Mwacheni mzee wa watu alale pema peponi, hili la Kikwete liko ndani ya uwezo wenu sio mungu wala Nyerere ndio wanaohusika.
Nivyema mkakubali wajibu wenu na kusimamia ya kwenu bila kumtegemea yeyote, sio mzungu wala mchina. Mnashindwa nini kumfata Kikwete na kuzungumza nae uso kwa uso kwanza kabla ya kuanza kulalamika. Mmelalamika sana kwa miaka yote ndio mfahamu pia inawezekana njia mnazotumia kutatua matatizo yenu sio sahihi.
Ipo njia nyingine ya kumaliza matatizo yenu sio kulalamika wala mgomo hizi ni za muda mfupi tu, umizeni vichwa kutafuta njia sahihi na sio kulalamika kila kukicha, mmelalamika sana inatosha.
Nyelele wakati wake umepita, huu ni wakati wenu goma liko uwanjani timbwilikeni. Kulalamika ni dalili za woga kama Kikwete sio basi atafutwe na achanwe live uso kwa uso, sio kujificha na kutupa maneno na kusingizia Nyerere. Mliambiwa kuweni myaone, sasa mnayaona sio magorofa ni Maisha.
Majibu ya matatizo yenu mnayo wenyewe, Nyerere keshamaliza ya kwake haya yenu. Manake dunia ilikuwepo kabla ya Nyerere na itaendelea kuwepo baada ya Nyerere.