Tunaendelea
Makuzi yake kielimu hayakua mazuri, Gacy shule ilimshinda akaenda Las Vegas huko akaona hapamfai kwakua hakupata pesa ya kumtosheleza akaamua kurudi Chicago. Alivyorudi Chicago mwenyewe akaamua kujiunga na Chuo cha Biashara,Gacy ni mzuri katika kuongea angeweza kujitoa matatizoni kwa mdomo tu.
View attachment 2244096
John Wayne Gacy
Hivyo hiki kipaji na elimu aliyoipata vikamnufaisha ipasavyo alivyomaliza chuo akaajiriwa katika kampuni ya Nunn-Bush Shoe Company kama Management Trainee. Kipaji na juhudi vikasababisha ahamishwe kwenda kusimamia Wing ya nguo huko Springfield, Illinois.
Gacy akaanza kugain uzito kwa fujo, akapatwa na matatizo ya moyo na mgongo na akaishi nayo milele. Alivyofika Springfield alijiunga na taasisi mbalimbali zilizojihusisha na jamii. Akawa mwenyekiti wa Chi Rho Club, akawa mjumbe wa bodi ya Catholic Inter-Club Council, akawa Kapteni wa Kamandi ya Chicago Civil Defense, akawa Afisa wa Holy Name Society na akawa makamu Rais wa Jaycees na huku ndipo alitumia muda wake mwingi.
Mwaka 1964 akakutana na Maryln Myers mtoto wa kishua, wazazi wake walimiliki migahawa mbalimbali franchise ya KFC. Baada ya ndoa baba mkwe akamwambia Gacy aje wafanye kazi pamoja. Kwa wastani Gacy alitakiwa kufanya kazi kwa saa 12 lakini haikua ajabu kufanya kazi saa 14 na zaidi alijitoa kwelikweli kwenye kampuni ya mkwe akiamini watakuja kuzirithi.
Wakapata mtoto wa kiume, kisha akafuatia wa kike. Myers akabaki kulea Gacy akaendelea kujitoa kihali na mali KFC na kwenye kila taasisi aliyohusika nayo na bado alipata muda wa kukaa na mkewe.
Katika kitabu cha Clifford Linedecker, The Man Who killed Boys, amenukuliwa volunteer wa Jaycees, Charlie Hill akisema "Mara zote alionekana kuna project anaishughulikia, alijitoa mno Jaycees. Hii taasisi ilikua ndiyo maisha yake" Mwaka 1968 akaanza kampeni za kuutaka urais wa Jaycee.
Kisha minong'ono ikazuka kwamba anapoonekana Gacy basi lazima kuwe na vijana wa kiume "Gacy is gay" kabla minong'ono haijasambaa sana May 1968 Gacy akashtakiwa na Mark Miller kwa kosa la kumlaghai, kumfunga kamba na kumbaka kikatili.
Gacy akajitetea kwamba alikubaliana na Miller juu ya kilichotokea na walikubaliana kua atamlipa na akapoint kua huu ni mchezo unafanywa na washindani wake wa nafasi ya urais. Kwa status yake ni rahisi kuaminika lakini kesi ikiwa inaendelea miezi minne mbele Gacy akashtakiwa kwa kosa la kukodi kijana wa miaka 18 ili ampige Miller.
Kijana alipokamatwa akasema alitumwa na Gacy. Gacy akarudi mahakamani akiwa na kesi mbili na akapigwa nyundo 10 jela katika gereza la Iowa State Reformatory. Baada ya hiyo hukumu mkewe akadai talaka wakaachana. Gacy alijua kua akionyesha tabia nzuri paroli yake italeta matunda, miezi 18 baadaye Gacy akaachiwa kwa paroli.
Akarejea Chicago.
. . .
Akafikia kwa mama yake, kama unakumbuka vizuri nilisema Gacy alikua muongeaji mzuri. Hivyo alipata majirani kwa haraka, na kwa ule uchapakazi wakampenda.
Mama yake akafanya mpanga Gacy akapata nyumba ya vyumba viwili, mahusiano mazuri na majirani na kupata hii nyumba ilikua kete nzuri kuthibitisha amebadilika.
Gacy akaondolewa kwenye uangalizi wa paroli.
Kabla hata mwezi haujaisha Gacy akafunguliwa kesi ya kumlazimisha mvulana kufanya naye mapenzi. Kesi ikafika mahakamani isipokua mlalamikaji hakufika mahakamani.
Gacy akaachiwa.
Halafu akamuoa Carole, Carole alikua ametoka kuachika akiwa na mabinti wawili. Wote wakaenda kuishi na Gacy.
Familia ikapendwa na majirani, parties zikaandaliwa mara kwa mara. Majirani wakahudhuria ila haikufanya waache kulalamikia harufu kali iliyokua inatoka kwenye floorboards za nyumba ya Gacy.
Mwaka 1974 Gacy akafungua kampuni ya mapambo akawa anaajiri wavulana wadogo kwa kisingizio cha cheap labor ingawa ukweli ilikua ni kuwashawishi ili alale nao.
Mwaka 1975 uhusiano wa Gacy na mkewe ukawa umedorora, Carole akawa anakuta majarida ya mashoga ndani kwao na Gacy akawa na bipolar na mood swings.
Mwaka 1976 hii ndoa ikafa. Gacy akaamua kufocus na siasa, lakini njia rahisi ya kufika huko ikawa ni kupitia Jaycees.
Akawa makamu wa Rais wa Jaycees, lakini hii pia ikamaanisha anakua karibu na wavulana wengi zaidi.
