Huku DRC ikisaini makubaliano ya amani na nchi ya Rwanda, siku ya jana, imeripotiwa kuwa serikali ya DRC,kupitia jeshi lake la FARDC, walidungua ndege, iliyokuwa imebeba misaada ya dawa za binadamu, ikiipeleka huko Minembwe, Kivu kusini. Kwa mjibu wa taarifa zilizosambaa, kutokana na ulinzi wa anga,maeneo ya Kivu Kusini, drone iliyohusika ilitokea nchini Burundi. Huku, inasemekana kuna wanajeshi wa Belgium wapatao 300, waliokuja kwenye oparesheni ya kuinyang'anya M23 Kivu kusini.
Mpaka sasa, inasemekana wanyamulenge bado wana hali ngumu, kutokana na kushambuliwa na jeshi la Burundi, la DRC(FRDC), FDLR na wazalendo.
Serikali ya Congo, kupitia msemaji mkuu wa jeshi, ilitoa tangazo na kueleza kilichotokea, kuwa ni ndege isiyojulikana iliyoonekana kwenye rada za jeshi, ikiwa inaelekea katika maeneo yenye mgogoro, na kwa kuwa uongozi haukuwa na taarifa yoyote, ndege hiyo ilidunguliwa.
M23 na yenyewe haikukaa kimya. Tangazo la AFC/M23, limekemea vikali kitendo hicho, na kuahidi hakiwezi kwenda hivo hivo, lazima ilipize kisasi. Imesema kwamba, serikali ya Kinshasa, bado inaonyesha nia ya kutaka kufuta kabila la watutsi kwenye makazi yao.