Waziri mkuu mstaafu bwana sumaye alikwenda uingereza kwa ajili ya matibabu(medical check up).
Lakini badala ya kuwa hospitalini amekuwa akizurura kwenye miji ya uingereza kuhubiri dini,kama mgonjwa aliyetakiwa kupata matibabu nje ya nchi asingekuwa na nguvu ya kuzurura kwenye miji mbalimbali badala ya kuwa hospitali au kama ugonjwa wake haukuwa mkubwa kwanini atumie pesa za kodi kwenda nje? Wakati mwakyembe anapata huduma muhimbili?
.....Hakatazwi kufanya ibada ila iwe kwa pesa zake sio kodi za wananchi.
Ina maana alijigharamia yeye mwenyewe kwenda kwenye mahubiri?lazima ubalozi ulimuandalia gari n.k
Ah eeehe!
Kama yupo huko na ana nguvu ya kutembea sidhani kama ni dhambi kupuyanga mitaani kidogo. Ulitaka aishi wodini kama asiyejiweza???
Nadhani hapa tujadili ubora wa huduma zetu za afya kiasi kwamba viongozi (watunga sera) wanaogopa na kwenda kutibiwa nje. Ila kuhusu routes zao wakishafika huko si suala kuntu sana kwani tukishatatua tatizo la wao kukimbilia nje kila asubuhi basi hilo suala la kupuyanga litajitatua automatikali.
Halafu tena unatuuliza:Sumaye afanya utapeli wa kodi yetu
Baada ya kuangalia title yako nilitegemea una information zote jinsi huo utapeli ulivyofanyika, lakini inaelekea unataka majibu humu, ndo maana unarudi kuuliza. Maybe huko ulikokuita 'kuzurura' ilikuwa ni sehemu ya maelekezo ya daktari, na nimesema 'maybe' kwa kuwa sijui na wewe pia hujui. Tukae kimya kusubiri anayejua!!!Ina maana alijigharamia yeye mwenyewe kwenda kwenye mahubiri?
Miaka 48 baada ya uhuru bado tunarudi kwa watawala wetu kwa ajili ya medical check-up! Kama mlivyotufahamisha tusiojua, medical check up si lazima uwe mgonjwa basi kwanini hawa wakuu wasionyeshe uzalendo wao kwa kufanyiwa check-up hapo nyumbani na waende nje kwa tiba tuu! Kama ni check-up ya kufuatilia tiba ya awali basi ni haki yake. Lakini na yenyewe iwe na kikomo. Mtu akiwa fit kuzunguka kuhubiri basi frequency ipunguzwe. Tuwaonee huruma wenzetu ambao hata mkunga wanamsikia redioni!
Amandla.........
Waziri mkuu mstaafu bwana sumaye alikwenda uingereza kwa ajili ya matibabu(medical check up).
Lakini badala ya kuwa hospitalini amekuwa akizurura kwenye miji ya uingereza kuhubiri dini,kama mgonjwa aliyetakiwa kupata matibabu nje ya nchi asingekuwa na nguvu ya kuzurura kwenye miji mbalimbali badala ya kuwa hospitali au kama ugonjwa wake haukuwa mkubwa kwanini atumie pesa za kodi kwenda nje? Wakati mwakyembe anapata huduma muhimbili?
,habari yake iko kwenye tanzania daima kwenye habari kuu maoni au kwenye picha za mtandao wa tzuk,com kwenye picha utamuona mheshimiwa sumaye akiwa kwenye ibada.
Hakatazwi kufanya ibada ila iwe kwa pesa zake sio kodi za wananchi.
Fundi Mchundo:
Chukua nchi. Nitaukana uraia wa kimarekani na kurudi bongo.
wewe uliyeanzisha thread ya vakesheni ya issa michuzi ulikuwa unamuonea wivu,husuda,majungu,gere au kijicho?acha wivu na majungu, unamuonea gere sumaye, hiyo ni husuda, msione mwenzenu akifaidi, acha roho ya korosho, mwache atumie. hata yeye analipa kodi, alaaaaa.
mod thread ya majungu hii, mmeiona au hadi kuireport?
Hamna haja ya kuukana. Wakinipigia kula wananchi, uraia wa nchi hata nane ruksa. Mshindwe wenyewe!
Amandla........
Mimi sijaona tatizo kwa Waziri Mkuu mstaafu kwenda kufanya medical check up UK,na sasa baada ya medical check up hali yake inaonekana ni nzuri je unategemea akae kwenye nyumba tuu alimofikia? nafikiri sio sahihi.Yeye kama Mtanzania mwingine yeyote anauhuru wa kutembea na kujionea mambo pamoja na kujifunza pia.
Kwa yeye kuchagua kwenda kanisani ni kheri na sidhani kuwa ni kosa lakini tungeambiwa kuwa anavinjari kwenye night clubs hapo kweli tungepaswa kuuliza kulikoni kiongozi mstaafu kuvinjari kwenye night clubs?