Leseni za udereva class A & D -

Shytown

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2025
Posts
1,275
Reaction score
2,389
Nafikiri kwenye leseni za vyombo vya moto takriban 85% ni za hayo madaraja mawili na ndio yanaweka msongamano mkubwa kwenye ofisi za Vehicle Inspectors wakitaka kurenew (naongelea ku-renew na sio kuomba leseni mpya).

Napendekeza;
1. Wenye leseni za hayo madaraja ya chini kabisa yakiisha muda wake; mtu awe anatumiwa control number na mfumo kwenye simu yake ili aende kulipia na baada ya wiki mbili aende kuchukua leseni yake huko TRA.
Nimefikiri hivyo kwa sababu suala linalo ulizwa ni unacheti cha macho? sasa kwa nini wasifikiri kuweka mfumo mtu aka apload hicho cheti hata kwa kutumia simu?. tungeokoa sana muda hapa.

2. Kunaweza kuwekwa utaratibu kuwa mfumo unatuma Control number mara moja/ inayofuata aende nk nk na pengine mfumo uache kutuma pale muhusika anafikisha umri wa miaka 70.
Naamini watu wenye hayo madaraja madogo (binafsi) wapo makini, wanapima macho kwani nafikiri hata kwa ratio ya wingi wao na matukio ya ajali yataonesha hilo.

3. Mapato yatokanayo na leseni yanaweza kuongezeka pengine mara 2 kwani kwa sasa wapo madereva wengi tu wanaendesha bila leseni hai wakifikiri urasimu wa kuanza kufuatilia leseni (ku renew)..

4. Nafikiri kwa kufanya hivyo tutawarahishia Vehicle inspectors kazi na pia kuwapa muda zaidi wa kushuhulikia kwa haraka changamoto za leseni kubwa ambazo ndizo zimeonesha kuwa na matatizo zaidi.

5. MWISHO: Kama huu utaratibu utashindikana; pengine wafikirie kuweka ONE STOP CENTRE ya leseni ya vyombo vya moto kwa kila mkoa (mtu akiingia hapo akute mtu wa TRA na wa vehicle wamalize kila kitu) tofauti na sasa mtu anaenda TRA, anatoka anaenda Polisi central, anatoka anarudi TRA anatoka nk nk na kila mahala anakutana na foleni....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…