Mzalendohalisi,
Ndani ya CCM wamo watu wazuri ambao wanaelewa kuwa nchi hii sasa inatawaliwa badala ya kuongozwa. Hawa ni wazee wetu, marafiki zetu na wengine huchelea kupiga makofi anaposimama mbunge wa Upinzani. Sii kwa sababu ya umaarufu wa mtu huyo ila wanajua kuna moto unawashwa!..
Wao kama wabunge wa CCM ambao wanajua fika kwamba kama sio nguvu ya mtandao wasingeipata ajira hiyo... na wakuu hawa wa chama ndio waajiri wao sio wananchi.
nafikiri tunapozungumzia sana Wapinzani ni kwa sababu wao hawawezi kumeza funda la mate na kumwachia Mungu.. huyatoa mawazo yao wazi, wakati hao wa chama tawala hufutika kurasa zao na kushika tama kusubiri wakati wa makofi!