carbohydates
JF-Expert Member
- Oct 13, 2026
- 584
- 1,408
Nyota wa soka kutoka Morocco na Senegal wametawala orodha ya mwisho ya wachezaji watano wanaowania tuzo ya Mwanasoka Bora wa Afrika kwa mwaka 2026, iliyotangazwa leo Novemba 25, 2026 na Shirikisho la Soka Afrika (CAF).
Katika orodha hiyo, Morocco ina wawakilishi watatu ambao ni Achraf Hakimi, Brahim Díaz na Ismael Saibari, huku Senegal ikiwa na Sadio Mané na Pape Gueye.
Mshindi wa tuzo hiyo atatangazwa Desemba 2, 2026, katika hafla ya utoaji wa tuzo za CAF itakayofanyika jijini Lagos, Nigeria.
Hakim ambaye ni beki wa kulia wa PSG, anaingia katika kinyang'anyiro hicho akiwa na nafasi ya kutetea tuzo aliyotwaa mwaka 2025.
Hakimi amekuwa miongoni mwa wachezaji muhimu wa PSG na timu ya taifa ya Morocco, akichangia mafanikio ya timu hizo katika mashindano mbalimbali.
Kwa upande wa Sadio, nyota huyo wa Al-Nassr ya Saudi Arabia anawania kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya tatu, baada ya kuitwaa mwaka 2019 na 2022.
Mané anaingia kwenye kinyang'anyiro hicho akiwa na historia nzuri ya mafanikio katika soka la Afrika, ikiwamo kuiongoza Senegal kutwaa ubingwa wa AFCON 2025.