kuhudhuria kwa rais wa zimbabwe robert mugabe wakati wa kuapishwa kwa rais kikwete kunaelezwa na wanazuoni huenda ikawa sababu ya nchi nyingi hasa za magharibi kusita kumpongeza rais kikwete aliyeapishwa leo.
Nchi hizo za magharibi zenye ushawishi mkubwa duniani zikiwemo marekani na uingereza, pamoja na kuwakilishwa na mabalozi wake hadi inasemekana hadi sasa hazijatuma salamu za pongezi za kuchaguliwa kwa kikwete kitu ambacho si kawaida yake.
Ikumbukwe kuwa wakati wa uchaguzi uliopita wa zimbabwe ambao ulilalamikiwa sana na uk na usa kuwa haukuwa huru na wa haki umepelekea hadi leo mugabe na familia yake kunyimwa hati ya kuingia katika nchi hizo isipokuwa kuhudhuria mikutano ya un pekee.
Wachambuzi wa mambo wanahisi tukio la leo kwa mugabe kuhudhuria linaweza kuwa limetia doa mahusiano ya tanzania na nchi hizo ikizingatiwa kuwa kuna madai yanayotolewa na chama cha upinzani tanzania kuwa kulikuwa na udanganyifu wa kura wakati wa kuhesabu.
Gazeti la MwananchiUchunguzi wa Mwananchi ulibaini kuwa kabla na baada ya kutangazwa kwa matokeo hayo, Dk. Slaa alikuwa kwenye ofisi za makao makuu ya Chadema ambako ilielezwa kuwa alikuwa na "vikao muhimu".
Kaimu katibu mkuu wa Chadema, John Mnyika ambaye pia ni mbunge mteule wa Jimbo la Ubungo, alisema Dk Slaa alikuwa akikutana na mabalozi wa nchi mbalimbali na kwamba aliendelea na vikao hivyo jana na pia alikutana na viongozi wa dini mbalimbali nchini.
Hata hivyo, Mnyika hakuwa tayari kueleza kilichokuwa kikijadiliwa katika vikao hivyo baina ya Dk. Slaa na mabalozi kwa upande mmoja, pia viongozi wa dini kwa upande mwingine.
nchi hii ipigwe BAN tule mapka vyura ndo tutatia akili...mijitu mijizi ya kura vibaya sanaaa
Interesting news. I didn't know Zimbabwe's dictator was good friends with Tanzania's dictator.
Kuhudhuria kwa rais wa Zimbabwe Robert Mugabe wakati wa kuapishwa kwa rais Kikwete kunaelezwa na wanazuoni huenda ikawa sababu ya nchi nyingi hasa za magharibi kusita kumpongeza rais Kikwete aliyeapishwa leo.
Nchi hizo za magharibi zenye ushawishi mkubwa duniani zikiwemo Marekani na Uingereza, pamoja na kuwakilishwa na mabalozi wake inasemekana hadi sasa hazijatuma salamu za pongezi za kuchaguliwa kwa Kikwete kitu ambacho si kawaida yake.
Ikumbukwe kuwa wakati wa uchaguzi uliopita wa Zimbabwe ambao ulilalamikiwa sana na UK na USA kuwa haukuwa huru na wa haki umepelekea hadi leo Mugabe na familia yake kunyimwa hati ya kuingia katika nchi hizo isipokuwa kuhudhuria mikutano ya UN pekee.
Wachambuzi wa mambo wanahisi tukio la leo kwa Mugabe kuhudhuria linaweza kuwa limetia doa mahusiano ya Tanzania na nchi hizo ikizingatiwa kuwa kuna madai yanayotolewa na chama cha upinzani Tanzania kuwa kulikuwa na udanganyifu wa kura wakati wa kuhesabu.
hivi mlitaka kikwete asimualike Mugabe kwa sababu ya kumuogopa mzungu? na asingeli mualika ningezidi kuamini kuwa Kikwete hafai kuongoza watanzania ndani ya bara la afrika kwa kuwa matendo yake yote ni kwa ajili ya kum please mzungu tu.
nchi hii ipigwe BAN tule mapka vyura ndo tutatia akili...mijitu mijizi ya kura vibaya sanaaa