Zwangedaba
Member
- Feb 1, 2009
- 99
- 25
suggestion zako opinion baada ya kugundua ndivyo tulivyo?Heheheheee....Miafrika Ndivyo Tulivyo....nani anabisha?
suggestion zako opinion baada ya kugundua ndivyo tulivyo?
Hakuna kuchoka ukichoka ndio utazidi kuwa ulivyo......kwahiyo kama masuggestions yanatolewa na hakuna mabadiliko una njia gani mbadala?huoni kila siku watu wanavyotoa ma-suggestions humu ndani? je, unaona mabadiliko yoyote? the answer is no. kila aina ya suggestions zimeshatolewa humu...ooh ifanyike hivi...aaah kifanyike vile....
icho chuo ni moja ya vyuo ninavyovichukia kuliko vyuo vyote duniani. nimesoma hapo, nimesota vibaya mno. nilikuwa na akili nyingi, nilijitahidi kiasi kikubwa lakini muda mwingi nilikuwa naishia frustrations. nashukuru Mungu nilimaliza salama. nilitaka kusoma mastaz hapo, lakini moyoni sina hamu, naona kama naenda jehanam. kwanza kabisa, ni kuhusu wanavyojifanya kubana maksi wakati mtu unapiga msuli na una akili za kumwaga. ndio maana first class kama ya wanasheria kule huwa hamna, ni kuanzia second. sasa kama hamna, ina maana maprof hawana uwezo wa kumfundisha mtu akapata hiyo first class. nili piga msuli niipate first lakini walinibania.
...duh, unatumia kipimo gani kujua ulikuwa unasoma na kustahili alama nzuri? Kusota sio kipimo cha kupata alama nzuri, unaweza kusota lakini usisome yenye manufaa kwa somo husika.icho chuo ni moja ya vyuo ninavyovichukia kuliko vyuo vyote duniani. nimesoma hapo, nimesota vibaya mno. nilikuwa na akili nyingi, nilijitahidi kiasi kikubwa lakini muda mwingi nilikuwa naishia frustrations. nashukuru Mungu nilimaliza salama. nilitaka kusoma mastaz hapo, lakini moyoni sina hamu, naona kama naenda jehanam. kwanza kabisa, ni kuhusu wanavyojifanya kubana maksi wakati mtu unapiga msuli na una akili za kumwaga. ndio maana first class kama ya wanasheria kule huwa hamna, ni kuanzia second. sasa kama hamna, ina maana maprof hawana uwezo wa kumfundisha mtu akapata hiyo first class. nili piga msuli niipate first lakini walinibania.
Halafu nini cha kushangaza hapa? Hali nzima ya nchi na hakika karibu bara zima la Afrika kusini mwa jangwa la sahara ni mbofu na yakusikitisha.
Kama mnadhani hapo UD kuna msoto hebu tembeleeni vijijini muone jinsi mazingira ya elimu ya msingi na sekondari yalivyo....heheheheheee...mnacheza nyie. UD ina afadhali maradufu.
Ndugu wanajamii hali ya chuko kikuu cha Dsm sehemu ya mlimani inatisha sana. Hii ni katka nyanja za elimu usafi mazingira na maadili.
Unapoongelea suala la ELIMU hali mbaya kwani siku zijazo tutaanza kuwa na wataalamu feki mitaani. Hii inatokana na ukweli kuwa miundombinu iliyopo haikizi mahitaji ya muda/haiendani na wakati, na ile iliyopo ni michache ukilinganisha na watumiaji. Ufundishaji umekuwa wa shida, upatikanaji wa vifaa vya kujisomea kama vitabu library na kompyuta imekuwa shida sana.Hali inapelekea wanafunzi kutumia madaftari ya na madesa ya waliomaliza zamani (kama miaka ya 90) na kutokana na uchache wa vitu hivi imekuwa ni kawaida wanafunzu wanapokuwa kwenye mitihani wanaingia navyo kwa minajili ya kuangaliziana siku hizi wanaitaa wayalesi (wireless). Sasa hapo tutegemee wasomi/wataalamu gani??!
HATA SEHEMU YA CHUO AFRICA IMESHUKA KWA SASA NI CHA 18 KUTOKA 13 NA NI CHA 3,496 DUNIANI KUTOKA 2500 NA.
USAFI ni mbaya sana hasa sehemu za kutoa haja. Vyoo vinanuka usafi wa maeneo hayo haupewi kipaumbele lakini kuna makampuni yaliyoajiliwa kwa ajili ya usafi huo uangalizi ndo hakuna. Kama wewe ni mgeni maeneo yale utatamani ukimbie utapokuwa unakatiza katika korido za majengo ya chuo sababu ya harufu.
MAJENGO nayo hayako kwenye hali nzuri kuna baadhi ya maeneo hasa kwenye korido mvua inapokuwa ikinyesha utafikiri chini ya mti, kuta zimechakaa, paa zinashuka, kuna vyumba huwa lazima viwe na AIR CONDITIONER lakini kwa sasa zina miaka kadhaa hazifanyi kazi n.k.
MIUNDOMBINU kama baranara za ndani zimeboka hakuna lolota linafanywa, taa za kumulika barabara usiku haziwaki na hii ni hatari kwani inasababisha kuwapo vibaka, waporaji na wabakaji wa dada na mama zetu.
Hiyo ni baadhi tu ya uozo kwa ufupi.
Uchunguzi unaonyesha kuwa haya yote yanasabishwa kwa kiasi kikubwa na ukweli kwamba uongoji wa chuo upo kwa ajili tu ya kuhakikisha wanafunzi hawagomi basi hawana lolote lamaana huko ofisini kwao hakua anayejali na miaka kadhaa ijayo udsm itakuwa ni magofu tu na mitaani kutakua na wasomi/wataalamu feki kibao.