Tukumbuke kuwa katika uchaguzi wa 2001 jumuia ya Uamsho ilikuwa ni mawakala (observers) wa Marekani kusimamia uchaguzi na waliwakushanyia report na takuwimu za Uamsho na zawangalizi wengine wa kimataifa zililingana ZANZIBAR
Sasa kumwambia Marekani /western kuwa Uamsho ni tishio kwa dunia yani ni magaidi hili nikujidanganya wahafidhina, maana huwezi kuwafananicha Uamsho na makundi haramu ya ugaidi kama Buharamu au Al Qaida it is fareway.
Uamsho imesajiliwa kihalali na Serekali ya Mapinduzi ya watu wa Zanzibar ambayo ina %99 ya wananchi wake ni waislamu, na maadai ya Uamsho hayahusu mizozo ya kidini maana wananchi wake ni waislamu assilia hio.
Kwa hio hakuna mivutano hapa kwetu Zanzibar ya Kidini tokea enzi hio, sera za uamsho ziko wazi na zinakubaliwa na wananchi wa Zanzibar katika kutetea na kudai haki na usawa wa nchi yetu na viongozi wetu wa smz chini ya Muungano ndio walengwa.
Laakini kwa zichukuwa Taka taka zao zenye kunuka kuzizika uani kwao basi wanataka kuzisukumiza kwengine, ndio hutafuta msada wa kufanya kama zanzibar nako kuna ugaidi ndio hukerwa na Ndevu, Majina ya Allah, viguo vifupi,etc.
Ndio ukaona huwatuma vijana wao wa Uvccm Janjawi waliowapa Mafunzo ya Udundu na kuwalicha sumu za Ubaguzi wachome Makanisa ,waibe na wavunje Bar ili wapate mwanya wazanzibar ya leo kila mtu ana simu ya mchina haaaaaa habari mpaka za giningi zinapatikana seuze za uamshoo hehee mchina ukitaka habari za space utazipata
njia pekee ya kuzuia uamsho ni kuzuiya kampuni za simu zisitoe GB za internent lakini hii ni bure sababu watu watapogiana simu ccm tizameni nini uamsho wanakidai ikilchobaki ccm magamba mubadilishe sera ili ziendane na matakwa ya watu
sera za CCM za sasa ni sera za STALIN NA LENEN wa russia ya enzi hizo kukamata watu kuuwa watu kunyowa watu ngozi za kichwa kuchoma makanisa kuchoma bar huu ni upuuzi wa kimagamba
sasa kitu cha msingi ccm fikirieni njia na sera nzuri za kudumisha muungano uwe wa kiuchumi kijamii na uweze kukabiliana na mawazo ya wakati
wahafithina wako ulimwengu wa kaburini wenyewe wako haii wanatembeekuipaka matope Jumuki .
JUMUIYA YA UAMSHO NA MIHADHARA YA KIISLAMU
(JUMIKI)
للجنة الدعوة الإسلامية
THE ASSOCIATION FOR ISLAMIC MOBILISATION AND PROPAGATION
P. O. BOX: 1266 -Tel: +255-777-419473 / 434145-
FAX +255-024-2250022 E-Mail: jumiki@hotmail.com
MKUNAZINI ZANZIBAR
.
'MOBILISATION AND PROPAGATION????
Uamsho walijisajili kama jumuiya inayohusika na mambo ya dini za kiislam. Sasa ilikuwaje wakaingia kwenye siasa? Au ndio 'Mobilisation and Progation yenyewe?
may be swahili is not your language? I'll offer you an executive swahili class, payment is negotiablewhat were you trying to say?
Wewe hufahamu na inaonesha wewe ni numb.naomba nikueleweshe chanzo cha migogoro hyo ni katiba mpya ambayo suala nyeti la muungano ndo source ya yote hayo.ccm kama kawaida wanataka serkali mbili kwenda moja na wanzanzibar wengi wao wanataka tatu,tatanganyika wamebakia walio wengi ni non-alliened.kwa hyo basi kama uamsho imesajiliwa kisheria ina haki pia kuongelea mambo yote ya kisiasa kwa sababu siasa ipo ndani ya jamii na ndo maana jaji warioba amesema makundi yote atayapitia ili kupata maoni yao juu yakatiba mpya yakiwemo wabunge,vikundi vya kidini,hata makundi ya rika tofauti.
1.uamsho hawafanani na al-qaeda au boko haram ILA BOKO HARAM LILIANZA KAMA UAMSHO
2.UAMSHO ni kundi la kidini ILA KUMBUKA KWA SASA LINAFANYA SIASA na kuiweka dini pembeni
3.uamso ichague kufanya siasa na kuomba usajili kama chama cha siasa-hii itawalazimu viongozi wake wabadilike na kusimikwa viongozi wenye ELIMU DUNIA na sii elimu ahera.
