Chama cha Mapinduzi (CCM), Serikali yake na watendaji wa umma (civil servants) wanatangaza na kuhamasisha sera/kauli mbiu mpya ya KILIMO KWANZA. Taifa letu limepita katika vipindi mbalimbali vilivyopelekea kutungwa kwa sera/kaulimbiu kadhaa. Mfano Siasa ni kilimo, Kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa nk. Kauli hizo zilikuwa na mwanzilishi, msingi na msukumo wake japo hazikufanikiwa.
Hii kauli ya sasa, imeanza ghafla, ni kama mtu ametoka usingizini na kutoa kauli ndipo Serikali na CCM wakapanga siku ya kuzindua sera hiyo. Nimekuwa nikifuatilia nini chanzo na msingi wa kauli mbiu hii bila mafanikio. Viongozi wamekuwa wagumu kueleza uwazi wa sera hii.
Laghaula, leo nimepata kusikiliza kipindi cha MUVIWATA kupitia Radio Maria Tanzania 89.1FM. Kipindi hicho kimejitahidi kuweka wazi kwa sehemu na kujaribu kujibu baadhi ya maswali ya msingi juu ya kaulimbiu au sera hii.
KILIMO KWANZA ni kauli mbiu iliyoanzishwa na WAFANYABIASHARA ili kutimiza malengo yao ya kibiashara. Kauli hii haikutoka kwa mkulima wala Serikali au viongozi wa kisisa. CCM na Serikali yetu walipoipata hiyo kauli wakaichukua kama kawaida yao, bila hata kuitafakari kwa umakini na kuanza kuihubiri.
Kutokana na msingi huu, Je sera hii itasaidia kuinua kilimo? Ni nini malengo ya KILIMO KWANZA?
Naomba wenye taarifa zaidi watusaidie kuweka wazi chanzo, msingi, malengo ya kauli hii. Binafsi nipo very pessimistic kutokana na sababu nilizozitoa hapo juu.
[COLOR=DarkRed said:KILIMO KWANZA ni kauli mbiu iliyoanzishwa na WAFANYABIASHARA ili kutimiza malengo yao ya kibiashara. Kauli hii haikutoka kwa mkulima[/COLOR]
Huu ni usanii mwingine. Haifiki kokote!!! Inahitaji pesa nyingi kutekeleza hizo pillars zao. Je serikali ya awamu ya nne imejiandaa kwa hili??? Kuna programmes nyingi na bado hazijatekelezwa, kwa kukosa funding. Hata development parners were a bit shocked na kuanza kuuliza kama wana acha kutekeleza ASDP (Agricultural Support Development Programme) ambayo wanaifadhili!!! Walitulizwa kuwa KILIMO KWANZA (GREEN REVOLUTION) ni sehemu ya utekelezaji wa ASDP???!! Mimi sijui hapo tena wakuu na mipango ya nchi hii. Hii imeingia kichwakichwa!!! Politics is the dirtiest game ever!!!
2010 is just at the corner!!1 Wapiga kura wengi ni wakulima, viini macho vya kuomba kura!!
Huu ndio msingi wa kilimo kwanza, mkulima original wa Tanzania amewahi kuangaliwa na kujaliwa na mtu yoyote? Kidogo wakati wa Siasa ni Kilimo subsidy ya mbolea na pembejeo mpaka vijijini, kilimo ni uti wa mgongo wa nchi hii pale mkulima alithaminiwa lakini sasa SIJUI LABDA MAAJABU YATOKEE!!!!!!!!!!!
Chama cha Mapinduzi (CCM), Serikali yake na watendaji wa umma (civil servants) wanatangaza na kuhamasisha sera/kauli mbiu mpya ya KILIMO KWANZA. Taifa letu limepita katika vipindi mbalimbali vilivyopelekea kutungwa kwa sera/kaulimbiu kadhaa. Mfano Siasa ni kilimo, Kilimo ni uti wa mgongo wa Taifa nk. Kauli hizo zilikuwa na mwanzilishi, msingi na msukumo wake japo hazikufanikiwa.
