenyeUshirikina"

Nalazimika kuchangia kutokana na attitude ya kupenda shorcut ya Pundit na Kuhani Mkuu ya kuita kila kitu wasichokijua kuwa "udaku". Hawaelewi kuwa huku Bongo wanasiasa, viongozi wa dini, timu za mpira n.k. hujipanga uchi wa mnyama wakiomba vyeo na ushindi Mlingotini, Bagamoyo na sehemu zingine zenye "mafundi" wa asili. Hivyo si kitu cha kuwashangaza hawa wenzetu, sijui wanaishi Ulaya, kwa Chenge, Msukuma, aliyekulia katika mazingira ya ushirikina ya kuua vizee vyenye macho mekundu, kuwanyunyizia Wabunge wenzake "nyuklia" za Kisukuma ili asiandamwe na sakata la rada na vijisenti. Mimi niko Dodoma na waandishi wa habari wenzangu ambao tumeshuhudia tukio hilo! Mzee wa vijisenti kamimina vibuyu viwili vizima kwenye meza na kiti cha Spika, Naibu Spika, na wabunge machachari akina Ole Sendeka, Anne Kilango, Mwakyembe, Manyanya, Selelii, Mnyaa, Slaa, Mwambalaswa, Zitto, Mkumba na wengineo. Hili ni suala very serious ambalo lazima Bunge lilifanyie uchunguzi wa kina. Vibuyu vya Chenge vinaweza kuwa na pilipili ya Kiafghanistan yenye madhara ya muda mrefu. Tayari tunaambiwa mmoja wa vinara wa Richmond anaumwa! Inawezekana kabisa inatokana na ndumba za Mjumbe wa Kamati Kuu ya CCM, Chenge! Acheni mzaha, nchi imekwisha! Lazaros

Niko makini sana kuepuka kuita watu majina, lakini hapa najisikia comfortable kusema hukushuhudia lolote, wewe ni muongo!

Na kama unadiriki kusema Bunge lichunguze vibuyu vya kichawi vya Chenge niko comfortable kusema wewe sio Mwandishi, umeongopa na hapo pia.

Unazidi kunukisha jina chafu la Waandishi wa Bongo!
 
Hii habari tulisema jana baada ya mwakyembe kujisikia hovyo. CHenge alirudi ndani baada ya kikao kuisha na ni kweli alionekana kwenye cameras akipita kwa spika na eneo la mwakyembe pamoja na wengine, coincidence or not, Mwakyembe kesho yake hoi baada ya muda mfupi tu. Hivi sasa
anatarajiwa kuenda Nairobi for uchunguzi zaidi. Siyo udaku, tuliongelea hii jana. Alisahau nini kwenye viti vya wenzake?
 
Niko makini sana kuepuka kuita watu majina, lakini hapa najisikia comfortable kusema hukushuhudia lolote, wewe ni muongo!

Na kama unadiriki kusema Bunge lichunguze vibuyu vya kichawi vya Chenge niko comfortable kusema wewe sio Mwandishi, umeongopa na hapo pia.

Unazidi kunukisha jina chafu la Waandishi wa Bongo!

Mwenzangu umejuaje kuwa huyo ni mwandishi?
 
Kwa nini nawewe usilete habari zako kama unazo? makelele mengi tu na hakuna kitu unafanya. Wewe unasema kuwa Chenge ni fisadi? una hakika na hili?

Kwetu sisi kama watz uhakika tunao,ila kwa KK sijui (maana yeye anasubiri source).Tuna uhakika kwa sababu Chenge tunamfahamu,tumeishi naye,tunajua anakula na kina nani,tunyumba twake twa Mikocheni na Bwiru Mwanza (alikopangisha wazungu) tunafahamika,ukiachilia mbali deals zake chafu...

Back to KK,habari ni content (irrespective of the source) tu period.Kwa sababu unapoongelea source unamaanisha authority (in literary works),na sasa kuaminika kwa authority/source yako inategemeana na credibiltiy ya jamii kuhusu source hiyo.Mfano katika jamii ya kiyahudi (na Uarabuni mpaka sasa) mwanamke ni kiumbe dhaifu incapable of doing men's undertakings...ndio maana katika Biblia wale wanawake watatu waliposema yesu kafufuka (kwa maana ya kutokuwemo kaburini) hawakuaminika mbele ya kina Petro mpaka Petro alipokwenda kuhakikisha (wakati kina mama hao walikuwa ni source ya habari hiyo)...ndo sababu nimekuuliza unapimaje credibility ya source yako?

KK wakati mwingine too much of academic arguments hazitupeleki popote hasa ukizingatia the reality of African politics which fact you simply and expressly ignore...
 
