Tazara Club,
Nikikunukuu:
.....pale WINSOR BARKSHIRE IN UK jirani kabisa na WINSOR CASSTLE LILEjumba la kifalme na ngome ya empire ya waingereza nilishangaa kuona kambi kubwa ya jeshi iko katikati ya mji huo ambao unavutia watalii toka sehemu mbalimbali duniani......
Hivi umeshawahi kupita maeneo ya jeshi ya Mgulani na Lugalo siku za usoni? Je unafikiri kwa jinsi yalivyo sasa yanaweza kuwa vivutio vya watalii?
La hasha! Jeshi letu limeshindwa kuyaendeleza maeneo hayo. Ukipita upande wa maeneo ya shule ya msingi ya Mgulani, kuna vijijumba vidogo vidogo vilivyochoka tulivyoachiwa na mkoloni (humu ndimo wanakaa kuruta). Jinsi vilivyochoka, unaweza hata kuvisukuma kwa mkono mmoja na vikadondoka. Vivyo hivyo, vijumba hivyo vipo lugalo. Tena Lugalo kuna mpaka mapori pia.
Hivyo basi, hakuna shaka, jeshi limeshindwa au halina nia ya kuendeleza maeneo hayo.
Cha msingi ni kujenga ukuta kuzunguka eneo hilo la jeshi ili liwe ndani ya ngome pia kuondoa uwezekano kabisa wa ile barabara ya bagamoyo kupita katikati ya Lugalo na kuamua itumike old bagamoyo road hadi kawe mwisho then hadi junction ya kuingia tanki bovu
Tatizo ni kwamba wameshindwa kuendeleza eneo lao. Ile ardhi pale imebaki kuwa kama "raslimali iliyokaliwa na majuha wa uzalishaji." Kwa hiyo hata kama waweke ukuta au kuhamisha barabara, ishu itabaki pale pale......
Labda pengine, badala ya kuhamisha jeshi zima, wanaweza kupunguza eneo lao na kubakia sehemu ndogo tu. Size ya eneo la kama pale Mlalakuwa au Upanga ingewatosha. Yaani, wangeweza kumiliki eneo dogo tu kwa ajili ya mambo ya administrative. Lakini mazagazaga mengine yote wangeyasogeza nje ya mji.
Tena unajua, sio lazima jeshi wayaachie yale maeneo completely. Wangendelea kuyamiliki tu, halafu wakayaazimisha kwa private sectors. Halafu jeshi kwa kushirikiana na serikali wangefanya usimamizi wa uendelezaji na mazingira katika maeneo hayo.
Kwani si jeshi limejiingiza kwenye biashara mbalimbali - wamejenga kumbi kibao ndani ya ngome zao kwa ajili ya shughuli za harusi na mikutano. Isitioshe wanataka kujiingiza kwenye biashara za ulinzi huko maofisini na majumbani. Sasa kwa nini wasijiingize kwenye biashara ya land leasing, land development na real estate pia???
Suala la new Dar kuna maeneo mengi tu ya kuhamishiwa mji huko kama vile mbweni ,boko, kigamboni hadi gezaurore, chanika, chamanzi, kisarawe, etc ni plan tu halafu itekelezwe
Ni kweli.
Lakini kwa mtazamo wangu, ukiondoa Kigamboni, sehemu nyingi ulizozitaja zinafaa kuwa sehemu za makazi, badala ya sehemu za ofisi, biashara, na vivutio.
Lugalo na Mgulani ni sehemu ambazo zinaweza ku-shift focus ya city center kwa kiasi kikubwa. Zinaweza kabisa kufanya Dar ionekane kama ina city center tatu, na kufanya jiji zima lionekane kubwa zaidi. Ni kama vile unapotundika mirror dining room . Ile reflection ya lights za chandelier inafanya dining na living room zionekane kubwa zaidi. Kwa hiyo, Lugalo na Mgulani zinaweza kabisa kuwa reflection ya Dar Chandelier (downtown Dar).