Tatizo hawa wajamaa wanajiona ni wao tu yaani wanavyojiona ni sawa na inavyojiona CCM hapa Tanzania ,lakini wanasahau tu ngoma ikivuma sana ujue mwisho wake itapasuka tu na kama unavyoiona CCM imejaa nyufa zinazoashiria ndio mwanzo wa kupasuka basi na hawa naona wapo njiani ,kama utakumbuka ilikuwepo Jambofurums jinsi ilivyokuwa ikivuma tulisema sasa mambo mazuri na Mtz amepata pa kujifaragua kufumba na kufumbua haijulikani hata ilipokufia ,katika kujikurupusha na kuonyesha kuwa mambo shwari wakavumbua kuwa wamebadilisha jina na sasa ni jamiiforums ila wamesahau kitu kimoja kumalizia Ujamaa na kujitegemea.Mwiba si topic tu ya Kesho ni mwisho wa dunia iliyoondolewa zipo nyingine zilizopata dhoruba hiyo pia. Nashukuru umeliona hili, imagine ukiuliza unajibiwa 'sasa tufanyeje'. Nafikiri sisi ndiyo tunaifanya JF kwa kutumia hata muda kuandika, kusoma na kuchangia ni lazima tulitambue hilo.
Pole mkuu, JF ndivyo ilivyo....!Yaani hata wakiulizwa kwa nini wameondoa ile jokes katika sehemu yake nakuhakikishia watakuja na jawabu utumbo mtupu,hilo halina upinzani kabsaa ,ila sishangai sana maana ndio kazi yao inayowapatia tonge.
Hizi tuhuma ni nzito naomba wahusika wazijibu..Nimefuatilia kwa karibu ,kumbe nimeambiwa ukionekana hapa ni mkandiaji wa CCM siku hizi tumazokaribia uchaguzi basi utakachoandika kinaondolewa na wameambiwa wasichague ni wapi au topiki gani ,amri waliyopewa ni kuiondoa topik ya wapinzani wa Chama Tawala.
Kama ukiangalia kule kwenye jukwaa la siasa topiki karibia zote ni za CCM iwe inaponda au inaunga mkono mradi iwe ni ya CCM ,na elekeeni kule kwenye jukwaa la siasa, muone hakuna Chadema wala CUF ni CCM na kama utaiona basi hiyo ilikuwa kabla ya amri kutolewa toka kwa wakubwa zao. Inawezekana kabisa wakajitetea lakini ukweli wamepewa amri ,haina haja ya kusema nani katoa amri maana hali yenyewe haihitaji mwenye macho hata kipofu akipapasa kwa kuuliza ili asomewe yanayojiri ataambiwa hapana topiki inayohusiana na harakati za vyama vya upinzani zote zinaihusu CCM.
Nawapa pole sana.
Hizi tuhuma ni nzito naomba wahusika wazijibu..
hahaha!dude vipi,upo masaki?