I think no one should be above the law. Kama jamaa wamefanya makosa ni haki yao kabisa kwenda kujibu mashitaka. Kwanini watu wanaogopa kuwakamata eti amani itatoweka....amani gani hiyo wakati wao ndo wamesababisha mauaji ya kikatili???
WAKUU mimi nimemsoma sana Mamdani. Ila kifupi huyu msomi ni apologetic tuu hana jipya. Anakaa nyuma ya Keyboard yake huko Columbia University anaona kwamba..swala ni takwimu. Hell no! Aende Darfur aone watu wanavyoishi kama ngedere porini! Hivi kwa nini maisha ya mwafrika tunayaona hayana thamani? Eti Bush kaua Iraq? is our concern in Iraq or the lives of our fellow Africans? Yaani mimi hapa ndo wasomi wetu siwaelewi...wanatusaliti...kwa hiyo..hata kama Bashir kaua..asichukuliwe hatua mpaka Bush ashtakiwe? Kama kiongozi kama Bashir kaua..aende ajibu mashataka. Simple. Hizi apologies za akina MAMDANI NI ZILE ZA KIZAMANI za kuona kwamba mkubwa lazima aheshimike. Hatujazoea kuwawajibisha wakubwa katika bara letu.
Kuna wanaosema eti...tuanzishe mahakama za kiafrika..but we ALL know the truth..hakuna kiongozi wa kiafrika aliye mkweli. wananchi hawana viongozi wa kuwaamini..perhaps kama hawatusikilizi sisi..basi watawasikiliza wazungu!
Well najua wengi hawajui jinsi hii mahakama ya ICC inavyofanya kazi..lakini kifupi..ni nchi zetu zilizosaini huu mkataba wa Roma mpaka leo ziko nchi 30 a kiafrika zilizo saini uu mkataba.... Sasa kama waafrika walijua athari zake mbona hawakukataa kusaini huu mkataba? Hivi sisi waafrika tuna akili kweli? US mpaka leo huu mkataba wameukataa kata kata..ndo maana hii mahakama hawaitambui. Leo mtu anaongea eti US ishtakiwe...hii inaonyesha viongozi wetu wanavyotumwa kusaini hii mikataba hawaelewi maana yake...wanaenda kufanya shopping...
Tuache kuwa apologetic...Bashir belongs in Prison..tuache hizi conspiracy theories..US has nothing to do with suffering in Darfur..its we Africans. Tuache kuwa na excuse for everything. We kill each other tunaanza kuwasingizia wengine..
Wanamjadala naomba msome kitabu kipya cha Mamdani, niko sehemu ya pili na nakubaliana kabisa na jamaa. Uchambuzi wake wa kina wa takwimu hewa kuhusu Darfur unaonesha kuna unafiki mkubwa kuhusu hali ya huko Sudan. Kitabu hicho kinaitwa 'Saviours and Survivors: Darfur, Politics, and the War on Terror'.
Kwa ufupi Mamdani anashauri kuwe na kitu anachokiita 'Survivors Justice' na sio 'Victor's Justice'. Hii ya pili ni hatari maana inafanya ambao sio 'victors' wawe 'victims'. Na wakishakuwa hivyo hawachelewi kugeuka na kuwa 'killers' kama ilivyokuwa Rwanda. Na hata wasipobadilika ni rahisi kwa 'victors' kuwaonea. Hiyo ya kwanza ni kama ile ya Sauzi ambapo kunakuwa na 'Truth and Reconciliation'. Hiyo inayapa makundi yote - yaliyoonea na kuonewa - fursa ya kujenga upya 'just society'
Africa kuwa na mahakama yetu wenyewe sio leo, itachukua muda sana. Viongozi wa Africa wameangalia Zimbabwe ikiteketea mpaka ikatembelea magoti sijui uamuzi wa kesi yoyote ile kwenye hiyo mahakama itachukua muda gani plus finacing the court?
Nahisi inaweza kuwachukua viongozi wa Africa karne nzima kukubaliana tu ni wapi hiyo mahakama ijengwe, au iwe makao makuu including its set up!.
Nakubaliana sana na swala kwamba kuna unafiki mkubwa "double standards" sana jinsi nchi zilizoendelea zinavyoshughulikia mambo ya Africa.
Leo hii silaha zote zinazotumika kwenye hizi conflict areas zote Africa zinatokea huko huko kwao, wanaozisafirisha ni wao na ndege na meli ambazo ni registered huko huko, kampuni ni za huko, leseni wanatoa wao. Kama kweli wanayo nia ya kutatua haya matatizo ya kuuana huku Africa wanajua kabisa la kufanya. Na dealers wa silaha wangekuwa ndiyo wa kukamata kwanza pamoja na watengenezaji na wasambazaji kama wanavyokabiliana na madawa ya kulevya! na kufikishwa kwenye ICC. Ukiangalia sana utaona wao wanajali kile kinachowaumiza wao moja kwa moja tu basi.
Ndiyo maana hatu wafanyi kitu mafisadi in the name of "truth and reconciliation". Mkuu bwana hakuna peace and reconciliation mpaka justice ipatikane. Wewe umemuua baba angu, mama angu, mke wangu au watoto wangu and you think tuki wekwa meza moja I will simply forgive and forget? Justice isipo patikana ndiyo animosity ina kua na kurithishwa from generation to generation. Na asi kudanganye mtu hizi "truth and reconciliation" siyo kati ya victims kwa victimizers, ni kati ya viongozi ambao hata hawaja athirika na maafa wanayo sababishwa. Wananchi wa kawaida mna lazimishwa kusahau na kusamehe. How do you do that?
