Habari, ndugu mteja.Najua TANESCO wana matatizo mengi, lakini katika mashirika ambayo angalau yanajaribu kuja hapa JF kujibu na kutoa updates nafikiri wamejitahidi, ni kama shirika pekee ninaloliona hapa.
Na kuna matatizo mengine inawezekana yakawa ni ya kisera na kimfumo zaidi yamewapita kimo watendaji wanajitahidi lakini huko juu kabisa kunakofanyika maamuzi hawasikii.
Siku ukipiga Yas utuletee ushuhuda hapa.Kwakweli watu wakifanya vizuri tuwasifie. Hata mimi juzi nilikuwa na,shida ya Luku inagoma kuingia. Tena ilikuwa usiku, nilipiga Customer care walipokea fasta, na walinielekeza vizuri na nikapata ufumbuzi. Big up TANESCO customer care, angalau kwa sasa
Ndugu mteja,Namba yangu ni 0755282346 nipo Kerege ccm- Bagamoyo.
Ndugu mteja,Naomba nitajiwe gharama za kuunganishiwa umeme kwa umbali wa nguzo mbili?
Ndugu mteja,Katika taasisi zote za umma nchi hii TANESCO wamenyooka sana utadhani ni shirika binafsi
I wish tanesco wapewe ttcl na shirika la ndege liwe chini yao
Ndugu mteja,Hii kumaanisha bwana Lazaro Twange ni mfanisi mzuri katika kuhakikisha huduma zinatolewa kwa wakati. Lakini ndani yao hao watoa huduma ni wafanyakazi wa mkataba wa muda(Temporary Employee) tena wapo miaka 4+ kazini hapa sasa ni wakati wa kuwapigania kwa wenye mamlaka wapate ajira za Kudumu hususani waliopo kanda ya Dar na Pwani yaani mikoa ya TEMEKE, KIGAMBONI, UBUNGO, ILALA, KIBAHA,RUFIJI pamoja na KINONDONI hawa watu wanafanya kazi tena EXTRA MILES yaani hadi usiku wapo active kwa malalamiko ya wateja na utoaji wa taarifa za hitilafu za umeme.
K.k
@L Twange
@J Homera
@Vp (x-Nishati incharge)
Wavusheni Customer service officers.
Ndugu mteja,Customer Care Pamoja na watoa huduma wa Tanesko wameendana ...Pongezi kwao sana
Ndugu Mteja,kuna nyumba hizi za NHC maeneo ya Muhimbili Upanga, tulinunua umeme wa 60k, tukapata 168.4 units, mara baada ya kuuingiza umeme, metre ikasoma 68.4 units, unit 100 zimekatwa.
Tulifatilia tatizo hili pamoja na kwamba watu wa Tanesco wa dharura walifika eneo hilo la Upanga Muhimbili, lakini mpaka leo hii hatujapata jibu lolote lile na units 100 bado hazijarudi.
Ndugu Mteja, Taarifa Na. ILL112026TB-6416 imewasilishwa kitengo husika kwa ajili ya kufanyiwa kazi. Asante kwa uvumilivu wako.
Tunaomba maelekezo TANESCO
Tunashukuru kwa pongezi, tunaenda hatua zaidi katika kukupatia huduma bora.Nilipata shida kidogo nikasema ngoja niwacheki aisee nikajua watanizungusha dakika 10 hawa hapa mko poa sana mnajali