-- Naomba uvute subira, nitashiriki kutoa mawaidha yangu baadae katika maswali uliyo ambatanisha.Je, mabadiliko haya yanaathari zipi katika ndoa, ...na je? njia zipi zinafaa kuepusha migogoro, ili mume nawe 'ujisikie/ajiskie ni mwanaume' nyumbani kwenu?
...
Mjue mchumba kadiri inavyowezekana na zingatia anachokuambia, kama unakubaliana na matakwa yake, iwe ni lifetime commitment. usijemchanganya tena baadae eti sikujua utapanda cheo, au utang'ang'ania kupeleka watoto international school. etc.
Believe me hii ni migogoro ambayo haina solution kabisaaaa.
bora kujihami mapema.
JADILINI MITAZAMO YENU YA FEDHA KABLA YA NDOA.
Heshima zenu wakuu
baada ya kufunga ndoa ( na kipindi chote cha uchumba) mume wangu alikuwa na income kubwa kuliko mimi na yeye ndio alikuwa kiongozi wa maswala ya budget, hilo halikuwa tatizo kwangu wala kwake
baadae nilipandishwa cheo kazini mshahara wangu ukawa mkubwa kumzidi. kwa bahati mbaya kifedha mambo hayakwenda vizuri upande wake, kipato chake kika pungua kiasi cha kutoweza ku support familia,
mume wangu akakosa raha, kukawa na dalili za insecurity upande wake.
Ili kuepusha migogoro, nikawa nampa mshahara wangu ili aendelee kuwa incharge kama ilivyokuwa mwanzo. kwa kweli ilisaidia sana
kwa mtazamo wangu, mume akiwa na inferioty complex kwenye maswala ya pesa, migogoro haiwezi kuepukwa.
Hizi changes za mshiko zinaleta songombingo sana mama akiwa nazo njulu nyingi na wakati huo mume kalamba galasa katika kipato.
Nyumba nyingi wamezoea kuona Dingi ndo incharge wa masuala ya kuhudumia kila kitu,sasa masuala yanapomwendea vizuri mama kumkatia baba kidogo kidogo,hapo ndipo sokomoko.
Mbali kwamba ndoa ni penzi na pendo lakini si rahisi kwa afrika mume ambaye ni hoi kifedha kuoa mke ambaye ni kibopa,lakini ni rahisi mume kibopa kumwoa dada ambaye ni hoi katika kipato na mambo yakawa shwari.
Cha msingi naona mapato ya mme na mke yawe wazi kwa wakati wowote hata wa kupandishwa vyeo kwa kila mmoja wao.Lakini ikiachwa kuwa mme ahudumie maana mke ni msaidizi ndipo gogoro linazuka
Nadhani Mwanaume akubali tu kwamba the Woman is slightly higher than he is na mwanamke has to maintain her role in the family and having selfrespect as well as respect to the husband.
For as long as love exists.
Love conquers all boundaries.
kwa kweli ikiwa mke ndo anakipato kikubwa dhidi ya mume..lazima mume atakuwa na ile inferiority complex..muhimu ni wewe mke kutoonyesha kiburi na kufanya wajibu wako as a wife..kiburi na majivuno kando as Kevo said hapo juu
Akiwa mwanaume mwelewa atazidisha bidii kutafuta sources nyengine za pesa ... mwanaume hasa ... rijali kabisa hawezi kupokea hela ya mwanamke .....
Mimi naamini kuwa mwanamme anatakiwa siku zote kuwa na kipato kikubwa kuliko mwenzi wake. Ni mabibi wachache sana ambao watamrespect mme wake kama huyo mme ni inferior in terms of income. So you need to work hard to beat her otherwise that relationship is gonna die, period!
...naimaomari, 'natanzika' na hii statement kwamba mwanaume akiwa rijali kabisa hawezi kupokea hela ya mwanamke,
Kwanini!???? nini inakupelekea wewe binafsi kufikiria hilo, i.e kama mwanaume umemzidi uwezo, kwanini unaona si sawa yeye kupokea pesa yako?
Au kwa tafsiri yako, mwanaume rijali kabisa ni yupi huyo?
Wana JF
Naomba ruhusa kwanza ya kubadili equation yetu.Ingawa mantiki ya mada itabaki kama ilivyo:
PENZI=MGOGORO + KIPATO
Penzi litadumu pale tu iwapo migogoro kama sio mgogoro utakapoweza/itakapoweza kutatuliwa na fedha au kipato kilichopo.
Mgogoro au migogoro naitafsiri kama majukumu katika ndoa.
Majukumu yale yanaposhindwa kutekelezeka yanabadilika jina na kuwa MGOGORO.
Ili muweze kuwa na KIPATO kizuri individually na kama couple ni lazima kwenye PENZI kusiwepo na Mgogoro au Migogoro.That is:
KIPATO=PENZI - MGOGORO
Mchongoma, once again, topic close to my heart, BRAVO!!
-- Naomba uvute subira, nitashiriki kutoa mawaidha yangu baadae katika maswali uliyo ambatanisha.
Thanks
SteveD.