Je unasema kwamba hakuna kosa kwa mauaji ya watu wa Sudan? ICCTR wanapelekewa mashitaka na kufungua faili. Hata wewe ukiwa na ushahidi wa kutosha unaruhusiwa kufungua mashitaka dhidi ya USA. kama american walifanya kosa wairaki watafungua mashitaka dhidi yao, wakinyamaza wameridhika kwasababu walimuhukumu Sadan kwa sheria zao. Uenda waliokufa kwenye vita wanahesabu kama damu zilizo waletea ukombozi ikilinganishwa na waliouwawa au wangeendelea kuuwawa na Sadam. Je haki isitendeke kwa watu wa Darful kwasababu ya vita vya Irak au kwa sababu ICCTR iko Ulaya. Africa wenyewe kwa wenyewe ndo kunatabaka and rule of arms nani amfunge paka Kengelewe. Kama Wadarfu wameona kuna kosa na ushaidi upo mashitaka yamefunguliwa tuaje sheria ifanye kazi siyo kulindana.Nakubaliana nawe hapo, ijapo mimi naona ingekuwa vizuri zaidi Afrika tuwe na mahakama yetu sisi wenyewe.
Sababu yangu kusema hivyo ni kuwa naona unafiki wa mataifa tajiri umezidi. Hivi wako tayari kuwahukumu watu kutoka afrika lakini husikii viongozi wa nchi zao wakishtakiwa.
Kwanini wasimletee Bush mashtaka kwa mauwaji ya raia wa Iraq kwa kuwa umeshathibitishwa kuwa Iraq haikuwa na hayo WMD na wala haina, yeye kaivamia nchi ya watu kwa njia ya udanganyifu.
Kwanini sisikii viongozi CIA, MOSSAD, MI5 na wengineo wakishtakiwa kwa mateso walio wafanyia washukiwa.
Itakuwaje mtu kufungwa zaidi ya miaka 7 bila mashtaka eti kwa kuwa nimshukiwa. Sheria za nchi hasa Britain ambayo ina the longest detension period ya siku 28 (wanataka kuongeza iwe siku 48), hata haikaribii!
Hao wamarekani ambao wanayafanya haya sheria zao haziruhusu mtu kudetainiwa zaidi ya siku mbili bila kushtakiwa. Sasa ni haki kweli?
Jamani tujiweke mbali na unafiki wa aina hii. Afrika naona wakati umefika tuanze kujitegemea sisi wenyewe, kutoka kwenye vyumba vya habari hadi mahakama za kijumuiya.
Wanamjadala naomba msome kitabu kipya cha Mamdani, niko sehemu ya pili na nakubaliana kabisa na jamaa. Uchambuzi wake wa kina wa takwimu hewa kuhusu Darfur unaonesha kuna unafiki mkubwa kuhusu hali ya huko Sudan. Kitabu hicho kinaitwa 'Saviours and Survivors: Darfur, Politics, and the War on Terror'.
Kwa ufupi Mamdani anashauri kuwe na kitu anachokiita 'Survivors Justice' na sio 'Victor's Justice'. Hii ya pili ni hatari maana inafanya ambao sio 'victors' wawe 'victims'. Na wakishakuwa hivyo hawachelewi kugeuka na kuwa 'killers' kama ilivyokuwa Rwanda. Na hata wasipobadilika ni rahisi kwa 'victors' kuwaonea. Hiyo ya kwanza ni kama ile ya Sauzi ambapo kunakuwa na 'Truth and Reconciliation'. Hiyo inayapa makundi yote - yaliyoonea na kuonewa - fursa ya kujenga upya 'just society'
Je unasema kwamba hakuna kosa kwa mauaji ya watu wa Sudan? ICCTR wanapelekewa mashitaka na kufungua faili. Hata wewe ukiwa na ushahidi wa kutosha unaruhusiwa kufungua mashitaka dhidi ya USA. kama american walifanya kosa wairaki watafungua mashitaka dhidi yao, wakinyamaza wameridhika kwasababu walimuhukumu Sadan kwa sheria zao. Uenda waliokufa kwenye vita wanahesabu kama damu zilizo waletea ukombozi ikilinganishwa na waliouwawa au wangeendelea kuuwawa na Sadam. Je haki isitendeke kwa watu wa Darful kwasababu ya vita vya Irak au kwa sababu ICCTR iko Ulaya. Africa wenyewe kwa wenyewe ndo kunatabaka and rule of arms nani amfunge paka Kengelewe. Kama Wadarfu wameona kuna kosa na ushaidi upo mashitaka yamefunguliwa tuaje sheria ifanye kazi siyo kulindana.
Namtih58 said:Ungesoma nilichoandika vizuri ungeona hakuna popote nimeandika mwenye kosa asishitakiwe, ila tuwe na mahakama zetu wenyewe.
..ninachotofautiana na wewe ni kwamba mabaradhuli hawa washitakiwe ktk mahakama za kimataifa kwasababu hizi zetu sina imani nazo.
..zaidi napendekeza wahifadhiwe ktk mahabusu zetu na watumikie vifungo vyao ktk magereza yetu Afrika. nina imani mahabusu na magereza yetu yatawanyoosha kuliko magereza ya ulaya na marekani.