Pole kwa wafiwa,tunapoteza wana mabadiliko hivihivi!
Unawaza kura tu mama 🙈
Poleni wafiwa.
Sheria za usalama barabarani zikazwe zaidi na adhabu kali sana zitolewe kwa wakiukaji wa sheria na askari wa usalama barabarani ili kuepusha ajali zisizo za lazima, lasivyo tutabaki kusema rest in peace kila siku wakati wanakufa kwa uzembe wa madreva na maaskari wa usalama barabarani, Mungu azipumzishe roho za marehemu mahali pema amen
Simaanishi hivyo mkuu Mbalamwezi1 ila nina maana kuwa kuna mazingira unakutana nayo ambayo hayaepukiki yanalazimisha kutokea ajali mfano ulikuwa unaendesha gari kwa mwendo wa kawaida tu tairi likapasuka nk lakini kumbukumbu za jeshi la polisi kitengo cha usalama barabarani zinaonyesha ajali nyingi zinatokana na uzembe wa madreva kwa kuendesha kwa mwendokasi sana na kufanya overtaking maeneo ya hatari ambapo huweziona gari au chombo kingine kinachotokea mbele, ndiyo nilichomaanisha kila mtu akiwa makini kufuata sheria ajali zitapungua sana kwa kiwango kikubwa sana