VIFAA VIWILI MUHIMU KWENYE UTENGENEZAJI WA HOMEMADE INCUBATOR
Kwa beginner anayepanga kutengeneza incubator yake mwenyewe, kuna vifaa viwili ambavyo ni muhimu kuvifahamu: Temperature Controller na Thermo-Hygrometer.
1. Temperature Controller (Digital Thermostat)
Kifaa hiki hutumika kudhibiti joto ndani ya incubator.
Unaweka kiwango cha joto unachohitaji, kisha controller huendesha mfumo wa joto kwa kuwasha na kuzima chanzo cha joto (Taa joto, heater) kulingana na settings ulizoweka.
Kwa mfano, unaweza kutumia XH-W3002 au controller nyingine inayofaa kwa mfumo wako.
Umuhimu wake:
- Kusaidia kudhibiti joto lisipande au kushuka kupita kiwango kilichowekwa.
- Kupunguza ulazima wa kuwasha na kuzima heater kwa mkono.
- Kusaidia kudumisha mazingira yanayohitajika kwa ukuaji wa kiinitete.
2. Thermo-Hygrometer
Hiki ni kifaa cha kuonyesha viwango viwili muhimu:
🌡️ Temperature (Joto)
💧 Humidity (Unyevu)
Tofauti na Temperature Controller, Thermo-Hygrometer ya kawaida haidhibiti heater wala humidifier. Kazi yake ni kukuonyesha hali halisi ya joto na unyevu ndani ya incubator.
Hivyo, kinakusaidia kufuatilia kama mfumo wako unafanya kazi kwenye viwango vinavyotakiwa.
KWA NINI UNAHITAJI VIFAA HIVI VIWILI?
Kwa kifupi:
- Temperature Controller: Inadhibiti joto.
- Thermo-Hygrometer: Inapima na kukuonyesha joto pamoja na humidity.
Kuwa na mfumo wa kudhibiti joto bila kuwa na kifaa cha kufuatilia humidity kunaweza kupunguza ufanisi wa incubator yako.
0657 923 089
Mwanza