NAANIKA UJINGA WANGU NA KUFICHA HEKIMA YANGU!
Upo wito wa maridhiano kitaifa. Ya namna gani? Tunapishana. Wapo wanaotaka tugange yajayo na wapo wanaotaka tugange yaliyopita. Mimi nina haya. Nimeona bora nianike ujinga wangu ili nipate msaada:
1. Inaonekana maridhiano bila Chadema hayakubaliki. Washawishiwe; wasilazimishwe.
2. Chadema hawawezi kwenda kwenye maridhiano bila Mwenyekiti wao. Siasa ilimweka ndani. Siasa imwondoe. Sheria tunaisingizia.
3. Chadema hawamiliki tena upinzani. Upinzani umehamia mioyoni mwa wananchi katika vyama vyote. Hata CDM wakienda maridhiano bila kuzingatia UKWELI na UWAJIBIKAJI, upinzani utabaki mioyoni mwa wananchi.
4. Tume zimesema mengi kuhusu yaliyotokea 29/10/2025. Tunajichelewesha kukubali kuwa “washauri-machawa” ndio wanahujumu maridhiano. Ukihujumu maridhiano unamhujumu Mkuu wa nchi unayedai unamtetea. Agenda ya rais ajaye atoke Zanzibar ina mantiki gani wakati huu?
5. Yaliyotokea 29/10/2025 yamewapokonya viongozi wetu ujasiri wa kuongoza na kukemea uovu. Maridhiano ya KWELI yatarejesha ujasiri huo. Nani ajitokeze kukemea RUSHWA na kuhimiza watu “walinde migongo” yao?
6. Hivi sasa silaha ya wananchi ni kununa na kuomba dua la kuku. Silaha ya serikali ni “kuacha” utekaji uendelee na “kutohimiza” waliotekwa kuachiliwa. Sioni maridhiano bila hao watu kuonekana!
7. Katika kuteka watu tumeteka UHURU wa wananchi. Bila uhuru hakuna utawala wa sheria. Bila utawala wa sheria tunaongozwa na shuruti ya watawala. Tuirejeshee mahakama uhuru wake kabla mahakama haijaamua kuurejesha yenyewe na kusababisha maasi.
8. Kuhusu Uhuru wa mahakama ninaamini: kwamba, Ni vigumu kwa Rais aliyepo na waliopita kuuaminisha umma kuwa hawaingilii mahakama. Iwe wanaingilia au hawaingilii, umma unaamini kuwa wanaingilia. Hekima ni kutoingilia, lakini wanapolazimika waingilie kwa manufaa ya taifa na si manufaa ya urais, chama au kundi. Kwa sasa waache kujitetea kuwa hawaingilii kwa sababu hakuna atakayewaamini.
9. Ninaendelea kuamini kwamba
Urais siyo rais. Urais ni taasisi.
Utaasisi unaweza kuwa kokoro.
Ndani ya kokoro waweza kuwamo wanaoijumu taasisi ya urais na rais mwenyewe.
10. Wasiojulikana wana nguvu kuliko wanaojulikana. Matokeo yake, viongozi wa kuchaguliwa na wa kuteuliwa, wanawatumikia na kuwatii wasiojulikana kuliko wanavyowatumikia wananchi. Mabadiliko haya ni kikwazo cha maendeleo.
Jamanie! Weusi wa Mjaluo si kukosa sabuni. Siri anaijua kamongo.
.
Eti Kamongo. Kuna msemo wa Kamongo Asinda Nyaamaa 😄😄😄