Habarindiyohiyo
JF-Expert Member
- Aug 11, 2008
- 263
- 16
Dk. Slaa: Sitagombea urais
na Deogratius Temba
KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa, amesema hana mpango wa kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010.
Dk. Slaa ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Karatu kwa mihula miwili mfululizo, alisema, jukumu alilonalo katika maisha yake ni kuwatumikia watu wa Karatu ambao wamemwamini na kumpa nafasi hiyo na si kugombea urais.
Akizungumza katika kituo cha Televisheni cha TBC1, katika kipindi cha Jambo Tanzania, Dk. Slaa alisema yeye ni mtumishi wa watu wa Karatu na hawezi kuwaacha kwenda kugombea urais.
"Wananchi wangu waondoe wasiwasi, na wala wasijenge hisia kuwa nitasimama kuwania urais, wala sina wazo hilo, wala sijawahi kuota kuwa rais wa nchi hii, na sitakubali kuwasaliti wananchi wangu kwa kuacha kuwatumikia kama mbunge," alisema.
Akizungumzia kuhusu CHADEMA kusimamisha mgombe urais katika uchaguzi mkuu ujao, Dk. Slaa alisema lazima wamsimamishe mtu kwani chama hicho kinaaminiwa na kupendwa na wananchi.
"Ni lazima CHADEMA tutamsimamisha mtu katika nafasi ya urais na kuendelea kupigania haki ya Watanzania mpaka mwisho," aliongeza Dk. Slaa.
Akizungumzia suala la kuungana kwa vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu ujao, Dk. Slaa alisema CHADEMA kitaungana na chama chochote chenye nia ya dhati ya kutaka kulikomboa taifa, na kilichojijengea sera yakinifu na imara zinazokubalika na wananchi.
"Kuungana tutaungana, ila tutaungana na watu ambao ni ‘serious' (makini), wenye mipango, tutaelekezana tukiwa mezani kama ni nini tunataka kufanya, na kila mmoja aseme ana nini, lakini haya yatafanyika wakati muafaka ukifika," alisema.
Aliongeza kuwa, lengo la vyama vya upinzani, hasa CHADEMA, si kuitoa CCM madarakani tu, ni kuungana, maana kuna kitu cha msingi kinatakiwa kufanyika kwa umoja ili maisha ya Watanzania yabadilike na kufanyiwa mabadiliko ya kweli katika maisha ya watu.
Kuwa rais atakuwa amewasaliti vipi wananchi wake? Na je, huyo mtu wanayemsimamisha hana 'wananchi wake', au wa kule kwetu wakisalitiwa powa tu?!
Na nilidhani watu wa jimboni kwake ni watanzania vilevile kwa hiyo angeweza kuwasaidia vizuri!
Mwenye ujuzi zaidi anifahamishe tafadhali.
dk. Slaa: Sitagombea urais
na deogratius temba
katibu mkuu wa chama cha demokrasia na maendeleo (chadema), dk. Wilibrod slaa, amesema hana mpango wa kugombea urais katika uchaguzi mkuu ujao wa mwaka 2010.
Dk. Slaa ambaye pia ni mbunge wa jimbo la karatu kwa [b]mihula miwili mfululizo[/b], alisema, jukumu alilonalo katika maisha yake ni kuwatumikia watu wa karatu ambao wamemwamini na kumpa nafasi hiyo na si kugombea urais.
Akizungumza katika kituo cha televisheni cha tbc1, katika kipindi cha jambo tanzania, dk. Slaa alisema yeye ni mtumishi wa watu wa karatu na hawezi kuwaacha kwenda kugombea urais.
wananchi wangu waondoe wasiwasi, na wala wasijenge hisia kuwa nitasimama kuwania urais, wala sina wazo hilo, wala sijawahi kuota kuwa rais wa nchi hii, na sitakubali kuwasaliti wananchi wangu kwa kuacha kuwatumikia kama mbunge, alisema.
Akizungumzia kuhusu chadema kusimamisha mgombe urais katika uchaguzi mkuu ujao, dk. Slaa alisema lazima wamsimamishe mtu kwani chama hicho kinaaminiwa na kupendwa na wananchi.
ni lazima chadema tutamsimamisha mtu katika nafasi ya urais na kuendelea kupigania haki ya watanzania mpaka mwisho, aliongeza dk. Slaa.
Akizungumzia suala la kuungana kwa vyama vya upinzani katika uchaguzi mkuu ujao, dk. Slaa alisema chadema kitaungana na chama chochote chenye nia ya dhati ya kutaka kulikomboa taifa, na kilichojijengea sera yakinifu na imara zinazokubalika na wananchi.
kuungana tutaungana, ila tutaungana na watu ambao ni serious (makini), wenye mipango, tutaelekezana tukiwa mezani kama ni nini tunataka kufanya, na kila mmoja aseme ana nini, lakini haya yatafanyika wakati muafaka ukifika, alisema.
Aliongeza kuwa, lengo la vyama vya upinzani, hasa chadema, si kuitoa ccm madarakani tu, ni kuungana, maana kuna kitu cha msingi kinatakiwa kufanyika kwa umoja ili maisha ya watanzania yabadilike na kufanyiwa mabadiliko ya kweli katika maisha ya watu.
Very smart position. For my opinion Dr. Slaa is good on what he does now, let him not leave his MP position. I respect his stand for knowing what he can do best and stick to it.
Mimi nafikiri Dr. slaa amesahau kuwa hata akiwa rais bado atawatumikia watu wake wa karatu kwa sababu nao wapo ndani ya TZ!!.
The one and only ambaye vyama vyote vya upinzani vikimuunga mkono ni John Cheyo anaweza kumpa wakati mgumu JK japo hawezi kumshinda...
Slaa hawezi kuikosa posho na marupurupu yanayopatikana kwenye ubunge ,jamani si aseme kweli tu ,kuwa penye ubunge ndio penye kula isyokuwa na shida ,kusema kuwa ana watu wake wa karatu hapo anakipa mtihani Chama chake na kuzidi kuonekana ni cha kikabila au kimajimbo ,ni bora angelisema kama atapendekezwa atafikiria au kwa kifupi aseme bado hajawa tayari au yumo katika matayarisho ambayo anaona hayajatimia katika kuifuatilia ngazi ya Uraisi ,kujikomba kwa watu wa Karatu ni kujitenga na WaTanzania wengine ,kama mbunge awe tayari vilevile kuongoza WaTanzania kama akipendekezwa kuwa Raisi awache woga wa kukosa posho.
Akili zako kama Maalim na Jussa mwenye kusema kwamba Dr Slaa na CHADEMA ni mafisadi!. Kwani Urais na Ubunge upi una posho kubwa?
CHADEMA inakuaje ya kikabila kwa Slaa kuwapenda wananchi wake wa Karatu?
Kwani akiwa Mbunge anatumikia watu wa Karatu pekee yake? Kama ingekuwa ni Karatu si angetoa orodha ya mafisadi wa Karatu!
Hivi ulisikiliza mahojiano yake yote na TBC au unarukia tu kutokana na hiyo mistari michache iliyoandikwa kwenye habari
Asha
Agombei au hagombei?Dr W. silaa, kasema agombei tena urais na lengo ni kutunza kiti chake cha ubunge ili kuleta ushindani Bungeni.
source: http://freemedia.co.tz/daima/habari.php?id=15352