Rais Samia Suluhu Hassan amesema kuwa Tanzania haitajengwa na mtu mmoja au chama kimoja bali itajengwa na Watanzania wote.
Rais Samia ameeleza hayo Jumanne Aprili 5, 2022 Jijini Dodoma wakati akizindua mkutano wa Kituo cha Demokrasia Tanzania (TCD), unaojadili maridhiano, haki na amani...