Bado hakujakucha subiri, hata maoni ya watu wengi kupitia itv walionyesha wasiwasi wa moja kwa moja kuhusu redet
Re: Dr. Slaa aongoza kwa 73% - CACT
taarifa ya REDET inaweza kuwa sahihi kabisa inategemea umemwoji nani? cha msingi hapa ni sampling.
ktk hawa watu 2600 ni lazima kuna wenye na wasio na vyama.
We still have a big challenge on professional ethics, njaa zinasumbua saana na hiyo ni kutokana na mtu kuwa trained ili awe tajiri kwa njia yeyote ile. Watu wengi wanasoma ili waibe na siyo kusoma ili wasaidie nchi kimaendeleo.
Ndiyo maana taasisi kama REDET zinatumiwa na wanasiasa kufanyia kazi zao. Sehemu zenye kuelimisha umma zimeshakuwa za waanasiasa badala ya hawa wanasiasa kupata mawazo kutoka kwenye hizi taasisi sasa zimekuwa zikipata maelekezo kutoka kwa wasiasa mfano halisi ni kwa hawa REDET pamoja na kupoteza muda mwingi wakichimba/wakisoma darasaani ili kuleta tija katika taifa changa kama hili lakini badala yake wanasahau kuwa elimu yao ni nuru kwa taifa.
Taasisi kama REDET ni kuanza nazo kuzivunja ili ziundwe zenye uhuru, kuaminika katika jamii na ufanisi wa hali ya juu. Tunahitaji kuamini tafiti toka kwa wataalamu ndiyo, lakini wa kwanza kutufanya tuamini ni hao wanaofanya hizo tafiti siyo kama sasa ambapo wanadhani watanzania bado wajinga kama 2005 au b4.
Nilikua nasikiliza taarifa asubuhi hii kutoka Radio Free Africa, nimeshtushwa na taarifa ya mtu aliyejitambulisha kua ni mkurugenzi wa taasisi inayojishughulisha na utafiti (CA kama wa REDET) akiipinga report ya REDET kwa kusema taasisi yao nayo inaendelea na utafiti huo kwa njia mbalimbali, sms, emails, kuhoji moja kwa moja, etc nchi nzima.
Kwa mujibu wa taarifa hiyo hadi sasa Dr. Slaa anaongoza kwa 73%, JK 12% na Lipumba 9%. Kwa mujibu wa mkurugenzi huyo anapinga kitendo cha REDET kuchagua baadhi ya mikoa na kuacha mikoa mingine especially kanda ya Ziwa ambako ndio kuna wapiga kura wengi na anapinga report yenye only 2600 samples.
Siifahamu kampuni hii (CACT), wanaJF mwenye taarifa zaidi atuhabarishe
MIMI ITAKUWA YA PILI, mpaka sasa anakura mbili hata kama hatajipigia.Kura ya Kwanza ya DR Slaa ni ya Kwangu so hawa sijui REDET sijui Synovate wataseeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeeema weeee, lkn mwaka huu Rais wetu ni Dr. SLAA period!!!!!!!
wewe hukuona jamaa wa REDET kuyatangaza alisema najua mtasema sana lakini habari ndio hiyo. huoni kama ile Tafiti imekaa kiumbea umbea!!
Taarifa ya REDET inaweza kuwa sahihi kabisa inategemea umemwoji nani? cha msingi hapa ni sampling.
ktk hawa watu 2600 ni lazima kuna wenye na wasio na vyama.
Kwahiyo ktk ripoti yao ilibidi waonyeshe ktk waliowaoji ni wangapi wana ccm, wangapi wapinzani na la msingi wangapi kati ya hao 2600 hawana vyama. Hawa ni muhimu kwa maana ndio hasa wanaochagua Rais kwa maana watanzania wengi hawana vyama.
Kwa Tanzania kama sample yako haina asilimia 30, aslimia 20 wapinzani na asimilia 50 ambao hawana
vyama. Basi utafiti au survey yako nzima haina maana kwa maana it does not reflect reality.
Kura ya tatu JF kwa slaa Dr. ni yangu. Nawashukuru wanaCCM a.k.a REDET kumpa %12 kwa Slaa manake hata hao REDET/ccm 12% wamempigia Slaa hawamkubali mwanachama wao. Then 12%ccm+100%chadema+ kura za wasio na vyama=Mr.PRESIDENT SLAA. Hivi siku ya kuapishwa dr. Slaa ni lini nianze kuandaa nauli kuelekea dar. Mpaka sasa nimeweka sh.7,800/= nina imani ntapata 100,000/= maana kwa mara ya kwanza Rais msomi mzalendo anatinga ikulu.