Hii ikampa wahanga wengi zaidi.
Ikampa Antonucci, akamhadaa na kumfunga pingu bahat nzuri pingu haikubana mkono mmoja vizuri. Antonucci survived na akafanya kazi kwa Gacy mwaka zaidi baada ya hili tukio.
Kisha wafanyakazi wake wakaanza kupotea akaanza Johnny Butkovich, akaja Michael Bonnin, akaja Billy Carol Jr, Kisha Gregory Godzik, halafu John Szyc, akapotea Robert Gilroy.
Mwaka mbele akapotea Robert Piest akiwa nje ya pharmacy, mama yake akiwa amemfuata warudi nyumbani akamjibu amsubiri kidogo.
Robert Piest hakurudi tena.
Tukio likaripotiwa polisi, luteni Joseph akakabidhiwa kazi. Kitu cha kwanza alichojua ni Robert alifika pale pharmacy kwakua kuna mtu alimuahidi kazi.
Mtu mwenyewe ni John Wayne Gacy, Jr. lt Joseph akaenda nyumbani kwa Gacy akamtaka waende kituoni. Gacy akajibu kuna msiba wa familia atashindwa kutoka muda huo.
Baadaye akaenda, akatoa maelezo akaulizwa maswali akaondoka zake.
Kesho yake Lt Joseph akaingiza jina la Gacy kwenye database ikasoma kwamba aliwahi shitakiwa na kufungwa kwa kosa la ulawiti. Lt Joseph akachukua search warrant akaelekea nyumbani kwa Gacy.
Aliamini kama kuna sehemu Robert Piest atapatikana basi itakua kwa Gacy.
Siku 11 kabla ya krismas ya 1978 inspector Kautz akaongoza upekuzi nyumbani kwa Gacy. Wakakuta visu, kamba, bastola, beji za polisi, vidonge vya usingizi, valium, zulia lenye madoa ya damu, pete, mzani, majarida ya mashoga, nguo size ndogo kwake, risiti n.k.
Wakarudi kituoni, Gacy alivyopata taarifa akafika kituoni akiwa amefura. Akamuita wakili wake, akasomewa Miranda rights, kwa kuzingatia hiyo akagoma kuongea na askari hawakua na kosa lenye uzito wakamuachia.
Ila wakamuweka kwenye uangalizi kwa saa 24.
Wakaita marafiki wa Gacy na kuwahoji. Marafiki kwa wanachojua juu ya Gacy kazi ya askari ikawa ngumu, wakaona wanachelewa wakamkamata Gacy na kosa likawa ni kukutwa anamiliki valium na bangi.
Ambacho askari hawakujua ni kwamba siku moja kabla hawajamkamata Gacy alikua amekiri kwa mfanyakazi mwenzake kwamba alimuua Robert Piest, na siyo yeye tu ila ameua vijana karibia 30 kwakua walikua wana nia ya kumdhulumu.
Polisi wakiwa wanaendelea na mahojiano wakapeleka maabara vitu walivyovipata siku ya ukaguzi nyumbani kwa Gacy. Pete ikagundulika ni ya John Szyc, risiti ni ya rafiki wa Robert Piest.
Kisha askari wakaja kugundua kuna wavulana wengine wafanyakazi wake walipotea katika mazingira ya kutatanisha.
Kufikia hapo Gacy akakubali amemuua Robert Piest, ila alimuua kwa kujihami. Askari wakaona huu utani wakarudi tena nyumbani kwa Gacy kwaajili ya uchunguzi mwingine.
Kufikia December 28, askari walikua wamefukua miili 27 iliyokua imefukiwa chini ya floorboard ya nyumba ya Gacy. Miili mingine ilikutwa imefukiwa karibu karibu, na Gacy alisema hiyo ilitokana na siku nyingine kuua watu wawili ndani ya siku moja.
Wiki kabla ya huu upekuzi kuna mwili uliokotwa Des Plaines River, mwili ulikua wa Frank. Askari wakakuta Kitambulisho cha Frank kwenye upekuzi wa pili. Na huu mwili ukaongezwa kwenye hesabu ya wahanga wa Gacy.
Gacy akasema miili mingine ipo kwenye huo mto kwakua nafasi ya kuifukia chini ya nyumba ilikua imeisha.
Gacy alikua anamdanganya mvulana yoyote aende nyumbani kwake, atamchanganyia valium kwenye kinywaji kisha atamfunga kamba shingoni na anaanza kumlawiti huku akiikaza kamba.
Ili kuzuia makelele alikua anawamezesha chupi au boksa zao. Miili mingine ilikutwa ina boksa au chupi bado zimenasa kwenye koo.
Kesi ikafikishwa mahakamani. Wakaitwa mashahidi 60, baba wa John Butkovich akawa sehemu ya ushahidi. Gacy akataka kutumia kigezo cha mood swings na bipolar kama defense kwenye hii kesi.
Mpango ukadunda. Wanasaikolojia wote wakasema Gacy alikua mzima na akili timamu wakati wa matukio. Hivyo awajibishwe kwa matendo yake.
Baada ya wiki kadhaa za hapa na pale kuisha baraza lilitumia saa mbili tu kufikia muafaka. Gacy alikutwa na hatia, akahukumiwa kifo.
Mwaka 1994 akachomwa sindano ya sumu ili kukamilisha adhabu yake. Mwili wake ukachomwa moto na majivu yake yalimwagwa sehemu ya siri, ubongo alikabidhiwa Mwanasaikolojia Helen Morrison.