Jana jioni nilikuwa natokea maeneo ya Changanyikeni. Changanyikeni ni eneo lililokaribu kabisa na Chuo Kikuu cha Dar es salaam. Nilikutana na kundi kubwa la wanafunzi wakitembea kwa mguu na wengine daladala pia bajaji. Nilizani wanaandamaa juu ya mikopo, haikuwa hivyo.
Niliamua kuwauliza nini hasa kimetokea, walikataa kuniambia nini hasa kimejili. Niliendelea kudodosa, ndipo nilipopata jibu wanatoka tution (mimi huita TUISHIENI) niliumia sana moyoni, mimi ni mwalimu ninajua madhara ya tution kwa taifa letu. Tokea kuanza kwa tution kuanzia elimu ya msingi na sekondari na sasa elimu ya juu, tumekuwa na wanafunzi wasioweza kufikiri, wasiosoma vitabu, wasiojenga hoja bali kukurupuka, wasiojitambua, wategemezi kinadharia na vitendo, watazamishwaji wa mitazamo na mambo mengine kama hayo.
Naumia sana, nilianza kuona Open University na sasa UDSM, yawezekana kabisa hili lipo kwa vyuo vya elimu ya juu vyote. Wanajamii naomba sana tupige kelele kukomesha hili. Wakati tunapiga kelele tuangalie yafuatayo:
1. Je tution chanzo chake ni nini?
(a). uhaba wa walimu
(b) Ugumu wa maisha ya walimu
(c) Ukosefu wa ajira kwa Vijana
2. Sera ya elimu ina matatizo
3.Elimu yetu ni utazamishwaji wa mawazo ya wakoloni/ mabwanyenye/ mabepari?
4. Walimu wetu ni wabobevu wa taaluma zao?
5. Msingi wa kuandaa walimu wetu ni bora
6. Je wanafunzi wetu ni wavivu
7. Turuhusu tution kwa walimu bora na sio bora walimu
8. kwa chuo Kikuu cha Dar es salaam
(a). mnalifahamu hilo
(b). tatizo ni nini?
(c). je hao ndio aina ya wanafunzi mnaowadahili?
(d). Mnawahadhili bobevu wa fani mbalimbali nini mchango wao katika hili
Wanajamii elimu ndio msingi wa taifa endelevu tusitegemee wanafunzi wa TUISHIENI waje wajenge taifa letu. Naumia sana.
Tujadiliane

makubwa! Hiyo ya open university sawa kwani wale ni kama distance learning hawapewi lecture, lakini huyu wa udsm apewe lecture, notes, reference/literature then ana muda wa kukaa tena apewe tuition? Au anapewa desa au paper? Udsm kuna mambo sasa! Yaani atafuniwe awekewe mdomoni - mh eac inakuja huko sijui tutaweza kweli?
kweli mpwa!.jamani hakikisheni hili kwanza kabla hamjaanza kuumia kichwa yawezekana mnajadili hewa hapa au uzushi.
COET! kwa hiyo ni engineering! mi nadhani sio viwango duni inayopelekea hiyo tuition ila hivyo vijisent vimewalemaza wanaendekeza starehe wakijua watapata kutafuniwa, pili hao waalimu nao njaa ya namna gani hiyo lol! Kama mwl wa Univ anashindwa kuwa creative kutafuta hela kwa njia halali kwa kutumia elimu yake je wanafunzi wake watakuwa nini?hao ni vilaza wanaitwa vidu pale coet...yani ni project ya mama mkapa kuwainua wanawake kwenye masomo ya sayansi, wanalipiwa ada mpaka accomodation na tuisheni ili kuwa-boost.
vidu kirefu chake ni viwango duni.
Lisemwalo lipo ,kama halipo.................Chukua tahadhari kabla ya hatarijamani hakikisheni hili kwanza kabla hamjaanza kuumia kichwa yawezekana mnajadili hewa hapa au uzushi.
Hivyo mtu anapoona notes alizonazo haziwezi kumfikisha sehemu anaona aende tuisheni ili apate version nyingine ambazo ni bora zaidi ndo maana kuna miaka fulani hapa mjini paliibuka majina makubwa sana ya walimu wa tuisheni wakina Mkandawile,Mama Shija....hawa ni maarufu sana among wanafunzi wa Science.Basically,sifa ya walimu hawa ilikuwa notes nzuri.
COET! kwa hiyo ni engineering! mi nadhani sio viwango duni inayopelekea hiyo tuition ila hivyo vijisent vimewalemaza wanaendekeza starehe wakijua watapata kutafuniwa, pili hao waalimu nao njaa ya namna gani hiyo lol! Kama mwl wa Univ anashindwa kuwa creative kutafuta hela kwa njia halali kwa kutumia elimu yake je wanafunzi wake watakuwa nini?
KAMA NI KWELI HAWA WAALIMU WAWAJIBISHWE HASA, WANATUHARIBIA WATOTO.
huyu mleta habari hajasema TWISHENI hiyo ni watu gani, WANAFUNZI WA UDSM, WANAFUNZI WA PRIMARY AU SEKONDARI.
kwani pale chuo kikuu kuna shule ya msingi, labda ndio hao wametoka twisheni, kwa level ya NTA sidhani kama kuna uwezekano na ekweli wanafunzi wafundishwe twisheni kama za shule ya msingi/sekondari. HAIINGII AKILINI @ ALL