Kula huku kula gani, mnakula hadi mbegu,
Kula huku kula gani, mwayala hata magugu,
Kula huku kula gani, huku mwatuita ndugu,
Kula huku kula gani, vya watoto navyo mwala?
Kula mmeshakwishakula, sasa muda wa kulipa,
Vya wanetu mmekula, kulipa na mtalipa,
Mlidhani tumelala, wajanja mkatukopa,
Vya kwenu hatutavila, na kura hatutawapa!
Na. M. M. Mwanakijiji (Sauti ya Kijiji)
Mzee wa Kijijini Kwetu Shikamoo!
Huwa nikisoma tenzi zako zinanikumbusha enzi zile tukiita middle school au primary school kabla haijawa shule ya msingi, kabla ya lile azimio letu la Musoma. Azimio lile halikuwa baya lilitufanya wengi tukajua kusoma na kuandika lakini halikutufanya tuelimike. Azimio lile ni sawa na Maamuzi ya shule za kata za Mkapa za Bila azimio, wengi watamaliza Vidato lakini MM nakwambia watoto hawajui kitu kinaitwa Bunsen Burner. Nasikia wanafanya
Alternative to Practicals, sijui ndio zikoje? Nachotaka Kusema HONGERA sana kwa kuelimika Mzee.
Kwenye hawa jamaa waliokula, naogopa kukwambia kuwa msimu wa kupanda umefika, sasa hii habari yako imetushtua sana kuwa wamekula mpaka mbegu, tutapanda nini? bahati mbaya hata yale majani yalikuwa yanafaa kwa mboga za majani yameliwa na tembo na wanyama wa poli, inasemekana baada ya nyani kuvuna mahindi yote shambani sasa wale wanyama wa pori waliokuwa waji kijijini wamekuja kwa wingi tu, si kwa mazao yalioko juu ya aridhi hata yale yalioko chini ya aridhi yameliwa na
Fuko. Mjomba alisema ataangalia upya uzio unaotenganisha kijiji na hifadhi za wanyama pori ili wakija basi nasi japo tupate nyama kidogo za wanyama lakini tunaona mpaka leo kimya.
Mzee Mwakijiji, akina shangazi na binamu nao wamesema ni ndugu zake na baba na wanahaki na mali na aridhi za ukoo wetu. Kwa hiyo inakuwa shida sana kuitisha kikao cha familia kujadili japo kubadilisha taratibu za kugawana hayo mazao. wamesema hata wakila kuna shida gani? nao si wanandug? lakini kibaya zaidi wapo wengine wanaotoa mazao wanaenda kuhifadhi kwenye
vihenge vya vijiji vya mbali, nadhani utakapo rudi utaona hata mabua wamehamisha.
Nashukuru kwa moyo wako wa kuwaambia kuwa walipe, na kuwa muda umefika, na kuwa kama hatawalipa watakipata cha mtema kuni. Mimi na wadogo zangu tunaogopa sana kuwawajibisha hawa akina shangazi na binamu na hata mjomba. Mwaka 1995 walituambia kama tutampa mtu mwingine kuwa msimamizi wa mirathi kutawaka moto kam kwa jirani yule mwembamba mrefu, si unaona hata yule dada walimpelaka mahakami kwenye sijui wanaita "Dar Haiji". Tukafikiria tena mwaka 2005, waksema si unaona huyu mnayetaka kumpa usimamizi wa mirathi atawavalisha wote Kombati, mtapiga gwaride weeee usiku na mchana. Walipoona tunaonekana hatuwasikilizi, wakasema huyu ni mchawi sana, si mnaona anaruka juu na Ungo, anawanga mchana kweupe.
Sasa mimi nimechanganyikiwa, sasa hivi wanasema kama mnataka kumpa mtu mwingine basi asiwe yule dogo wa kushinda kwenye matreni hajakomaa kisiasa, mara alishanunuliwa, tukasema basi tumpe yule mwinjilist maana ni msema ukweli mtu wa Mungu, nao wana hoja wanasema kama alishindwa kutunza mkataba na kanisa ndio ataweza kutunza mikataba na nyie yatima,
Mzee wetu hali ni ngumu, sijui kama tutaruhusiwa kuwa na wasiofungamana na itikadi ya familia yoyote, maana wanaonekana hawaipendi hii hoja pia. upande wao inaonekana ile hoja ya kusema watoto wa mjomba watamtaka Mjomba kwa hiari aachie usimamizi wa mirathi imepingwa vibaya mno na wazee na vijana wanaomzunguka mjomba. Hadi Mtera nao walisema hawaoni sababu.
Kuna akina binamu watoto wa mjomba wanonekana kuja juu sana kwa maneno sijui kama watakuwa tofauti na baba yao, labda wanafanana rangi lakini matendo ni tofauti, labda watasema mali za yatima ziwafikie walengwa sijui, unawajua akaina Jafari, akina mashaka, akina Bernad, akina Lawrence sasa hivi ni wakubwa sana. Ila yule mtoto wa mzee wa strategy za ushindi wakati ule alishindana nao kwenye ujenzi wa nyumba ya vijana, yupo kimya sana.
Mzee ninayo mengi ya kukwambia lakini muda hautoshi, Nitakuandikia siku nyingine, wasalimie huko kwako, nasikia vi-nzi vyako vinafanya kazi ya
"Nge" Kama hujawasikia hao nge walikuwa wanaangalia mali za kijiji cha kule chini ambako baba yao alifungwa kisiwani kwa miaka 27. Mkuu waangalie walipowaua hawa Nge, lakini naamini kama hata sungusungu wetu wangefanya kazi hata kwa miezi sita tu kama hao nge, kijiji chetu kingekuwa cha mfano. Inawezekana nzi wakawa ni njia mbadala ya sungusungu, tuwape chakula, nitatuma noti ya sh.20 unitumia lile karatasi walilochafua hao nzi kule wapi sijui asia.
Nisalimie wazee wenzio watakapokuja kunywa kahawa Jamvini.
Mwanao
Kijijini Kwetu
🙁