Raia Fulani
JF-Expert Member
- Mar 12, 2009
- 11,866
- 4,267
Kwa lipi la maana aliloongea hususani jana? sijaona maneno ya hekima hata moja,labda mipasho na taarabu.Hata kama ana point ya kuongea,presentation ni very poor nasikitika kusema hilo.Rais wetu ni muongeaji mzuri ila si mtekelezaji. Kasema kuwa yeye ndie mwajiri mkuu. Hajajua kuwa sisi wananchi ndio tumemwajiri? Kama haamini hilo basi asitekeleze matakwa ya watanzania
Kitu ambacho kimenisikitisha ni kauli zake, na vitisho. Hii inaonesha kiasi gani mfanyakazi wa nchii hii anavyodharaulika. Rais anaongea kwa uhakika namna ile wakati karibia na uchaguzi? na wale wajinga wajinga waliokwepo pale shida zimewajaa mpaka midomoni eti wanashangilia tuu, aaaagh waDanganyika lini tutazinduka jamani? Hivi kwa nini wafanyakazi wa nchi hii hatuna nguvu katika serikali yetu? tunachezewa tuu kama watoto wadogo! hivi kauli kama hizi zingetolewa kule Bondeni kwa MADIBA nadhani COSATU wange zaa na mtu. Kule wenzetu chama chao ni very very powerful, tatizo sisi tulifanya cha cha wafanyakazi ni jumuia ya CHAMA, wakajazwa ma shushushu tu huko, na hakukuwa na lolote miaka yote iliyopita. Sasa hivi ndo tunazinduka na kukuta mfumo mbaya mno. Kingine nimestajaabu ni idadi ya wafanyakazi serikalini. Miaka yote nasikia Serikali ndo mwajiri mkuu yaani serikali ndo imeajiri watu wengi kuliko sekta binafsi. Lkn idadi niliyosikia jana kumbe watu laki tatu na nusu tu ndo wapo serikalini, nchi yenye watu millioni arobaini, ukitoa watoto na wanafunzi labda wabakie millioni ishirini, waliobakia hapo labda laki moja wapo sekta binafsi, wengine wakulima na jobless. Ndo maana nchi hii ukukaa Dar utadhani imepiga hatua sana lkn nenda mrogoro tu hapo utashangaa maisha jinsi yalivyo ya kijima. Ule Umati na mshikamano na kutomwalika pale shamba la bibi (Uwanja wa Uhuru) ndiko kulikomfanya jasho limtoke, kaona mambo yanaweza kwenda mrama, ndiyo tunaweza badilisha serikali, kwa nini hatuwezi? huu mshikamano wa wafanyakazi ni muhimu sana kwa maslahi ya taifa hili. Tusikubali kuburuzwa tuuu wakati wao wanamaliza keki ya nchi hii halafu sie tunaonekana tunawabugudhi katika ulaji wao.
Hivi wageni rasmi huwa wanalipwa posho?Ni kweli,hasira na mipasho ya jana ni hasira ya kutoalikwa kuwa mgeni rasmi.
Kiukweli kikwete anahitaji changamoto ili aamke alikolala. Jana kachonga sana juu ya tucta. Mengine ya ukweli, mengine vitisho, mengine kujitetea, na mengine ushauri, n.k. Lakini ukweli unabaki palepale kuwa tunahitaji kina mgaya wengi wa kumchangamsha rais anayeona kuwa kila kitu ni shwari kumbe sio. Takwimu zake alizotoa si za kimantiki kiivyo. Kuna hela nyingi sana zinavuja nchi hii ambazo zingeweza kuboresha mambo. Rais asingoje kuwaka na kutoa vitisho yanapotokea ya tucta. Ni kweli katishika kwani hajawahi kuona hayo yakitokea. Rais wetu ni muongeaji mzuri ila si mtekelezaji. Kasema kuwa yeye ndie mwajiri mkuu. Hajajua kuwa sisi wananchi ndio tumemwajiri? Kama haamini hilo basi asitekeleze matakwa ya watanzania
Eti kama mnataka kuninyima kura ninyimeni tu! Maskini wafanyakazi – mmeshiriki mara nyingi kuwaweka madarakani (tena wakati mwingine kwa mbinu chafu) sasa wameshika mpini wanawaringia, mmekuwa kama "takataka', hamna thamani tena kwao na hawawahitaji! Poleni sana –sikutegemea maneno haya yatoke kinywani mwa Rais
Wandugu mmesema ukweli. Rais anaamini kuwa watanzania laki 3 walio katika serikali hata wakimnyima kura bado atakuwa rais! Ni kweli hakupaswa kuongea na wale wazee, tena wa ccm. Angekuwa hodari angeitisha mkutano na waandishi wa habari na kucheza na hoja kama kina Blair. Wale wazee wana shida zao hivyo watacheza na mdundo wowote watakaopigiwa. Ni watu ambao hawana taarifa za kutosha kuhusu nchi hii na yale yanayoendelea. Sema tu alikuwa anatupasha kwa mlango wa nyuma akijua fika kuwa ujumbe ungetufikia huku akishangiliwa. Ili rais athibitishe kuwa yeye yuko sawa, aitishe mkutano na waandishi
Mimi simo. Jana muungwana ndiyo katoa best speach ever. Hivi ukitaka kuongea na TUCTA unaita wazee au TUCTA wenyewe? Hauwezi kuwaita watu ambao hawafanyi kazi kuwaelezea madai ya wafanyakazi. Ni kuwadhalilisha wazee hao japo wao hawajitambui. Mbona hawaiti kuwaeleza Kagoda and kinds ni nini na kwa nini kama anataka kuwashirikisha informations.
Hivi wageni rasmi huwa wanalipwa posho?
Hivi wageni rasmi huwa wanalipwa posho?