IshaLubuva
JF-Expert Member
- Dec 4, 2008
- 250
- 12
Kwenye kipindi cha Bongo Star Search kinachorushwa hewani na Runinga ya ITV, jana wale vijana wawili (Msechu na mwenzake anayewakilisha DSM) ambao mmoja wao ndiyo anatarajiwa kvikwa taji la BSS wa 2009 walijikuta wakiwa kwenye Ukanda wa Hatari (Danger Zone). Kwa mujibu wa Majaji wa Kipindi hicho hiyo ilitokana na watazamaji na washabiki wao kutowatumia ujumbe wa simu wa kutosha. Lakini mimi nilipata mashaka kwa kiasi fulani kwa kuzingatia ufanisi ambao umekuwa ukionyeshwa na vijana hawa hasa Msechu ambaye hata wao Majaji wamakiri kila mara kuwa huwa anawashangaza kila wakati anapotakiwa kupanda jukwaani kwani amekuwa na kawaida ya kuweka ubunifu wa hali ya juu katika nyimbo na hivyo kuweka mvuto wa kumtazama na kumsikiliza. Siamini kama hawa vijana hawakupata kura za kutosha bali wameingizwa kwenye ukanda wa hatari kwa malendo ya kibiashara zaidi na ndo maana naona kama wamewafanyia watazamaji kiini macho kama kile kinachofanywa kenye kamari ya kakarata kekundu/ka pesa. Mnasemaje wadau
Unapiga kura unaliwa visent vyako mwisho wasiku wana mchangua mshindi wanao mtaka wao na sio kutokana na kura za wananchi.....Mi ndo maana iwa siharibu pesa yangu kutuma viujumbe hivyo mnawanenepesha wajanja endeleeni kuliwa hakuna cha kura wala nn wizi mtupu.
Unapiga kura unaliwa visent vyako mwisho wasiku wana mchangua mshindi wanao mtaka wao na sio kutokana na kura za wananchi.....
Hapo ndipo nilipo choka kabisa kwani Rogers alikuwa mkali kuliko Misoji.Mnakumbuka ya Misoji na Rogers?
teh teh, unajua hivi vitu ni kama siasa. mwaka 1995 Mr Mrema alikuwa na mashabiki wengi sana,walikuwa tayari hata kusukuma gari lake umbali wowote aliotaka. lakini siku ya kupiga kura wengi hawakupiga kwa sababu kadhaa ikiwemo kutojiandikisha na kauvivu tu. katika hili ni kibiashara zaidi ila nikikuuliza wewe mleta mada umepiga kura mara ngapi kuwatetea hawa watu? vijana wamejipanga wanapiga kura kwa malengo ya kumshindisha ndugu/jamaa yao kama unafikiri unawakubali piga kura nyingi mpaka uishiwe Mama Rita ajipatie Return ya investment yake..