Ahsante Sekretareti ya Ajira

Ahsante Sekretareti ya Ajira

Baada ya kupata ndio unawashukuru, walipokaa kimia ulisema wanafanya kazi kwa kujuana. Au na wewe tukutuhumu umepata kwa memo? Kuna ushahidi gani kua hujapata kwa memo kama ulivyokua unalaumu hapo kabla.

Ujifunze umbea haulipi.

Huna akili.
 
Mkuu umeungana na mimi mkuu
Mi nilienda km kutest zari. Mkuu ila duu siamin hata majib yamewahi sana halafu yako poa
 
Nmetumia nauli ya sh 800 kupata ajira mshahara TGS C hahaaa ntafanya kazi kizalendo ila HARAKATI ZA KUMSAIDIA MTANZANIA SIZIACHI NGO'OOO
 
Nimekuwa mingoni mwa watu ambao wanaiponda sana sekretariet ya ajira na hii ni kutokana na kutokufahamu uhalisia na kusikiliza yasemwayo mitaani. Ukweli hawa jamaa wapo fair kwa kiasi kikubwa wala kufahamiana si kigezo cha kupata kazi cha msingi ni kujituma bila kukata tamaa. Nimepata kazi kupitia sekretariet ya ajira, sikuwa hata na jamaa ninayemhisi kuwa namfahamu. Mwaka jana nimefanya interview 5 sikuona ndani mwaka huu nimefanya 3 ya 4 nikafanikiwa kati ya hizo moja nilifanikiwa hadi hatua ya oral interview nayo nikapata kazi. Ushindani ni kigezo, kutokukata tamaa na kumwomba Mungu ndiyo sifa ya kufanikiwa. Ambao ni wadau wa kutafuta ajira msikate tamaa hawa jamaa ni wakombozi wa sisi maskini tusokuwa na wa kutupendelea kule kwenye zile taasisi za kujuana. Hakika Mungu ni mwema. Nimefanya safari 9 toka huku machame kwenda dar lakini Mungu ameniona. Na sasa najiandaa kuwa mtumishi mwaminifu.

Hizo za T.Z.S 710,000/= kwa mwezi mbona wanazitoa na ndo uliyopata wewe hongera
 
Hongera sana mkuu, na Mungu azibariki kazi za mikono yako.
Kubwa kuliko, fanya kazi kwa bidii na ukuwe muaminifu mwenye uadilifu.Pia itunze kazi then itakutunza
 
Hongera sana mkuu, na Mungu azibariki kazi za mikono yako.
Kubwa kuliko, fanya kazi kwa bidii na ukuwe muaminifu mwenye uadilifu.Pia itunze kazi then itakutunza

Nashukuru mkuu. Nitaifanya kwa uaminifu asee.
 
Hongera sana, mi pia ni mhanga wa Ajira naomba kuuliza ivi NHIF na open University of walishaita watu kwenye interview?
 
Hongera sana ila inabidi uwe unakubali ukweli. Hivi kwa mfano usingekuwa umechukuliwa wewe na wakachukuliwa wengine je bado ungesema wako fair?
 
Hongera sana ila inabidi uwe unakubali ukweli. Hivi kwa mfano usingekuwa umechukuliwa wewe na wakachukuliwa wengine je bado ungesema wako fair?

Mkuu, ukweli nilishakubali baada ya kuona watu ninaowafahamu wamepata na wakanipa ushahidi kuwa hakuna hila. Mwanzoni niliwahi kuamini kuna hila kutokana na maneno ya baadhi wa watu na mitandaoni. Hata nisingepata ningeamini bado siku haijafika. Cha msingi nashukuru Mungu ameniwezesha na iwe ni ushahidi kwa wengine kwamba hawa jamaa hawanaga fitna kama isemwavyo na kama ipo lazima kuwepo na ushahidi ila tuache kuwatuhumu kama hatuna ushahidi.
 
scam!!!!!!
 
Back
Top Bottom