Zitto hawezi kuwa mgombea Urais wa CHADEMA kwenye uchaguzi wa 2015 kwa sababu hizi zifuatazo:
1. Zitto amezaliwa September 24, 1976. Hivyo, mwaka 2015 atakuwa ametimiza miaka 39 Inshallah. Katiba inasema mgombea Urais Tanzania awe na si chini ya miaka 40.
2. Zitto amechafuka ndani ya CHADEMA kama Lowassa alivyochafuka ndani ya CCM. Wakati CCM wanaweza kumchagua Lowassa kuwa mgombea wao wa Urais 2015 kutokana na upumbavu wao, CHADEMA si wapumbavu.
3. Bado Watanzania wanamhitaji na kumwamini DK. WILLIBROD SLAA. Pamoja na kuwa DK. SLAA mwenyewe hana mpango wa kugombea 2015, wito wa Watanzania utakuwa ni mkubwa sana na nadhani ataitikia wito huo.
4. Hata yeye Zitto anajua kuwa hana nafasi ya kuwa mgombea Urais wa CHADEMA, hata kama DK. SLAA akiamua hagombei. Amejiharibia mwenyewe kwa uhusiano wake wa kifisadi na Rostam Aziz na watawala wa serikalini.
5. Zitto akiwa mgombea Urais wa CHADEMA, Watanzania wengi wataamua kutopiga kura au kumpigia kura mgombea Urais wa CCM.
uzuri ni kwamba hata akigombea atashindwa vibaya sana. Na ukitokea muujiza akashinda, basi watanzania tumekwisha. Kama mlidhani mkapa alikuwa na jeuri na nyodo, you ain't seen nothing yet!! Zitto is mkapa on steroids na mimi nitafanya juu chini ashindwe na kulegea ktk jitihada zake hizo.
Nipo naangalia Taarifa ya habari, nimemuona zito kabwe akihutubia kwenye kampeni za kuomba ubunge huko jimboni kwake kigoma. Katika mkutano huo Kabwe anawaeleza wananchi kuwa mwaka 2015 hataenda tena jimboni hapo, lakini si kugombea ubunge tena bali ni URAISI. Hivi ni nini mantiki ya hii kauli kwa kiongozi mwandamizi wa chama. Je ni kauli ambayo inaleta taswira gani, Je inajenga au inabomoa?
Kwa maslahi ya nani?Anatimiza haki yak ya kikatiba
Aliingilia maslahi yako? Au alibeba ile dogox2 yako Mr NN? be open! ili na mimi nikuunge vidole:glasses-nerdy:Zitto hajui kuwa ktk siasa usiangalie mbele na kuruka kihunzi kilichopo mbele yako sasa. Badala ya kulenga ktk kushinda ubunge kwenye uchaguzi ujao yeye anaanza kutangaza nia za mwaka 2015.....to me that demonstrates poor judgment. Hafai kuwa raisi huyu kwa sababu nyingi tu.....
Kama ametanganza ni vema ametangaza mapema ili tupate muda wa kutosha kumpima... si vema kuwashtukiza watu katika suala nyeti kama hili. Lakini nilivyomsikia si kama ametoa tamko rasmi, maana alikuwa anawauliza watu waliohudhuria mkutano wake wa hadhara pale Kidahwe