Tuwape tena CCM 2015? Ila kabla ya kuwapa tujiulize wamefanya nini kwa miaka 50 tuliyowapa na tumefaidika kwa lipi? Je wenzetu tuliopata uhuru nao au baada ya sisi wako wapi?maana hawachelewi kusema barabara nzuri wamejenga mashule yasiyokuwa na walimu muindo mbinu vyuo vya kata ndege za kukodi ,tunawaza kuongeza safari za mikoani wakati wenzetu wana waza kuongeza safari za nje na idadi ya ndege.
Tuwangalie wenzetu kama Rwanda ,Kenya, Afrika kusini ,Zimbabwe na wengineo.Je Ccm bado wanatufaa ? Tunataka mabadiliko,tunataka elimu, tunataka ajira huduma bora za afya ,viwanda kilimo bora na nchi isiyo kuwa ya mafisadi .Je bado huyu mwali anasifa za kuwa mke bora? Je unaridhika na kiwango chako cha mshahara ulicho pangiwa na serekali yako? Sera za mifuko ya kijamii?
Jf najua kuna vijana wengi huku tuliangalie hili na kuchangia bila kuangalia itikadi za vyama vyetu.
Mwenzako katoa hoja yenye mantiki inayostahili kujadiliwa kwa kina!! Nadhani ni vema ungejadili hoja aliyoitoa. Lakini kwa kauli yako hii, umejidhihirisha wazi kuwa ubongo wako umejaa kimeta cha ufisadi!!Huwezi kuyaona hayo kwa vile macho yako yana utando wa siasa za majungu, vurugu na uongo za baadhi ya wanasiasa wanaopenda kufanya siasa nyembamba.
Ni kweli kabla ya kuchangia mada hii ni vema wana JF wakatafakari siyo tu bila kujali itakadi za vyama, bali na pia kutathmini kama mada yenyewe imeletwa na mtu mwenye kutaka kweli mada yake ichangiwe na watu wenye upeo wa kuchambua mambo. Binafsi naona kama mleta mada ana mawazo mgando, mawazo ambayo yamepandwa mbegu za upofu, ukiziwi, fitina, majungu na chuki binafsi. Watanzania siyo wajinga kiasi hiki, cha kutaka kuwalazimisha waseme kile ambacho wewe unafikiria badala ya uhalisia wenyewe. Watanzania wanajua kabla ya uhuru ni watoto wa akina nani walikuwa wakisoma tofauti na hivi sasa, watanzania wanajua kabla ya uhuru ilikuwa ikichukua siku ngapi kusafiri kutoka Dar es salaam hadi mikoa ya Mwanza, Mbeya, Kilimanjaro na Mtwara tofauti na leo hii ambapo mtu hutumia masaa matano tu, Watanzania wanajua kabla ya uhuru ni watu gani walikuwa wakifaa nguo za heshima tofauti na sasa hivi, Watanzania wanajua kabla ya uhuru nchi yetu ilikuwa na hospitali na zahanati ngapi na upendeleo wa huduma za tiba ulivyokuwa mkubwa. Ni watu wenye mawazo yaliyolishwa sumu ya kudharau, kubeza kila jambo, kudhoofisha juhudi za maendeleo n.k ndiyo wanweza kuunga mkono hoja yako yenye unafiki wa kutaka kwaseme tofauti n hali halisi.Tuwape tena CCM 2015? Ila kabla ya kuwapa tujiulize wamefanya nini kwa miaka 50 tuliyowapa na tumefaidika kwa lipi? Je wenzetu tuliopata uhuru nao au baada ya sisi wako wapi?maana hawachelewi kusema barabara nzuri wamejenga mashule yasiyokuwa na walimu muindo mbinu vyuo vya kata ndege za kukodi ,tunawaza kuongeza safari za mikoani wakati wenzetu wana waza kuongeza safari za nje na idadi ya ndege.
Tuwangalie wenzetu kama Rwanda ,Kenya, Afrika kusini ,Zimbabwe na wengineo.Je Ccm bado wanatufaa ? Tunataka mabadiliko,tunataka elimu, tunataka ajira huduma bora za afya ,viwanda kilimo bora na nchi isiyo kuwa ya mafisadi .Je bado huyu mwali anasifa za kuwa mke bora? Je unaridhika na kiwango chako cha mshahara ulicho pangiwa na serekali yako? Sera za mifuko ya kijamii?
Jf najua kuna vijana wengi huku tuliangalie hili na kuchangia bila kuangalia itikadi za vyama vyetu.