Ni lile anaposali Spika Samwel Sitta... (KKKT Kinondoni).
Aichangia kwaya Tshs Milioni 7...
Amalizia na kuwaomba waumini kuiombea nchi kwani iko kwenye kipindi kibaya cha watu kutafutana uchawi na kuonesha hali si shwari nchini.
Zaidi tusubiri kutoka vyombo vya nyumbani kwani walikuwepo wengi. Wasipoandika tutaandika!
Hela chafu itabakia kuwa chafu. Ukiipokea wakati mwingine yaweza kukutia nuksi tu. Lakini simhukumu mheshimiwa moja kwa moja ingawa sijui kama naye ni muumini wa KKKT au kakaribishwa kwakuwa 'anazo' ili awe mwezeshaji kwa shughuli ya kwaya naye akaamua 'kutuma salaam' kwa kumalizia ili waumini waifanye kazi ya kuiombea nchi...!Hiki ni kiji part tu cha 'operation jisafishe' ya mafisadi lakini mwizi ni mwizi tu, tule hivyo vijisenti vyetu wanavyoturudishia kiaina lakini 2010 sanduku la kura lifanye kazi yake.
Hela chafu itabakia kuwa chafu. Ukiipokea wakati mwingine yaweza kukutia nuksi tu.
Kanisa lishinikizwe lirudishe hizo pesa za fisadi haraka sana, juzi juzi tu makanisa yalikuwa yanakemea mafisadi na ufisadi na kutaka JK awashughulike mafisadi. Leo wanatizama pembeni na kuchukua pesa kutoka kwa fisadi. Viongozi wa Kanisa hilo waache unafiki na kuzirudisha pesa hizo haraka sana au wazipeleke kwenye vituo vya watoto yatima.
Hiki ni kiji part tu cha 'operation jisafishe' ya mafisadi lakini mwizi ni mwizi tu, tule hivyo vijisenti vyetu wanavyoturudishia kiaina lakini 2010 sanduku la kura lifanye kazi yake.
Huyu fisadi naona ana wasiwasi mkubwa. Kanisa linastahili kuzikataa fedha zake zilizotokana na ufisadi. Huyu jamaa kwanza ni mkristo au ndiyo mfa maji...?
kanisani nao wakapokea za ufisadi, Yesu na Maria na Yosef!
KKKT ni moja ya kanisa linalosaidia masikini/yatima moja kwa moja mie bado sioni misingi ya kuzikataa fwedha hizo.