Kwa nini nawewe usilete habari zako kama unazo? makelele mengi tu na hakuna kitu unafanya. Wewe unasema kuwa Chenge ni fisadi? una hakika na hili?

Kwa sababu mimi sijajiweka kama mleta habari. Na, kama responsible news consumer, ukiniletea udaku nakataa!

Tusipokuwa na savvy news audience tunaendelea kulishwa tabloid journalism. Na tutaendelea kuwa hatuna Press Tanzania. Nchi litazidi kuangamia kwa sababu katika information age huwezi kuwa na jamii yenye dead Press!

Na sio kila mtu ni mleta habari. Kama sina habari haina maana nitengeneze jibberish nizilete hapa.

Naamini Chenge ni fisadi, lakini sikubali habari za kikuda kuda za kichawi katika karne ya 21. Halafu kesho kutwa tunasikia mnawaomba misamaha mafisadi, na mkishindwa kesi za libel and defamation mnaomba mafisadi wawaachie, wasiwadai hela. Mnawapa mafisadi kusema.
 
Kwa sababu mimi sijajiweka kama mleta habari. Na, kama responsible news consumer, ukiniletea udaku nakataa!

Tusipokuwa na savvy news audience tunaendelea kulishwa tabloid journalism. Na tutaendelea kuwa hatuna Press Tanzania. Nchi litazidi kuangamia kwa sababu katika information age huwezi kuwa na jamii yenye dead Press!

Na sio kila mtu ni mleta habari. Kama sina habari haina maana nitengeneze jibberish nizilete hapa.

Naamini Chenge ni fisadi, lakini sikubali habari za kikuda kuda za kichawi katika karne ya 21. Halafu kesho kutwa tunasikia mnawaomba misamaha mafisadi, na mkishindwa kesi za libel and defamation mnaomba mafisadi wawaachie, wasiwadai hela. Mnawapa mafisadi kusema

Sasa wewe si uwapigie maeditor wa magazeti haya huko bongo. ukipigana na waandishi wa habari hapa JF utafanikiwa? Hii ni JF men chill out, mbona unakuwa mkali hivyo na ndio mwanzo ijumaa imeanza? hivi utamaliza weekend kweli?

Hapa mambo mengi yanaanza bila uthibitisho kama ya deni la Mbowe na baadaye yanakuja kuwa wazi. usipambane sana na messengers, peleka vita yako kwa wenye propaganda wenyewe - kina Mrema na wenzake.
 
weye kuhani saa nyingine unakuwa kana mgema aliyesifiwa......

Kwanza mi nasikitika vibaya mno nimeanza kusifiwa sifiwa hapa JF. Inaninyima uhuru! Sitaki kasifa wala ka status hapa JF. Nilisema toka mwanzo sikubali kiutamaduni wala ki pecking order cha hapa.
 
Kwanza mi nasikitika vibaya mno nimeanza kusifiwa sifiwa hapa JF. Inaninyima uhuru! Sitaki kasifa wala ka status hapa JF. Nilisema toka mwanzo sikubali kiutamaduni wala ki pecking order cha hapa.

Hakuna makosa kusifiwa mkuu wangu, wewe kamata sifa tu kadiri zinavyokuja na kuendeleza kazi. Wengi hapa tunapenda mambo yako so endeleza kazi ya kupambana na wapinzani kama ulivyokuwa umeianza kwa moyo mkunjufu.
 
THOMA_WAN.jpg
 
Hata nukuu niliyoiweka kwenye posti yangu kumbe hukuisoma. Jamaa kadai hivi:



Halafu unataka kuni force feed me this type of crock!

Kwani watu wakijiita waandishi wa habari basi hiyo inawafanya wawe waandishi wa habari? wewe naona unapoteza nguvu kupambana na wana habari badala ya kupambana na habari zenyewe. Shauri yako
 
Kwanza mi nasikitika vibaya mno nimeanza kusifiwa sifiwa hapa JF. Inaninyima uhuru! Sitaki kasifa wala ka status hapa JF. Nilisema toka mwanzo sikubali kiutamaduni wala ki pecking order cha hapa.


mzee, sifa na kebehi, hongera na dhihaka ni sehemu za pande zile zile za watu.. so huwa hazikaribishwi zinakuja tu..
 
Kwa sababu mimi sijajiweka kama mleta habari. Na, kama responsible news consumer, ukiniletea udaku nakataa!

You are doing a very good job kuukataa huu UDAKU kwa kukazania kuomba sources za UDAKU!!!!
 
