uchaguzi

Uchaguzi Tanzania
Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.

Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.

Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.

Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.

Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
  1. Samia atosha tukutane2030

    JamiiForums Tanzania Kukosekana kwa uzalendo wa kweli miongoni mwa Watanzania ndio sababu ya CCM kushinda kila uchaguzi. Nov 2024 CCM itashinda, Oct 2025 itashinda tena

    Kwa tafsiri sahihi isiyogemea chama chochote cha siasa UZALENDO ni hali ya mtu kuipenda nchi yake na kuwa tayari kuifia. Kwa nyongeza ni pale raia anafikia hatua ya kupambana na mtu yeyote bila kujali cheo, hali au mali alizonazo ikiwa tu mtu huyo atahatarisha au kuweka rehani mali za umma...
  2. funaku

    JamiiForums Tanzania Chama kisichoshiriki uchaguzi kifutwe

    Msingi wa uwepo wa chama ni siasa na uchaguzi Mtima wa Siasa za vyama vingi. Unapokuwa na chama kinachotoa visingizio wakati wa uchaguzi na kutupigia kelele wakati kufanya maendeleo.Vyama vya namna hii vinapaswa kufutwa mara moja.
  3. GENTAMYCINE

    JamiiForums Tanzania Kwanini Benki Kuu iliyo chini ya Serikali ya CCM imeamua kubadili Noti za Tanzania mwakani ambako pia kuna Uchaguzi Mkuu?

    Endeleeni tu kudhani Watu wote hatukunywa Maziwa na hatukula Samaki wa Sato na Sangara ili tuwe na Akili Kubwa za Kuwatangulieni kujua kile mlichokipanga au kuna mbinu gani mmeitumia hapa kwa Zoezi hili na hasa kuelekea huo mwaka wa Uchaguzi Mkuu (2025)
  4. M

    JamiiForums Tanzania Kusainiwa Mkataba ujenzi wa Barabara za DSM - MUNGU TUSAIDIE ISIWE NI SIASA ZA UCHAGUZI

    Serikali kupitia waziri wake wa Tamisemi Mh Mchengerwa imetutangazia kusainiwa kwa mikataba ya ujenzi wa Barabara za halmashauri za jiji la DSM. Maoni ya wananchi wengi wanaonyesha kutokuamini uhalisia wa jambo hili kwani inaonyesha ni kila mwaka kumekuwa kukitolewa ahadi nyingi ambazo zimekuwa...
  5. M

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Wananchi Kata ya Zingiziwa Wagomea Uchaguzi Wakidai Kurudishiwa Ardhi Zao

    Wana Jamiiforums mko salama? Mimi naomba Wakazi wa Chanika Zingiziwa mtusaidie kuhusu suala hili, kwa mwenye kufahamu. Juzi, nilitembelea Kata ya Zingiziwa, iliyopo Chanika na kuzungumza na wakazi kuhusu uchaguzi. Nilijulishwa kuwa takriban Wananchi 10,000 wamekataa kujiandikisha na wameapa...
  6. chiembe

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Tafsiri yangu uchaguzi serikali za mitaa: Huo wingi wa watu wanaogombea kuwapigia kura wana CCM ni ishara nzuri kwa 2025. Mtaji huo utunzwe!

    Hii ni ishara tosha kwamba CCM ni maisha yetu, sawa na maji. Watu wako tayari kukesha, hata kuchapana makonde ili waipigie kura CCM. Nadhani makao makuu au ofisi za mikoa na wilaya, zitupie jicho la karibu chaguzi hizi ili anayeshinda au kushidwa, yeye na wafuasi wake wabaki CCM ili 2025 mtu...
  7. J

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 LGE2024 Demokrasia nyakati za uchaguzi inavyokiimarisha Chama Cha Mapinduzi (CCM)

