Mzee Mwanakijiji
Platinum Member
- Mar 10, 2006
- 34,275
- 44,788
Na wewe unapenda MAFISADI. Na wengi wametokea huku. Wengine walitokea kwenye nyumba walizochangia na ng'ombe lakini sasa hawawezi tena kuishi humu.Na humo wanazaliwa "MAFISADI" watarajiwa wengi tu.
haya ndio maisha bora kwa kila mtanzania?
Najaribu kufikiria kama kweli wakazi au wamiliki wa nyumba hizi kweli wameridhika au wamekata tamaa. Yawezekana kabisa mtu anayeamka asubuhi kutokea katika moja ya nyumba hizo akawa ni mtu mwenye mawazo mabaya interms of kwanini wao na sio sisi???
Kwa hiyo hata mafisadi wanaozaliwa katika nyumba hizo wanapopata nafasi ya kukamata kamfereji ka ufisadi huwa wananyonya mpaka wanakausha kwani wanaamini ndio njia ya kulipiza na kujifariji.....Nadhani mvua za masika zinapofika hiyo sehemu sijui inakuwa katika hali gani jamani.....Lazima tujiangalie tena kuna tatizo mahali fulani katika utendaji kama sio akili za viranja wetu!!!
Eneo hili limo ndani ya Manispaa TAJIRI kabisa hapa Nchini, KINONDONI. Meya wake, Mstahiki Londa, ni mmoja wa matajiri wazawa wa Dar kwa sasa?
Na vipaumbele umeviangalia? Meya wa Ilala amezindua kampeni maalumu ya usafi wiki iliyopita...je Meya wa Kinondoni ana ajenda hii? Je nani anapaswa kuwajibika kwa hicho tunachokiona kwenye picha? ni manispaa, wakazi wa eneo husika? wapita njia au nani?
Maeneo mengine yalitakiwa yasiwe makazi ya wananchi. Bonge la Mpunga ni mfano halisi kabisa.
Je, lawama zingine zitupiwe kwa wale vijana wetu tuliowasomesha chuo cha ardhi? Mipango miji ni aje nyinyi?
Na ninaamini kuwa ukienda kuangalia kwenye master plan ya jiji la dar, Bonde la Mpunga halijawa indicated kama eneo la makazi
Hapo umegusia tatizo lingine....
vijislams vinajitokeza polepole kila mahali na viongozi wanaangalia na hawasemi kitu.Hivi wahusika wa mipango miji kama mpo humu JF hebu tupeni ufafanuzi ni kwani hamfanyi kazi yenu kwa makini?As professionals, mnajiskiaje mnapoona jiji/mji mnalypaswa kuusimamia unazidi kuharibika siku hadi siku? Na je, hamuoni historia itakuja kuwahukumu maana " landmarks" mnazoacha zitabaki kwenye kumbukumbu? Jirekebisheni jamani!Tusikalie kuwasema viongozi wa kisiasa tu humu JF tujiseme hata sisi wenye taaluma na dhamana.
Kazi gani unataka wafanye? Kazi kubwa sana wameshafanya. Kwani hujasikia maboss wao wanawasifia?
Profession gani unaongelea? Kuna pesa pale? Kama hakuna pesa mtu aende kufanya nini??
Umewauliza wanataka kuacha legacy gani?? Mimi najua legacy zetu kama WaTz wa kizazi hiki ni kuacha "pesa nyingi sana" (bila kujali umezipataje), nyumba ndogo za kutosha, watoto kibao wasiojuana (walau mmoja kila mtaa) na misifa kibao (angalau uwe umerushwa walau mara moja kwenye bongo flava). Sasa hiyo historia unayoongelea siyo yetu!
Lakini mwisho wa yote, sisi waathirika tunajua kuwa tunaathiriwa na mazingira yetu ambayo ni matokeo ya matendo ya watawala? Mpaka hapo tutakapojua ndio tunaweza kuanza kuongea! Vinginevyo tuache tuendelee kuuchapa usingizi!!
I like this!
mambo ya mshiko siyo? Mshiko jamani unatufikisha pabaya!Hakuna tena kujali maslahi ya taifa wala kujali historia itakuja kuhukumu vipi! Ina maana ndiyo tumeridhika au tumekata tamaa?
Kamanda naona unawatukana watu hapa...Maeneo mengine yalitakiwa yasiwe makazi ya wananchi. Bonge la Mpunga ni mfano halisi kabisa.
Je, lawama zingine zitupiwe kwa wale vijana wetu tuliowasomesha chuo cha ardhi? Mipango miji ni aje nyinyi?