Uchaguzi hasa wa viongozi katika nchi ni utaratibu (mchakato) rasmi unaoendeshwa kwa mujibu wa sheria kuwawezesha wananchi kufanya maamuzi kwa njia ya kuwapigia kura kuwachagua watu ambao wanawataka kuwaongoza kwa kipindi maalum.
Uchaguzi ni utaratibu wa kawaida wa demokrasia wa kuwapata wawakilishi wa kisiasa ambao umekuwa ukitumika tangu karne ya 17. Kuna aina tatu za msingi za uchaguzi zinazotumiwa kuwapata viongozi kulingana na mfumo unaotumiwa na nchi husika.
Aina hizo ni uchaguzi wa Rais, Uchaguzi wa Wabunge na Wawakilishi katika Baraza la Kutunga Sheria na Uchaguzi wa Viongozi wa Serikali za Mitaa.
Vyama vya Siasa kwa upande wao navyo huendesha chaguzi ambazo zinajulikana kwa jina la “Chaguzi wa Msingi” zinazotumika kuwachagua wateuliwa wa vyama katika aina za uchaguzi ambazo zimetajwa hapo juu.
Endapo Tume haitaridhika kabla ya kutangaza matokeo ya uchaguzi kwamba kulikuwa na kutokufuatwa kwa taratibu, matumizi mabaya au ukiukwaji wa taratibu za uchaguzi au pale ambapo kura za wagombea waliopata kura za juu imelingana, Tume itasimamisha au kufuta uchaguzi au sehemu yoyote ya uchaguzi na itatangaza siku nyengine ya kurudiwa kwa uchaguzi huo.
Chama cha ACT-Wazalendo kimesema kitashiriki Uchaguzi Mdogo wa Jimbo la Muhambwe, ambalo liko wazi baada ya kifo cha Astashasta Nditiye ambaye alikuwa mbunge mteule wa jimbo hilo
Wamesema hauwezi kusimamisha shughuli zote kwa sababu ya kusubiri jambo moja. Hivyo watashiriki Uchaguzi huku...
ACT Wazalendo kusema watashiriki uchaguzi Kigoma kumpima Rais ni kuuadaa Umma wa Watanzania. Juzi wameshiriki uchaguzi Zanzibar, je walikuwa wanampima Rais?
Je, Rais ni msimamizi wa uchaguzi? Ni vyema wawe na msimamo tu kwamba Kama walivyoshinda Zanzibar ndivyo watakavyoshiriki uchaguzi huko...
Huenda uchaguzi mkuu wa mwaka jana umeleta funzo kwa vyama vya upinzani. Maana sasa wanaonekana kupata funzo.
Jambo ambalo wanatakiwa kutambua ni kuwa tume huru ya uchaguzi ambayo itaendesha chaguzi kwa uwazi na ukweli bila upendeleo inahitaka.
Tangu mwaka 1995 walipaswa kususia uchaguzi kama...
Katika hili la kutoshiri uchaguzi mimi nakubaliana kabisa na Chadema kwamba wamefanya maamuzi sahihi.
Kwani wale wabunge 20 wa Chadema mule bungeni wanafanya kazi gani yenye maslahi kwa upinzani. Wao muda wote wanarandaranda na viongozi wa CCM akina babu Tale.
CHADEMA komaeni hivyo hivyo hadi...
Nimemsikiliza huyu Prof nguli wa sheria toka nchini Kenya akizungumzia juu ya uzalendo wa hayati JPM juu ya kuwa kiongozi aliyekuwa kada wa CCM. Na kwa mujibu wa Prof Lumumba anadai CCM ni chama kinamchomuenzi hayati Julius Nyerere ndio maana kinakuwa kinahakikisha kuwa rasilimali za taifa la...
Chama cha CHADEMA kimesema hakitashiriki uchaguzi mdogo wa ubunge jimbo la Muhambwe lililopo wilayani Kibondo Mkoa wa Kigoma.
Jimbo la Muhambwe liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge Atashasta Nditiye kufariki dunia Februari 12, 2021 katika Hospitali ya Benjamin Mkapa mkoani Dodoma alikokuwa...
Hili sina huruma nalo. Wananchi walio wengi huingizwa kwenye mkenge na viongozi hawa wa upande wa vyama vya upinzani na hata kuthubutu kuwaambia waandamane. Hivi sasa wamekaa kimya huwasikii kabisa na hata ukiwasikia sauti zao ni kama vile unatafuta station ya redio kwenye shortwave2...
Mbunge akiteuliwa kuwa Makamu wa Rais anakoma kuwa mbunge.
