duh!! kasheshe hiyo sasa mamsap wa huyo rafiki yake sijui aingie mitini... utaanzaje we!! ni kuzua balaaa noma sana.. si angekwenda kwa sperm bank naye.... ah hivi alimpa ruksa kabisa huyo beste yake kula mavituz?????? mmmmmmmmmmmmmmmmmm
waendeleze tu suala la siri zao na safari
hii itabidi rafiki aruhusu mkewe amegwe
na jamaa na arudishe nusu ya pesa aliyochukua.
Loh! nimecheka mie, haki ya ww hii inaonyesha jinsi baadhi ya wanawake wasivyokuwa waaminifu kwenye ndoa zao. Anyway mie naona huyu mama aliamua kuzaa na mwanaume mwingine mara baada ya kuona miaka inaenda hashiki mimba. Akaona bora ajaribu nje labda atapata. Hii ipo sana ktk jamii.
Sijakusoma.....Wanaume muwe waangallifu ila msishtuke ni wachache tunafanya hivyo maana unakuwa na mumeo huku wengine wana kidumu kidogo sasa ni ngumu kujua mimba ya nani, ila hatufanyi makusudi ni kutojua na kufwatilia kwa sababu ya ndoa na wengine wanajua kuwa mimba siyo ya mume basi unauchuna tu kuogopa aibu na kuachika.
Mbu!
Kwanza hiyo habari niliisoma nikashtuka,ughaibuni kuna mambo lakini ha ha..
Jamaa aliyesaidia kumpa mimba rafiki yake kwanza lazima amechanganyikiwa maana mkewe noma yaani kumbe watoto wote wawili siyo wa mumewe. Kwahilo lazima huyo mwanamke lazima alaumiwe.
Ila kama asingeombwa kumsaidia kumpa ujauzito mke wa rafiki yake asingejua yote hayo kuhusu hao watoto,ingekuwa afadhali ila ndo hivyo kalea watoto kumbe siyo wake tena ndani ya ndoa akiamini ni wa kwake.
Pia inawezekana huyo daktari alikosea au hiyo test haidanganyi??nimtetee mbeijing mwenzangu, huh!
Wanaume muwe waangallifu ila msishtuke ni wachache tunafanya hivyo maana unakuwa na mumeo huku wengine wana kidumu kidogo sasa ni ngumu kujua mimba ya nani, ila hatufanyi makusudi ni kutojua na kufwatilia kwa sababu ya ndoa na wengine wanajua kuwa mimba siyo ya mume basi unauchuna tu kuogopa aibu na kuachika. Yaani mtoto akizaliwa ndani ya ndoa na mke wako ni mtoto wako..vinginevyo DNA ingekuwa tunafanya kiholela TZ,ndoa nyingi zingeporomoka!...
Siri ya mtoto kuhusu baba yake ajuaye mama!
...π ha ha ha Belinda umezungusha zungusha maneno, umejiuma uma halafu mwisho umechapa bakora "...yaani mtoto akizaliwa ndani ya ndoa na mke wako ni mtoto wako"... duuuuh! yaani unalazimisha ikubalike tu japo ukweli unaujua, ha ha haaa...
Hiyo imekaa vibaya saana maana mimi katika umri wangu nwa miaka 51 sjawahi kusikia watu hupeana magari au kuazimana lakini mke na wkulaumiwa ni huyo bwana aliyetoa mke wake sadaka maana ndiye aliye sababisha mpaka akamuumbua na yule mama wa mwanzo mmmh
...π Pretty, pretty, pretty.....! kwahiyo akishapata mimba huko nje ni busara kuuchuna kimyaaaaaaa!?
...kula n'kule π ! ...yaani jamaa mshtuko wa kutambua watoto si wake, bado unataka rafikiye ajivinjari na huyo mama watoto wake pia? ha ha haaa... yataka moyo!
Nawasikiza kina mama baada ya wikiendi watavyolivalia njuga hili, si unaona shishi alivyoruka kimanga! ...in no particular order,... nyamayao, Belinda Jacob, mwanajamii1, penny, Joyceline, pretty, WoS, na wewe hapo shishi π na wengineo, njooni hapa mtupe mtizamo wenu kuhusu huyu 'mbeijing' mwenzenu 'alivyolikoroga!'
Sio busara,sasa afanyeje? na wakati mumewe hana uwezo wa kutoa manii za kuwezesha kupata mtoto. La msingi huyo bwana akubali kulea watoto kwa kuwa wamezaliwa ndani ya ndoa yao. Kama ni ndoa ya kikristo sheria inaruhusu kuwa ni watoto kwa maana wamezaliwa ndani ya ndoa yao.
.. Jamani unajua haya mambo yanachangiwa na vitu vingi na si ukosefu wa uaminifu tu.
hivi mie sielewi watu wanawekagaje mambo yao humo ndani, mume angemshauri mama akaokote mbegu kwingine kokote sio kwa mtu wa karibu hivyo, je baadae huyo nae akija kutoboa siri inakuwaje?anatembea huko nje anashika mimba yake asonge na familia yake kama ndio ilikuwa plan yao,hapo kwingine jamani ni shughuli looo, mie nasema tu siku zote baba wa mtoto amjuae ni mama.
...baba mwenye nyumba akawa amefanikiwa kuepusha ile aibu ambayo angeipata kama jamaa angeondoka na yule mtoto.Hapa nadhani tunaona matatizo ya wanandoa wanaoshindwa kupata watoto na kukataa kukubali hali zao na kutafuta mbadala ulio bora.