Hii ndiyo kilimo kwanza. Maswali ya kujiuliza je, matatizo ya kilimo chetu ni nini? vipaumbele ni vipi?Date::10/1/2009Serikali yatangaza Sh58bilioni kila wilaya za Kilimo Kwanza
Na Gedius Rwiza
SERIKALI imetenga Sh 58 bilioni kwa kila wilaya kwa ajili ya kuboresha mazingira ya maofisa ugani ili waweze kutekeleza vema mkakati wa Kilimo kwanza.
Fedha hizo zitatumika kununulia magari, pikipiki na baiskeli zitakazotumika katika utendaji wa kazi za maofisa hao mashambani.
Akizungumza na Mwandishi wa habari hii, jijini Dar es Salaam juzi, Naibu Waziri wa Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika Dk David Mathayo, alisema kuwa serikali imetenga fedha hizo za kila wilaya kwa ajili ya kuhakikisha kila ofisa ugani anapata usafiri wakati wa kutoa huduma za kilimo.
Dk Mathayo alisema kutokana asilimia 90 ya watanzania kutegemea chakula kinachotoka hapa nchini, serikali imeona haina budi kuboresha mazingira ya kilimo ili kutimiza kauli mbiu ya kilimo kwanza.
Serikali imejiandaa kuhakikisha kila wilaya inapata magari na wale wa ngazi ya kata kila mmoja atapewa pikipiki na wale wanaofanya kazi ngazi ya vijiji watapewa baiskeli pamoja na kujengewa nyumba ili wawe na moyo wa kutoa huduma za kilimo kwa wakulima,alisema Dk.Mathayo.
Kuhusu watalaamu wa kilimo, alisema serikali inatarajia ifikapo mwaka 2011 kutakuwa na uhakika wa kupata wahitimu wa fani za kilimo takribani 15,000 na kwamba kwa sasa wana uhakika wa kupata wahitimu zaidi ya 2,500 kila mwaka wanaomaliza katika vyuo mbalimbali vinavyotoa mafunzo ya kilimo.
Alitoa wito kwa vijana kujitokeza kusoma fani za kilimo bila kujali kwamba watapata ajira bali ni faida hata kwa maisha yao mahali popote na kwamba mtu mwenye utaalamu wa kilimo anaweza kujiajiri mwenyewe.
Mtu mwenye ujuzi wa kilimo sio tu kwamba ajiriwe bali anaweza kuishi mahali popote na akaweza kuanzisha mashamba yake binafsi bila kumtegemea mtu, kwahiyo napenda kutoa wito kwa vijana wote kupenda kusomea masuala ya kilimo,alieleza Dk.Mathayo.
Naibu waziri huyo pia alisema serikali imetenga Sh 118 bilioni kwa ajili ya ruzuku, mbolea, mbegu na dawa ya mazao na kwamba serikali inathamini sana wakulima ambao wanajihusisha na masuala ya kilimo na imepanga kuwawezesha kuwapa ruzuku ili wafanikishe kuendeleza kilimo.
Kuhusu maandalizi ya kilimo, Dk Mathayo aliwataka wananchi kutunza vyanzo vya maji na kutunza mazingira ili kupata sehemu za kupanda mazao mbalimbali.
Hii ndiyo kilimo kwanza. Maswali ya kujiuliza je, matatizo ya kilimo chetu ni nini? vipaumbele ni vipi?
well, kwa hapa inaonekana matatizo ni magari, pikipiki, baiskeli na nyumba. Je, hii ni kweli?
Sera ya Serikali ktk kilimo kwanza inaonekana kuto mlenga mkulima moja kwa moja. Je, itafanikiwa kuleta mapinduzi ya kilimo?
My opinion, Serikali ingeweka mikakati na mipango ya kuongeza uzalishaji na tija (productivity) ktk kilimo. Baada ya kufanikiwa ktk hilo ndipo tatizo la watalaam kukosa usafiri lingejitokeza kutokana na uwingi wa uhitaji wa huduma yao. Anyway I'm done
Hivi unapoongelea mikakati na mipango ya kuongeza uzalishaji hili la vitendea kazi kwa maafisa ugani sio moja kati ya hiyo mikakati unayoongelea ya kuongeza uzalishaji?