    DEMOKRASIA NYAKATI ZA UCHAGUZI INAVYOKIIMARISHA CHAMA CHA MAPINDUZI Safari ya CCM 🚍 Simulizi hii ya 'Safari ya CCM' inatueleza namna michakato ya kidemokrasia nyakati za uchaguzi inavyokiimarisha Chama cha Mapinduzi (CCM), kwanzia zama za siasa za chama kimoja hadi ulipokuja mfumo wa vyama...
  8. M

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Idadi ya Wapigakura katika daftari la Wakazi haiakisi Takwimu ya Sensa hii ni dosari kubwa ya kubatisha uchaguzi

    Baada ya kupitia takwimu ya sensa 2022 ina jumla ya wananchi wapatao 61 mil. Na inaonyesha watoto wa Tanzania bara ni 29.365 mil sawa na 49.1% Waziri TAMISEMI ameripoti idadi ya wapiga kura 31 mil. Hii inamaana kuwa watu wote wenye umri wa miaka 18+ sawa na 100% wamejiandikisha kupiga kura...
  9. T

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Wapinzani wasisherekee rough za uchaguzi ndani ya ccm hilo ni jalamba la kuja kwao! Ikiwa yanaupata mbichi vipi mkavu?

    Inavoonekana CCM wana utaalamu wa hali ya juu sana katika kucheza rough za uchaguzi. Na dalili za wazi tunaziona kwenye chaguzi za kura za maoni ndani ya chama, na kama haufikiri kwa kina unaweza kudhani zile ni rough ndani ya CCM, lakini ukweli ni kwamba lile ni tangazo la wazi kwa upinzani...
  10. Waufukweni

    JamiiForums Tanzania LGE2024 CCM wacharuana, Uchaguzi Mwananyamala-Kisiwani waahirishwa

    Zoezi la kupiga kura kwa ajili nafasi ya Mwenyekiti na Wajumbe mtaa wa Mwananyamala-Kisiwani jana, Oktoba 23 lilishindikana kutokana na sababu mbalimbali, ikiwemo baadhi ya majina kutokuwepo kwenye orodha ya wakazi, hivyo kusababisha uchaguzi kuhamishiwa Ofisi za CCM Kata ya Mwinjuma. Soma...
  11. MamaSamia2025

    JamiiForums Tanzania Uchaguzi mkuu wa JF

    1. Rais 2. Wabunge Majimbo yatakuwa majukwaa ya JF. Tutapendekeza majina. Hakuna kuhusisha vyama. Tunaweza chagua mwenyekiti wa kuongoza uchaguzi.. kimsingi sisi wengine tupate uongozi angalau wa mtandaoni. Napendekeza majina yafuatayo; Urais wa JF 1. MamaSamia2025 (fomu ni moja tu) Ubunge...
  12. The Watchman

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Mgombea wa Uenyekiti wa Kitongoji huko Makete ambaye ni mwanaume asema yeye ni mwanamke

    Hiki ni kihoja cha mwaka wakuu Mgombea wa Uenyekiti wa Kitongoji wa Chama cha Mapinduzi (CCM) huko Makete amezua gumzo baada ya kudai kuwa yeye ni mwanamke, licha ya kuwa ni mwanaume. Tukio hilo limetokea wakati ambapo mgombea huyo alikuwa akinadi sera zake kwa nia ya kuvutia wapiga kura...
  13. Mwanongwa

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Kwa kasi hii ya kurekebisha miundombinu Mbeya, tunatamani Uchaguzi uwe kila Mwaka

    Hizi chaguzi zina raha yake jamani, huku Mbeya karibia kila Mtaa utakaopita unakutana na Magreda yakiendelea na kazi ya kurekebisha Barabara. Hii huwa inatokea kila tuingiapo kwenye kipindi cha kuelekea uchaguzi tofauti na kipindi lingine. Mwanongwa natamani uchaguzi uwe unafanyika kila baada...
  14. The Supreme Conqueror

    JamiiForums Tanzania Dr Slaa:Chadema acheni visingizio hamkujiandaa uchaguzi wa Serikali za Mitaa msiwadanganye Wananchi.

