Hakika nakubaliana na Shy, Jumanne nilisikia BBC Swahili wakitangaza kuhusu ihub,na tunajua Ushahidi imepata umaarufu kote duniani - si kitu cha ajabu ni idea iliyozaa software yenye practical use katika global scale.
Taznania tunakosa focus na priority ya nini muhimu cha kufanya kwa taifa kuweza kushindana na majirani zetu na hata nje ya mipaka ya Afrika.
Nimekuwa nikifanya utafiti kwa muda sasa katika kuandaa mipango ya mradi wa kuhamasisha IT Tanzania bara na Zanzibar, nilichogundua ni kwamba Kenya wametuacha kwa umbali mrefu sana, wakifuatiwa na Rwanda hata Uganda - kwenye hiyo league sisi tuna-face relegation.
Kenya wamepiga hatua kubwa na wanaendelea kupiga hatua zaidi ikiwa ni pamoja kuandaa mipango ya serikali na sekta binafsi na isiyo binafsi. Mfano wameandaa Malili Technopolis Concept Paper eneo maalum nje ya Nairobi kuwa business park ya IT projects - exclusively.
Sisi ardhi tunayo, mfano Kigamboni - ingetumika kwa kiasi fulani kuandaa mipango ya baadaye iwe IT business park.
Sera zetu za IT zipo kwenye makabrasha, lakini utekelezaji kama upo basi hauko wazi - na serikali is not leading us - then individuals tunaweza kujisukuma wenyewe.
Hatupo creative! Natoa changamoto kwa walio tayari (kama induviduals tutakaofanya umoja) tukusanye mawazo tufanye kitu cha kuanzia, mpaka mwisho wa mwaka tuwe na ukurasa wa kwanza.