4.Uamsho kwa kukosa viongozi makini walitumia mbinu za KIGAIDI ili kuleta vurugu zenji.FARID eti alitekwa na hata kibao hakupigwa.huu ni uongo tunavyoijua nchii hii jamaa angerudi na maumivu tele.FARID aliibuka kutoka mafichoni kabla ya deadline ya masaa waliyotoa uamsho serikalini nia NI KUWAONESHA WAFUASI WAKE KUWA SERIKALI INAMWOGOPA IMEMWACHILIA. serikali sasa imeamua kuuonesha ulimwweng kuwa farid ni ndulele
5.NAIPONGEZA SERIKALI YA CCM KWA NAMNA ILIVYOAMUA KUPAMBANA NA UAMSHO NA PONDA ila inggekuwa rahisi sana LOWASSA angekuwa rais angetoa amri moja tu. nayo ni risasi mmoja maiti mmoja kisha dumbukiza maiti baharini
umeweka points zako kutoka kinywani mwako bila ushahidi wowote.
Msikilize huyu padri anasema nini
Na Lilian Nyenza
Kanisa halitaacha kutoa mwongozo kwa watu wake hata kwa mambo ya kisiasa ukiwamo uchaguzi kwa kuwa, siasa bila dini ni sawa na uendawazimu.
Aidha, imedaiwa kuwa tabia ya kuwalaghai vijana kuwa ni taifa la kesho, ndiyo inayowadumaza kiakili na kuwafanya watumiwe na wanasiasa kufanya fujo, badala ya kujitokeza kuongoza kwa kufuata taratibu za nchi.
Mkurugenzi wa chama cha kifamilia cha Undugu Association Tanzania, Padri Baptiste Mapunda, alitoa kauli hiyo katika sherehe za kuuaga mwaka 2004 na kuukaribisha mwaka mpya wa 2005, zilizofanyika katika ukumbi wa Parokia ya Mt. Yosefu, Jimbo Kuu Katoliki la Dar es Salaam.
Mkurugenzi huyo wa UNDUGU ASSOCIATION TANZANIA alisema kuwa, Tanzania imeanza kuonesha dalili mbaya za machafuko kutokana na baadhi ya watu wakiwamo wanasiasa kuweka mbele ubinafsi.
"Tukikaa kimya huku mambo yanaharibika katika jamii; eti tuwaachie wanasiasa wafanye watakavyo, tutakuwa hatutendi wajibu wetu na hivyo, Kanisa halitaacha kusema ukweli kwa maslahi ya umma hata kama unamkera mtu.
Hii ni kwa kuwa tunajua wazi kuwa siasa bila dini, ni uendawazimu ambao mtu hajui akifanyacho kwa kuwa akili yake haijatimia kiroho." alisema.
Aliitaka jamiii ya Kitanzania ijifunze thamani ya amani na siasa safi kutokana na hali ya amani na usalama katika nchi jirani za Rwanda na Burundi ambayo ni hatari na inasikitisha.
Alisema vita na mauaji yanayoendelea katika nchi hizo, yanasababishwa na uroho wa madaraka wa watu wachache ambao hawajali utu wa wengine.
Aliongeza kuwa, "Siku zote tunapaswa kukumbuka kuwa, amani na mapendo ambayo Mungu ametujalia, tunapaswa kuyaenzi sisi sote kwa kuwa siasa bila dini, ni sawa na uendawazimu."
Padri Mapunda aliiasa jamii kuendelea kumuomba Mungu ili azidi kuwajalia amani,upendo na utulivu uliopo sasa, kuwa uwepo hata baada ya Uchaguzi Mkuu kupita.
Amewataka Waamini kuwaombea viongozi wanyanyasaji kama Herode, wabadilike na hivyo, kuongoza nchi kwa haki na akawasihi Watanzania kuyashinda maovu kwa kutenda yaliyo mema.
Hata hivyo, Padri Mapunda amewatahadharisha vijana kujiepusha kutumiwa na baadhi ya viongozi wa siasa, kwa nia ya kufanya fujo katika uchaguzi.
"Vijana mara nyingi wamekuwa wepesi wa kurubuniwa na vijizawadi vidogo vidogo, ili wafanye kile wanachokitaka wanasiasa wabinafsi. Sasa mimi nasema mkae chini na mlitafakari hilo kwa makini.
Mtakao angamia ni ninyi na si wao," alitahadharisha.
Alisema vijana ni Taifa la leo na Taifa bila vijana limekufa, hivyo aliwasihi kuwaheshimu wazazi na walezi ili wapate kuishi maisha marefu na yenye heri duniani, kama walivyojaliwa kuuona mwaka huu mpya.
Naye Mwenyekiti wa Umoja huo, Bw. Benjamini Komba alisema, lengo la Shirika la Undugu, ni kuiunganisha jamii, ikiwa ni pamoja na kuimarisha Ukristo katika kupata hamasa katika kazi ya umisionari, ili ijengeke roho ya umisionari wa kweli nchini Tanzania.
Bw. Komba alisema kuwa, Shirika limekuwa na mchango mkubwa kwa jamii, kwa kuwa ni chombo cha kuelimisha jamii na kuendeleza mawasiliano na wamisionari wa Afrika ambao wapo ndani na nje ya nchi kwa lengo la kusukuma mbele kurudumu la Injili katika Taifa hili.
Umoja huo haujishughulishi na mambo ya siasa na hauna ubaguzi wa dini, rangi, imani wala itikadi.
Katika sherehe hizo, Wanaundugu na watu wengine walialikwa na kuhudhuria pamoja na familia zao.