Mbunge anaswa akifanya tambiko bungeni Dodoma
*Alisindikizwa na kigogo wa Bunge
*Spika akiri kupokea taarifa hizo


Na Mwandishi Wetu, Dodoma


MBUNGE na Afisa mmoja Mwandamizi wa Bunge wamekutwa ndani ya Ukumbi wa Bunge wakifanya vitu vinavyodhaniwa kuwa ni vya kishirikina.


Taarifa zilizopatikana mwanzoni mwa wiki hii na kuthibitishwa na ofisi za Bunge, inadaiwa mbunge huyo alifanya tambiko hilo Jumatatu, kabla ya mkutano wa Bunge la Bajeti kuanza Jumanne wiki hii.


Shuhuda aliieleza Mwananchi kwamba, mbunge huyo aliingia kwenye ukumbi huo akiwa ameongozana na katibu mmoja wa bunge (jina tunalo) na kuanza kupita kila kiti cha mbunge na hatimaye aliishia kiti cha Spika.


Aliongeza kuwa, watu hao wakiwa wamefuatana walikuwa wakipita kila kiti huku mbunge huyo akinyunyiza vitu vinavyohisiwa kuwa dawa za kienyeji katika viti vya wabunge.


"Alipofika kwenye kiti cha Spika, alisimama muda mrefu akiwa ananyunyizia vitu fulani, lakini sikujua ni nini na wao waliamini kamera zote zilikuwa zimefungwa," alidai shuhuda huyo.


Shuhuda huyo alidai kuwa, mbunge huyo na mtumishi wa bunge walifanya shughuli yao bila kufahamu iwapo walikuwa wakionekana, bila kujua kuwa kulikuwa kuna watu wanafanya majaribio ya kunasa sauti na picha za ukumbini.


"Walianza kwa kusimama nje kwa muda mrefu wakiwa na wabunge wengine, baada ya wabunge kuondoka, mbunge huyo alibaki na katibu na kuingia ukumbini na kuanza kufanya kazi zao," alidai.


Alipoulizwa Spika wa Bunge, Samuel Sitta, iwapo ana taarifa hizo jana, alisema amezipata na kueleza kushangazwa kwake iwapo bado kuna watu wanaoamini mambo ya ushirikina.


"Taarifa ninazo ila siamini, isipokuwa inashangaza kuona kama bado kuna watu wanaamini mambo hayo kwenye dunia ya leo," alisema Sitta.


Sitta alisema baada ya kupata taarifa hizo, Katibu wa Bunge ameanzisha uchunguzi wa suala hilo. Hata hivyo alisema ushirikina hauwezi kusimama badala ya ukweli na haki.


Wakati huo huo, jana alasiri uvumi ulienea mjini hapa kuwa Mbunge wa Kyela, Dk Harrison Mwakyembe alikuwa amefariki dunia.


Dk Mwakyembe ambaye juzi hali ilibadilika ghafla akiwa bungeni, alieleza Mwananchi kuwa afya yake ilikuwa imeimarika na kushangaa lengo la watu wanaoeneza uvumi huo.


Baada ya Dk Mwakyembe kukimbizwa kliniki juzi, baadhi ya wabunge walianza kuhusisha tukio hilo na 'tambiko' hilo lililofanyika Jumatatu, huku wengine wakiapa kutokubali hali hiyo kuendelea.


"Hawa watu na washindwe kwa Jina la Yesu. Wanataka kutuulia mtu bure na matambiko yao, Mungu yupo atasimama kati, ukweli utashinda," alisema mbunge mmoja wa Chama Cha Mapinduzi(CCM).


Mbunge huyo ndiye aliyeoongoza Kamati ya Bunge ya Kuchunguza Mchakato waUshindi wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura kwa Kampuni ya Richmond Development.


Watu mbalimbali nchini walikuwa wakipiga simu mjini Dodoma kuuliza ukweli wa taarifa hizo, lakini wote walikuwa wakijibiwa kwamba hakuna kitu cha aina hiyo.


Kaimu Katibu wa Bunge alikanusha kuhusiana na uvumi wa kifo cha mbunge huyo na akasema Dk Mwakyembe ana afya njema na kwamba jana alizungumza naye akiwa na pamoja Spika wa Bunge Samuel Sitta ambaye aliwaaga jana kwenda safarini Dar es Salaam.


Alisema kuwa ni kweli walipata taarifa za kuzidiwa kiafya hali iliyomfanya akimbizwe kituo cha afya cha karibu ambako alipumzishwa kwa muda kabla ya kuruhusiwa siku hiyo hiyo.


Alisema kuwa hivi sasa afya ya mbunge huyo ni njeama na haina mashaka ya aina yoyote yaliyosababisha watu kadhaa kupata hofu.
 
Back
Top Bottom