Kawaulize wakubwa wako CHADEMA ni nini? Tanzania kuna vyama vitatu tu vya upinzani, chadema ikiwemo. Rudi kamwulize makamba akuonyeshe mipango yote ya uanzishaji wa vyama vya upinzani, na majukumu aliyopewa kila mtu kwa nafasi yake. Au muulize Marando anafahamu zaidi ni kwanini alianzisha NCCR Mageuzi. Muulize Chief Fundikra (RIP) ni kwa nini hasa alianzisha chama. Pia kamuulize Edwini Mtei ni kwa vipi alianzisha CHADEMA.
Kwa taarifa yako vyama vingi vya upinzani vilianzishwa na serikali ya CCM kuitikia mwito wa umoja wa mataifa wa kuboresha demoncrasia. Chama kilichoanzishwa kwa misingi ya upinzani wa dhati ni CHADEMA, ambayo Edwini aliianzisha kumpinga Nyerere. Na alikuwa anamatumaini makubwa sana ya kuchukua nchi na kumtimulia vumbi Nyerere. Na kama utafuatilia kwa makini utajua ni kwanini Nyerere alikisifia CHADEMA siku za uhai wake. Alijua katika vyama vya upinzani vya kweli vyenye nguvu na vyenye uwezo wa kuongoza nchi ni CHADEMA pekee yenye sifa za kutosha. Kumbuka Nyerere hakuwa mnafiki.
Usijidanganye ndugu yangu chadema ni chama cha upinzani cha kweli kabisa, tofauti na NCCR, CUF au TLP.
Halafu Mwambie kuwa CUF ilianzishwa na James Mapalala, then afuatilie ni kitu gani kilitokea mpk Mapalala akapokwa chama na kupewa Waziri kiongozi wa zamani na huyo mshauri wa uchumi wa Rais Mwinyi ambao tangu hapo mpaka sasa wao wapo madarakani, kila msimu wanagombea wao uongozi na chama kimekuwa na chembe chembe za udini.
Wenye akili walirudi nyuma na kuangalia chama chenye kufuata misingi ya sheria ya chama na utawala bora.
Utagundua kuwa CHADEMA walikuwa nafasi ya 3 ktk uchaguzi wa rais wa mwaka 2005.
Lakini ktk uchaguzi huu pmj na wajomba kuchakachua CHADEMA wameshika nafasi ya pili na wingi wa viti vya ubunge.
Hii inatokana na watu kuamka na kufahamu kuwa CUF si wapinzani wa kweli.
ukifuatilia malumbano ya CCM na CUF tangu walipoanza kulumbana utagundua kuwa hawa jamaa hawana tofauti kabisa na muundo wa ule mchezo wa Mieleka wa WWE, kwamba leo fulani ataingia kisha atasema hili, then kesho yule nae ataibuka na kisha kusema lile.
Tangu mwaka 1995 wamekuwa wanapigizana kelele za mwafaka, then ukikaribia uchaguzi Seif Shariff anaibuka na kuwaambia wafuasi wa CUF wenye akili zilizolala kama Mtindi kuwa ''safari hii ni ngangali jino kwa jino''...kisha baada ya uchaguzi anapanda Ndege na kutokomea ughaibuni kisha anawaacha wakojani wakipambana na Polisi na wengine kupoteza maisha.
Then baada ya Muda anarudi na kuja na sera za mwafaka.
Sasa kwa wenye uelewa wakapasukia chezo, so jamaa ndo wamekuja sasa na style hii ya kumpa wadhifa wa waziri kiongozi ambaye hana mamlaka yoyote zaidi ya kusubiri ftari mwezi wa ramadhani.
Chadema ni chama ambacho mwalimu Nyerere hayati alishatamka kwa mdomo wake na kusema kuwa hiki ni chama cha uhakika, na msipokuwa makini CCM hawa jamaa watakuja kuwasumbua sana.
Huyo ni Nyerere anayeijua CCM in n out.
Na ndio huyuhuyu alimwambia mkwere asubiri coz yeye bado saaaana, na ndie huyuhuyu mwaka 95 aliwaita wagombea urais na kisha akamuona mmasai mmoja akiingia na mvi zake kichwani...kisha akastuka na kuuliza ''heeh nawe umo?''...kisha mmasai huyo akainama na kufungua mlango na kutimua vumbi.
Yoote aliyoyasema mzanaki huyu leo wenye akili tunayaona....
Viva Chadema...
Hakuna kukatishwa tamaa na mamluki.