    Kada na kiongozi muandamizi wa zamani wa Chadema, Dk. Wilbroad Slaa, ameshutumu vikali chama hicho kwa kushindwa kujiandaa kikamilifu kwa uchaguzi wa serikali za mitaa, vitongoji, na vijiji. Katika kauli yake isiyo na kificho, Slaa amewapa somo Chadema, akiwataka wafahamu kwamba kwenda...
  15. DogoWaNjombe

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Ester Thomas (ACT Wazalendo): Kuelekea Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Watiania Msikubali Kutishwa

    Naibu Katibu Mkuu wa Chama cha ACT Wazalendo Bara, Ester Thomas amesema ACT Wazalendo imejipanga vyema kuhakikisha wanachama wake waliotia nia kugombea kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa wanapata msaada wa kisheria katika kipindi cha uhitaji. Amesema maneno hayo leo Oktoba 23 Jijini Mwanza...
  16. F

    JamiiForums Tanzania Kwa kifupi jinsi kura zinavyoibiwa kupitia daftari la mpiga kura. Unajua kwanini vyama vinapigania daftari la mpiga kura kuliko Tume ya Uchaguzi?

    Kimsingi zoezi la uandikishaji wa wapiga kura linapaswa kufanywa na kusimamiwa na Tume Huru ya Uchaguzi pekee na sio watendaji wa serkali za mitaa ambao wanawajibika moja kwa moja kwa watawala wa serkali. Jinsi kura zinvyoibwa kupitia daftari la mpiga kura: Unakuta kituo X waliojiandikisha...
  17. M

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Leo kwenye uchaguzi wa kura za maoni, usanii Mtupu

    Wana Jf, wazima? Leo katika pita pita zangu, nilikuwa Kigamboni. Unaambiwa usanii sio tu kwenye uandikishwaji kwenye daftari. Nimeongea na watu kadhaa pale Kigamboni, Kata ya Vijibweni wanasema Diwani wa Kata hiyo, Zakalia Mkundi siku ya jana alikuwa anafanya kazi ya ugawaji wa Kadi na...
  18. Mtoa Taarifa

    JamiiForums Tanzania Umoja wa Ulaya: Kuna udanganyifu kwenye matokeo yanayotangazwa na Mamlaka za Uchaguzi Msumbiji

    Umoja wa Ulaya umesema umebaini ukiukwaji wa taratibu wakati wa Kuhesabu Kura na hivyo baadhi ya matokeo ya Uchaguzi Mkuu yanayotangazwa hayaendani na uhalisia wa Kura zilizopigwa Taarifa ya Waangalizi wa Uchaguzi wa EU imesisitiza Mamlaka za Uchaguzi kufanya mchakato wa kujumlisha Matokeo kwa...
  19. kijana wa leo

    JamiiForums Tanzania LGE2024 Naunga Mkono Serikali kuongeza majina (Kama kweli hilo limefanyika) kwenye uchaguzi wa Serikali za Mitaa

    Ndugu zangu Watanzania, Unajua sio kila jambo ni la kulalamika, serikali zote Duniani zinahitaji uungwaji mkono na kukubalika kwa wananchi wake mbele ya mataifa mengine. Sasa kwa sisi Tanzania tumejijengea kautaribu ka kulalamika kila siku bila kutimiza wajibu wetu kisheria na kikatiba. Leo...
  20. K

    JamiiForums Tanzania PreGE2025 Kama kweli CCM ingekuwa inabebwa na Tume Huru ya Uchaguzi, tungeshuhudia...

    Kwa kuwa tume huru ya Taifa ya Uchaguzi ndio yenye jukumu la kuratibu na kusimamia zoezi la Uchaguzi Tanzania basi kwa mamlaka iyonayo kama kweli ingekuwa inaibeba CCM, tungeshuhudia : Tusingeshuhudia mahali popote upinzani wakishinda kwenye sehemu yoyote lakini kwa sababu tunaona ushindi wa...
Back
Top Bottom