Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,281
- 44,793
Wee jamaa wewe...
Mbona mungu amekujalia sana??
Mtu mmoja vipaji lukuki.
Napenda riwaya na mashairi yako...
Nafikiria namna ya kuyakusanya yote,
kisha niyahifadhi katika maktaba yangu.
[FONT=Times New Roman, serif]TUNDA[/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelitungua, chini puu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nikalichukua, mikono juu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda ninalingatua, utamu huu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda ninalilambua, uhondo mkuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda linanizingua, kwenye miguu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelibanjua, kwa utunduu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nililotungua, ni jekunduu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelichambua, ni tamu tuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nikaliparua, bila kisuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda sitoliumbua, kwa wenzanguu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda hili siyo mua, si karafuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda langu sio bua, na si kifuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda limejichanua, uroda huu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nimelichambua, kwa mkoguu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda msijebagua, kisa wivuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]Tunda nililotumbua, sio vivuu![/FONT]
[FONT=Times New Roman, serif]na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)[/FONT]
Matunda mwitu mengine matamu na mazuri kwa afya.Lakin huku Darislamu hayapo.i hope si tunda mwitu. hongera
Wewe Charity, kumbe humo kiasi hiki karibu kwenye JF Jazz Band chini ya uongozi wa mtunga mashairi maarufu Bigirita. NimefurahiHongera nakumiminia,
Kwa juhudi nakuaminia,
Hatimaye tunda umejipatia,
Jitihada nyingi umejifanyia.
Maswali yamejaa kichwani,
Mzee Mzima tunda la nini?
Ulichelewa nini ujanani?
Na tunda hili tunda gani?
Tunda hili la mti gani
Tunda hili la mwaka gani
Tunda hili utamu gani
Tunda hili tunda gani?
hehehe, Mwanakijiji I salute you.
Tunda ukilikagua kichefuchefu kitakupata2.Ulilikagua kuona kuwa halina dalili ya mdudu ndani?
Promota unatisha!!!!Hongera nakumiminia,
Kwa juhudi nakuaminia,
Hatimaye tunda umejipatia,
Jitihada nyingi umejifanyia.
Maswali yamejaa kichwani,
Mzee Mzima tunda la nini?
Ulichelewa nini ujanani?
Na tunda hili tunda gani?
Tunda ni tamu mchana au usiku
Tunda linatia kiwewe zaidi usiku
Tunda linazua magomvi kila siku
Tunda ni tamu zaidi ukililamba
Tunda ni tamu ukipiga jaramba
Tunda ni tamu zaidi la Tanga
Tunda ni tamu husipotangatanga
Tunda ni la mmoja si la umoja
Tunda si la kura kama serikali ya umoja
Tunda mshirikiane ili mshibe pamoja
Mwenye kulitoa hasiudhike hata mara moja
Nimepitia ugani, fumbo sijafumbua,
Nauliza akilini, ubongo unaungua,
Jibu halipatikani, hakika wanisumbua,
Tunda hilo tunda gani, tunda ulotungua.
Tunda lako la ajabu, namna ulivyochukua,
Uhondo huo aghalabu, miguuni kuingia,
Mzee naomba jibu, kivipi uliparua,
Tunda hilo tunda gani, tunda ulilotungua.
Hongera nakumiminia,
Kwa juhudi nakuaminia,
Hatimaye tunda umejipatia,
Jitihada nyingi umejifanyia.
Maswali yamejaa kichwani,
Mzee Mzima tunda la nini?
Ulichelewa nini ujanani?
Na tunda hili tunda gani?
Afu nahisi hili tunda lipo humu JF.labda ni............Hivi wengine mbona hatuna vipaji hata vya kudonoa