Recent content by macho_mdiliko

  1. macho_mdiliko

    Tumalize utata jamani , Ha, Kinga, Chagga, Sukuma? Nani namba Moja kiutajiri!?

    Uko sahihi. Watu wanaotoa shutuma za kuwepo utajiri wa dawa, mara nyingi ni kujiliwaza na kutokubali kuwa wameshindwa kujikwamua. Hakuna madawa yanayoweza kukuletea utajiri.
  2. macho_mdiliko

    Zipi sababu zinazozuia gari za Masoud Kipanya kuanza kutumika

    Wabongo tuache utani. Mtu anaunganisha ma-vyuma na mota ya umeme halafu mnataka auzie watu? Hamwoni ni hatari kwa watumiaji wa barabara na magari yao? Ameshalipitisha kwenye test. Yeye analitumia? Tunapenda sana wagunduzi lakini siyo kwa kulazimisha.
  3. macho_mdiliko

    Mafwele amesaidia kupatikana Madereva waliodhaniwa kutekwa

    Hawani wajinga kabisa. Nadhani wameachiawa kwa masharti ya kusema hivyo na kumsifia. Kweli nchi imefika kwenye level ya juu ya ushetani.
  4. macho_mdiliko

    Yeriko Nyerere: Najutia kuwahi kuwa Mwanachama wa CHADEMA

    Mkuu huyu jamaa ni nothing, hata CHADEMA hakuwa mtu muhimu. Huyu hata huko CCM wanamdharau wanajua kabisa hana ushawishi. Huyu ni mpiga domo tu hata elimu yake ni ndogo sana.
  5. macho_mdiliko

    Kikwete alijua kula na upinzani, Samia anataka kula kwa upanga

    Magufuli hakufikia kiwango cha sasa cha utekaji na mauaji. Na victims wengi walikuwa ni kweli watu wabaya, wenye rekodi chafu. Ni wachache kama kina Lissu ndiyo unaweza kuwatofautisha.
  6. macho_mdiliko

    Kikwete alijua kula na upinzani, Samia anataka kula kwa upanga

    Wewe ndiye umegonga penyewe. Kikwete hana lolote, na alikuwa ana deal na kina Mbowe ambao walikuwa kwenye siasa kutengeneza fedha. Na pia asingethubutu kuleta ujinga wa sasa kwa sababu kina Mkapa walikuwepo na tena walikuwa na ushawishi mkubwa.
  7. macho_mdiliko

    Kikwete alijua kula na upinzani, Samia anataka kula kwa upanga

    Mkuu, Kikwete siyo smart kama unavyodhani. Ni kuwa alikuwa hajui kama unaweza kutawala kibabe kwa kuua na kuteka na watanzania wakakuangalia tu. Baada ya Magufuli kuonyesha njia yeye sasa anafanya zaidi. Halafu kingine... wakati wa utawala wake bado CCM ilikuwa na watu wazito wenye ushawishi...
  8. macho_mdiliko

    Soon wanasuguana hapo juu

    Jamaa fix sana huyu. Watu wanaongelea kimama kutaka kujiongezea muda yeye analeta jambo ambalo haliko kabisa. Hii fi-si-em ya sasa ikuache utengeneze mtandao? Mkwere kashika usukani kikamilifu na rais wa mawe anajua hatari iliyopo kama atathubu kuleta fyoko. Sana sana anaugulia ndani kwa ndani tu.
  9. macho_mdiliko

    HOJA Baba yangu alichukuliwa na waliojitambulisha kuwa Askari Polisi, hajaonekana tangu Oktoba 23, 2026

    Mtu anapokamatwa inatakiwa kila kitu kiwe wazi... anakamatwa kwa kosa gani na anapelekwa wapi. Hata haya mambo ya kupita kwenye vituo kuulizia, siyo sahihi japo raia wengi wameshazoea. Tatizo kubwa lililopo sasa hivi ni kuwa vyombo vya dola vinafanya kazi kihuni, kama majambazi. Hii inatoa...
  10. macho_mdiliko

    Tatizo la Mbeya sio Bajaji tatizo la Mbeya ni barabara

    Lakini hii ndiyo ghilba ya CCM kila sehemu na kila kwenye tatizo. Tanzania ya sasa inakabiliwa na matatizo ya uongozi mbovu wa CCM yaliyojilundika kwa muda mrefu. Uongozi wa kufukia matatizo badala ya kuyatatua. Uongozi wa kukataa kuambiwa ukweli. Kuna mmoja anauliza Tulia alikuwa anafanya nini...
  11. macho_mdiliko

    Kwanini Kamari inaruhusiwa Tanzania?

    Umeuliza ''kamari'' lakini kuna wengine wanajibu ''kamali'' tena wengi tu. Kweli nchi yetu elimu ni janga. Watu wa namna hiyo ukiwapa kazi zinazohitaji umakini wa hali ya juu ni hatari sana. Nakumbuka hasara niliyopata ofisi moja, mwanangu nimemwandikisha kwa jina Maria, wao wakabadilisha na...
  12. macho_mdiliko

    Kimedani hakukuwa na sababu ya mauaji kiasi kile. Akili yangu inanituma huenda ilikuwa Kafara

    Na kuna jingine..... waliopata majeraha wakaenda kuchukuliwa hospital na kuuawa. Kuna elements za udini na kuna watu wamejiapiza wako kwenye vita vya jihad. Kinara ni mzee wa Msoga akipata support kutoka uarabuni! Kuna siku haya yatakuja kujulikana ndiyo watu wengi watashangaa
  13. macho_mdiliko

    Serikali ya CCM, imewakumbatia Wachina. Huyu Operator, Mzazi wake amefariki mwezi ulopita kwa kukoswa Pesa ya Matibabu!

    Mwafrika ni kulia lia kila sehemu. Utasikia ohoo, tukiwa China tunanyanyaswa. Haya sasa hata kwenu bado mnalia lia? Jambo ambalo watu wengi wantakiwa kulijua ni kuwa duniani usipojitambua wewe mwenyewe basi hakuna wa kukutambua. Usipojithamini wewe mwenyewe basi hakuna wa kukuthamini. Serikali...
  14. macho_mdiliko

    Ombi Maalum kwa Rais Samia, tafadhali rejesha Adhabu ya Viboko Mashuleni ili kurejesha Nidhamu na Maadili kwa Kizazi cha HATARI cha sasa

    Hizi ni hisia za kishamba kama ule ujinga wa kusema ugali ndiyo chakula kinachofanya watu wawe na nguvu. Ni ukosefu wa elimu na sterio type za wanavijiji na watu wasio elimika.
Back
Top Bottom