Nakupa offa uje tuone hii picha kwangu off course na Belinda akiwepo maana huwezi jua....labda utaondokana na wazo eti wakina mama wanalea vizuri kuliko kina baba....
Masa
una manyanyaso makubwa wawili wanapoachana;
1. Mume anashikilia mali
2. Mke anashikilia watoto
Kihivi na sababu hii: Nimeona watu wengi wakienda cancelling mambo ya mahusiano na kama wakitaka kuachana kwa talaka wafanyaje tena kama wana kids na kuwashirikisha. I mean ni ngumu ila inaweza kuwa rahisi na mkabaki friends baada ya kutua mzigo kwenye maisha yenu.
Kufikishana kwenye vyombo vya sheria inatokana na wengine kutalikiana kwa kushirikisha sheria huku mojawapo ya kitu muhimu ni malezi ya watoto(incase wanao)..Ina mana wenyewe binafsi wanandoa wameshindwa kukubali kuwa lea watoto ninatoa support nk kwahiyo wanabishana na kila mmoja akivuta watoto upande wake..
Back to you: Wewe unaonaje?Watoto wakae na nani, mama au baba?Maana kuhusu kuoa/olewa tena kati ya hao wanandoa watakaoachana inaweza itokee au isitokee japokuwa lazima relationships watakuwa nazo na watu wengine watakaokutana nao maishani mwao tena.
...BJ nadhani unamaanisha Counselling, au? ...kwa maana hiyo, kutokana na mila na desturi zetu wabantu inatuwia ngumu kupata suluhisho za namna hiyo kutokana na mapungufu ya kisheria au?
Tukirudi kwenye maaadili na tamaduni za kikwetu. Panapotokea mifarakano, mara nyingi pataitishwa kikao cha familia kujaribu kuwasaidia makubaliano mtavyoachana. Mara nyingi hii humpelekea mzazi aliye na uwezo kupewa jukumu la kulea watoto wakubwa, na yule/wale wadogo kuendelea kulelewa na mama, au sio jamani?
Tatizo langu linakuja, hata kama mama anaamini mumewe ana uwezo wa kulea watoto wote, bado yeye atang'ang'ania kuwachukua wanawe, na kama hiyo haitoshi...ugomvi kila mara kutaka mafungu na mafungu yaliyopitiliza ya hela za matumizi toka kwa mtalaka wake.
Hamuoni hapo mama anatumia mtoto/watoto kama fimbo ya kumchapia mumewe?
Mume nawe, kwa kumwambia mkeo aondoke na kila alichokuja nacho, huoni unamnyima mkeo haki ya kudai kila mlichochuma naye?
Mbu unavituko sana nilikuwa sijaona signature yako looohh haya mpwa!
Mzee kama ni mali nitamwachia kila kitu, ila watoto wangu aniachie...maana njemba nyingine ianze kubandua mama yao watoto watajisikia vibaya.....I will rather fight again to achieve mali zingine....
...kwahiyo mpwa upo radhi njemba nyingine zitanue ndani ya 'Prado' yako na ile 'mansion' uliosota kuijenga miaka nenda rudi pale 'Rock City?'...upo tayari kusota 'uswazi' na wanao kwenye chumba cha kupanga na kila kukicha kukimbizana na dala dala? mambo ya pride magumu bana, yataka moyo aisee... π
...Tatizo kubwa ni jinsi ya kuachana na maisha ya hao watu baada ya talaka tena kama wana watoto. Kuambiwa ondoka na ulicho nacho bila kujali muda na mali mlizochuma wote inauma ndo mana urafiki hauwezi kuisha na kuona talaka ni kama sehemu ya maisha.
Mazee kwa kweli niko tayari, nitanunua hata Kibajaj 4WD na kupanga nyumba kule Kapili point baada ya muda nitakuwa kwenye mstari najua kwa kuwa nitakuwa mzima nitamtimulia vumbi na X5 mpya.....nikiwa na amani na raha zangu...
Ndo maana sikuachii nakwambia, kwako nitabanana tu mpaka kieleweke maana najua mwisho wa siku lazima niachie kasri na mikoko. Nimekosa nini sasa mpaka nikimbilie kwengine muda huu..ha ha ha
Ndo maana sikuachii nakwambia, kwako nitabanana tu mpaka kieleweke maana najua mwisho wa siku lazima niachie kasri na mikoko. Nimekosa nini sasa mpaka nikimbilie kwengine muda huu..ha ha ha
Masa naona muda si mrefu Mbu atakuwa kwetu tunasema 'mtwanzi' wako kwa mdogo ake Bellies tafadhali muheshimu lasivyo atakupa maralia mwaka mzima.
Nimekusoma mazee, anakaribishwa ila asilete ushabiki wa mpira home!
....ha ha haaa π sawa, nikifika mlangoni navua jezi, tukiangalia mpira kwenye Tv hakuna kushangilia goli wala ku smile! kaaaaaazi kweli kweli.
that's what am talking about!
Ukishaliweka akilini suala la kuoana kwa heri, na kuachana kwa heri nadhani haitokuwa ngumu kuzingatia haki za kila mhusika kwenye ndoa yenu.
Ile shari ya kukomoana ndio inayoletesha mama kuingia mitini na watoto, mume naye kung'ang'ania mali! Haipendezi mmeachana halafu mazungumzo baina yenu yanafanyika via watoto, solicitors, au ustawi wa jamii π
wewe BJ wewee, π shauri yako,...kuna wengine wataku challenge hiyo sentensi niliyoitia wekundu. Kasri na mikoko vitu vya mpito hivyo, penzi likichuja je?
Anyway,...kwanini mume na mke wakishaachana, utawaona (wengi wao) bado wanaendelea kukomoana?
... next time tuongelee upande mzuri wa ndoa na raha zake pia jinsi ya kuboresha mahusiano ya wanandoa.
... Kukomoana ni kama vile kumwonyesha mwenzio kuwa bila wewe naweza au wewe umesusa wenzio wala ila yana mwisho na inabidi upande mmoja udharau kukomolewa hatimaye mkomoaji atajiona mbona hafuatiliwi na kuacha mwenyewe.