Ladslaus Modest
JF-Expert Member
- Jun 27, 2008
- 635
- 27
Mie nilikuwa ninapendekeza tuanzie hapa: - Badala ya kumuita baba mkubwa na/au baba mdogo UNCLE tuwe tunawaita ELDER FATHER na YOUNG FATHER. Badala ya kumuita mama mkubwa na/au mama mdogo AUNT tuwe tunawaita ELDER MOTHER na YOUNG MOTHER ... ... ... nakadhalika.
Hii inafaa kuwepo kule kwenye jukwaa la lugha/elimu
Kwanza asante Kibunango kwa kubonyeza "Report this" icon. Kijakazi has been banned for misbehaving.Hii inafaa kuwepo kule kwenye jukwaa la lugha/elimu
Kiingereza cha kiTanzania
Wapendwa wana JF na wale wote wenye mapenzi mema na nchi yetu Tanzania; hapa ulimwenguni katika nchi zote zilizotawaliwa na mwingereza takriban kila moja ina kiingereza chake mfano kuna kiingereza cha Australia, Belize, Canada, Caribbean, Hong-Kong-S.A.R., India, Indonesia, Ireland, Jamaica, Malaysia, New-Zealand, Philippines, Nigeria, Singapore, South-Africa, Trinidad-&-Tobago, UK ,US, na Zimbabwe.
Ukifuatilia kwa makini kila nchi iliyotajwa hapo imeongeza au imepunguza au imebadili neno au herufi fulani kutoka kwenye kiingereza cha asili cha Uingereza.
Mfano Mwingereza anatumia neno POST CODE lakini mMarekani anatumia neno hilo hilo kama ZIP CODE
Kinachosikitisha ni kwamba sie waTanzania tunatumia either American English or British English.
Kuna maneno mengi ambayo wataalam wa lugha mnayafahamu (mie sio mtaalamu wa lugha bali ni Mchungaji) ambayo mnaweza kuyabainisha hapa ili tuweze kuwa na kiingereza chetu cha kiTanzania.
Mie nilikuwa ninapendekeza tuanzie hapa: - Badala ya kumuita baba mkubwa na/au baba mdogo UNCLE tuwe tunawaita ELDER FATHER na YOUNGER FATHER. Badala ya kumuita mama mkubwa na/au mama mdogo AUNT tuwe tunawaita ELDER MOTHER na YOUNGER MOTHER ... ... ... nakadhalika.
Naomba kuwasilisha.
Huku pwani ambako ni chimbuko la Kiswahili, dada hasa ni ndugu mkubwa wa kike, na kaka ni ndugu mkubwa wa kiume. K/sbb ya kuiga lugha na utamaduni wa Kiingereza, hata mdogo wangu (wa kike) ni dadangu, na mdogo wangu wa kiume naye ni kakangu!
Sidhani kama ni utamaduni wa kiingereza. Kwa waswahili, Dada ni 'ndugu wa kike' na Kaka ni 'ndugu wa kiume' bila kujali umri wao. Tizama kamusi zote za kiswahili, hasa zile zilizoandikwa zamani utaliona hili. Kwa asili neno 'ndugu' ni mtu ambaye mmechangia baba na/au mama. Kwa hivi ukimtambulisha mtu kwamba ni nduguyo, moja kwa moja mtu anajua huyo ni dada yako au kaka yako.
Sidhani kama ni utamaduni wa kiingereza. Kwa waswahili, Dada ni 'ndugu wa kike' na Kaka ni 'ndugu wa kiume' bila kujali umri wao. Tizama kamusi zote za kiswahili, hasa zile zilizoandikwa zamani utaliona hili. Kwa asili neno 'ndugu' ni mtu ambaye mmechangia baba na/au mama. Kwa hivi ukimtambulisha mtu kwamba ni nduguyo, moja kwa moja mtu anajua huyo ni dada yako au kaka yako.