Pundit,
Nimeambatanisha vipengele ambavyo vinatumika kibunge kudai kuondolewa kwa Spika na Waziri Mkuu. Pamoja na kifungu hiki cha Katiba kuwa "vague" lakini wao kwa madaraka waliyopewa wana wajibu mkubwa sana kuhakikisha Katiba inalinda na kipengele kama hiki kinalindwa.
Kosa lao ambalo mimi nalizungumzia ni kushindwa kulinda katiba na inabidi vipengele vya kuwaondoa madarakani vitumike ni masuala ya Uhujumu uchumi ambayo ama kwa uzembe au utashi binafsi na hasa kisiasa Spika na Waziri Mkuu hawakufanya maamuzi ya msingi kwa manufaa ya Taifa.
Suala la Buzwagi, Richmond, BOT na hata ATCL, hayakutolewa uamuzi mkali na mahiri wa kiutendaji kwa kuitia katiba au kanuni za Serikali na Bunge.
Spika alisitisha kusikilizwa hoja za Buzwagi na BOT. Waziri Mkuu akaridhia kupuuzwa kwa kuundwa kwa kamati za Bunge kuchunguza tuhuma za Uhujumu.
Kushindwa kwao kufanya kazi zao kulinda uchumi, katiba na sheria za nchi ndio vigezo tosha vya kuwasilisha hoja za kutokuwa na imani na uongozi wao na hivyo kupigiwa kura ya kuvuliwa madaraka.
Game Theory,
Ni haki yako kutokukubaliana na mimi. katika vita hii ya Uhujumu na Ufisadi, kuna njia nyingi za kufanya. Hapa JF tumezoea kupiga kelele na kuvimbisha mishipa ambayo hupasuka kila wiki na kila Nyeti mpya zikija, basi hakuna cha kufanyia kazi wala nguvu kuzivunja.
Kumuondoa Spika na Waziri Mkuu ambao ni viongozi wakuu wa Serikali ni mwanzo wa kusafisha uozo uliopo. Wateuliwa wa Uwaziri na Ukuu wa mikoa ni hiari ya Rais kuwafukuza. Waziri Mkuu pamoja na kuteuliwa, yeye huthibitishwa na Bunge na hivyo kiti chake ni "ruksa" kupigiwakura ya kukosa imani hivyo kumpasa Raisi wawasilishe jina jipya kwa nafasi hiyo.
Spika naye ni hivyo hivyo, Katibu wa Bunge akipata muswaada, huuwasilisha Bungeni na kura hupigwa.
Tunachotaka si kumwajibisha Spika na Waziri Mkuu pekee, bali Bunge zima la Jamhuri ya Muungano kama litakuwa na azma ya kutetea maslahi ya nchi na si ya chama.
Hoja au miswaada hii ya kutokuwana imani inaweza kutolewa n mbunge yeyote yule na hata kama Chama tawala kitageuza mkao na kufanya kikao cha chama na kutupilia mbali hoja huku wananchi wakiwa na ushahidi tele wa uzembe na Ufisadi, basi jua safari ya CCM 2010 haitakuwa salama!
Huu ni mwanzo tuu, usikate tamaa!