Hivyobasi, Dk. Philip Isidori Mpango atakapo apishwa kuwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania atakoma kuwa mbunge wa Jimbo la Uchaguzi la Buhingwe lililopo Mkoani Kigoma, haya ni matakwa ya masharti ya Ibara ya 47 (6) ya...
Najua watu wenye Nia njema wamekua wakiomba kwa uwazi ama kwa kificho kuhusu haki mbalimbali za kisiasa hapa Tanzania.Mimi Ni mmojawapo niliyeomba kivyangu ili Mungu afanye mabadiliko bila vurugu Wala madhara.
Mambo Ni hatua kwa hatua.
Katika uchambuzi wangu pamoja na maombi naona yafuatayo...
Katika mchakato wa kupata Rais wa JMT, katiba inaelekeza kuwa ni lazima kuwe na mgombea mwenza ambaye Rais akishinda uchaguzi then mgombea mwenza huyo anakuwa Makamu wa Rais.
Nikiri kuwa sikuwahi kuchukua cheo cha Makamu wa Rais kwa uzito mkubwa. Mara nyingi niliona kuwa makamu wa Rais ni takwa...
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron ametahadharisha juu ya Uturuki kuingilia kati katika uchaguzi wa rais nchini Ufaransa mwaka ujao.
Ameituhumu serikali ya mjini Ankara kwamba inaeneza uwongo kupitia vyombo vyake vya habari. Akihojiwa na kituo cha televisheni nchini Ufaransa cha France 5, Rais...
Marehemu Raisi Magufuli ameondoka na kaiwacha nchi katika sintofahamu ya manunguniko ya matokea ya uchaguzi ,tunaweza kusema ameiwacha nchi wananchi wake wakiwa ndani ya mgawanyiko mkubwa sana unaofukuta.
Ninavyoamini hata kama uchaguzi usingekuwa na mizengwe bado CCM wangeibuka videdea kwa...
Kiongozi wa upinzani nchini Jamhuri ya Kongo (Congo-Brazzaville) na mgombea wa kiti cha urais amefariki kwa COVID-19 ikiwa ni saa chache tu baada ya vituo vya uchaguzi kufungwa.
Guy-Brice Parfait Kolelas alifariki akiwa kwenye ndege akipelekwa nchini Ufaransa kwa matibabu baada ya kuumwa. Saa...
Kigoma kuna jimbo moja la uchaguzi liko wazi baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo ndugu Nditiye kufariki dunia.
Kwa kuwa Rais mpya mhe. Samia Suluhu amesema tushikamane na tuache kunyoosheana vidole, ndio najiuliza Chadema watashiriki uchaguzi huo mdogo?
Maendeleo hayana vyama!
Lazima mfumo wa uchaguzi wa Rais kizamani ambao hauendani na misingi ya kidemokrasia usiwepo tena hapa Tanzania.
Kama kuna mgombea Urais ambaye hajaridhika na matokeo basi kuwepo na utaratibu wa kupinga hayo matokeo mahakamani. Ili kuhoji uhalali wa aliyeshinda.
Kuishi na taifa amabalo baada...
Waliojitokeza mapema kabisa kutia nia ni pamoja na Kamanda Elizabeth Mwakipesile ambaye kwa sasa ni Mwenyekiti wa Bawacha wa Mkoa wa Mbeya, Huyu yeye ametia nia kwenye nafasi ya Makamu Mwenyekiti Bara.
Nako kwenye nafasi ya Mwenyekiti wa Bawacha Taifa amejitokeza mzito mwingine anayeitwa...
Huyu kijana aliponzwa na ndoto yake ya kugombea Udiwani , kosa lake hilo la kutumia haki yake ya kikatiba la kugombea udiwani limemsababishia kutengenezewa kesi ya Mauaji , ambapo baada ya kukamatwa kama maagizo yalivyoelekeza mgombea udiwani wa ccm kwa kasi ya radi akashinda bila ya kupingwa ...
Baraza la wanawake wa Chadema (BAWACHA) , limetangaza rasmi kuanza mchakato wa kujaza nafasi za Wasaliti waliotimuliwa ndani ya Chama wakiongozwa na Halima Mdee.
Fomu za Kugombea nafasi hizo za uongozi wa Bawacha Taifa zinapatikana kwenye ofisi za Mikoa za Chadema, ofisi za Kanda zote na ofisi...
DHAMIRI YAMLAZIMISHA RAIS MAGUFULI KUKIRI UHARIBIFU KATIKA UCHAGUZI WA OKTOBA 2020!
Nilipokuwa nahojiwa na Jeshi la Polisi jijini Dar es Salaam wiki iliyopita, nililazimika kumueleza mmoja wa maofisa waliokuwa wananihoji nikasema kuwa Uchaguzi Mkuu wa Oktoba 2020 haukuwa Huru na wala haukuwa wa...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.