Bodaboda wa Ferry- Posta Wapandisha Nauli.

Bodaboda wa Ferry- Posta Wapandisha Nauli.

Jaji Mfawidhi

JF-Expert Member
Joined
Feb 20, 2016
Posts
17,588
Reaction score
27,631


boda.jpg
boda.jpg
Leo kijana wangu wa kazi kapanda bodaboda toka ferry mpaka Posta ya zamani na kulipishwa 5000.
Nauli ya Shilingi 5,000 kutoka Ferry kwenda Posta ya zamani ni mzigo usiohalalishwa na umbali mfupi wa safari hiyo.
Mfumo wa kidijitali wa kupima nauli moja kwa moja—kama inavyofanya kazi kwenye programu za usafiri kama Bolt—unapaswa kuwekwa kwenye bodaboda zote ili kuondoa makadirio ya kiholela na kumlinda abiria.

Mzigo wa Nauli ya Shilingi 5,000 kwa Umbali mfupi, bei kubwa: Safari ya kutoka eneo la Ferry (Kivukoni) kuelekea maeneo ya Posta ni fupi sana, lakini baadhi ya madereva wamegeuza kituo hicho kuwa sehemu ya kupangia bei za juu bila mpangilio.

Lakini pia Kukosekana kwa uwazi ambapo abiria mara nyingi hulazimika kujadiliana kwa nguvu au kulipa kiwango kikubwa kutokana na haraka za kazini au mazingira ya kituo.Ukijadili sana anakuacha na kuchukua abiria mwengine asiye bargain.

Athari kwa watumiaji wa kila siku: hasa Wafanyakazi, wafanyabiashara wadogo, na wasafiri wanaovuka bahari wanapata gharama za ziada zisizotarajiwa kila siku. Wanacholipwa kinaishia kama nauli, hebu fikiri kijana wangu wa kazi anakaa Mwembe mtemvu anapanda gario za kisemvule ni 800 mpaka ferry, anapanda sea express ya Bakhresa kwa 500 alafu anapanda boda kwa 5000, kwa siku elfu 12 .na kwa mwezi 300,000/-
Mshara namlipa laki nne na kodi yake take home ni kama 350,000 means mshara unaishia kwenye nauli tu.

Suluhisho: Mfumo wa Umeme wa Kusoma Nauli:-
1. Bei kulingana na umbali halisi: Mfumo wa kielektroniki unaotumia GPS na hesabu ya umbali (kama Bolt) utahakikisha abiria analipa kulingana na kilomita halisi alizosafiri, badala ya kutajwa bei ya kujumlisha.

2. Kuondoa ubishi na urasimu: Nauli inapojitokeza moja kwa moja kwenye skrini au mfumo rasmi, pande zote mbili (dereva na abiria) zinakuwa na uelewa wa pamoja kabla ya safari kuanza.

3. Usalama na uwajibikaji: Mifumo ya kidijitali husaidia kufuatilia safari, kutambua chombo na dereva, na kurahisisha usimamizi unaofanywa na

Hatua Zinazohitajika za Usimamizi wa vituo vikuu: Mamlaka husika na viongozi wa vituo vya bodaboda wanapaswa kuweka utaratibu madhubuti katika eneo la Ferry ili kuzuia ulanguzi wa nauli na Uhamasishaji na uwekaji wa mifumo: Wamiliki wa pikipiki na watoa huduma wanapaswa kuungwa mkono kuingia kwenye mifumo ya kidijitali ya kupanga nauli ili huduma ya bodaboda iwe ya kisasa, ya haki, na yenye kuaminika.​
 
Niliwahi kulipngelea hili sana mifumo ya tax mtandao bado haitosherezi mahitaji ya madereva pia na abilia, kulikua na haja ya kuweka vifaa maalum ili mtu ukifika kwa dereva hamuongei sana unamuuliza ni shingapi kwa kilometer iyo ni simple kuliko kuamua bei kwa makadirio.
 

Attachments

  • IMG_1205.jpeg
    IMG_1205.jpeg
    64.3 KB · Views: 1
Hakuna huduma ya boda boda kww maeneo ya posta, hizo inflated prices zinahusisha hongo kwa maafisa usalama maeneo husika.
Ungetegemea kwa hizo nauli boda wawe na pesa mingi sana, la! pesa nyingi nao wanapeleka
 
wapuuzi sasa siwapande mwendokasi kwa buku tuu, mbona hamtumii akili wakati mwingine? mafisa usafirishaji kwanza ni akina nani? hao ni vibaka tu waliokosa ajira wana justify kuwepo mjini, wakataeni hao jamaa kwanza wengi wao ni majizi kabisa na ynashirikiana na waporaji.
 
Leo kijana wangu wa kazi kapanda bodaboda toka ferry mpaka Posta ya zamani na kulipishwa 5000.
Hata kama alikuwa na mzigo mkubwa, ferry to Posta ya zamani siyo mbali kwa kutembea na umesema ni kijana au ndiyo wale kina Junior??


The walking distance from the ferry terminal (Kigamboni / Kivukoni Ferry Terminal) to Posta ya Zamani in Dar es Salaam is 1.2 km (about 17 minutes on foot via Kivukoni Rd)

AI Overview
 
Hata kama alikuwa na mzigo mkubwa, ferry to Posta ya zamani siyo mbali kwa kutembea na umesema ni kijana au ndiyo wale kina Junior??


The walking distance from the ferry terminal (Kigamboni / Kivukoni Ferry Terminal) to Posta ya Zamani in Dar es Salaam is 1.2 km (about 17 minutes on foot via Kivukoni Rd)

AI Overview
Ni kweli kabisa, lakini kutoka nyumbani mpaka kwenye daldala anatembea kilometa tatu.
 
Back
Top Bottom