ALIYEKUWA kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni katika Bunge lililopita, Hamad Rashid Mohamed amewashambulia viongozi wa Chama Cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kwa kuwataka wawe na msimamo na wafanye uamuzi kisiasa kama watu wazima.
Hamad amewatuhumu Chadema kuwa wabaguzi kwa kuwa walitaka kushirikiana na Chama Cha Wananchi (CUF) kuunda kambi hiyo lakini walidhamiria kuvitenga vyama vingine ya upinzani.
Mbunge huyo wa Wawi (CUF) alimewaeleza waandishi wa habari mjini Dodoma kuwa, wao (CUF) hawana shida ya vyeo kwa kuwa waliwahi kuwa na madaraka makubwa kuliko ya kwenye hiyo kambi ya upinzani bungeni.
Amewataka viongozi wa Chadema wawe ‘matured' na watambue pia gharama za kisiasa za kutomtambua Rais Jakaya Kikwete.
Kwa mujibu wa Hamad, CUF wana msimamo, waliwahi kufanya uamuzi mgumu na wakautekeleza hivyo Chadema wajifunze kwao (CUF).
Alisema, Mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe, alimfuata akamueleza nia ya kushirikiana na CUF kuunda kambi ya upinzani bungeni lakini kwa kuvitenga vyama vingine vyenye wabunge katika Bunge hilo.
Hamad amesema, alikataa wazo la Mbowe na akampa ushauri ambao hadi sasa hajautekeleza.
Mwanasiasa huyo amesema, CUF wanataka kambi ya upinzani bungeni ushirikishe vyama vyote vya upinzani, Chadema hawataki.
Hamad amesema, viongozi wa Chadema wamemkwaza Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia na Mwenyekiti wa CUF, Profesa Ibrahim Lipumba, hivyo waende wakazungumze nao wayamalize.
Source: Basil Msongo,HabariLeo ,Dodoma; Tarehe: 18th November 2010
tusiwe blinds kwenye hili... Lazima tuelewe ukweli kabla ya kudhani CUF hawana pointJamani kumbe CHADEMA wana maadui wengi ,CUF wanakeraa sana ,toka waunde serikali(waolewe) na CCM wana nyodo sana.Sijui mimba inawasumbua?? Khaa!!!!!!!!:angry:
- Well, hii ni nothing but cheap politics halafu you wonder who is immature here Mwenyekiti wa Chadema aliyeongea naye huyu kiongozi wa CUF in private, au huyu kiongozi wa CUF aliyeyaleta mambo ya Private kwenye Public? Sasa unaunda vipi umoja wa Upinzani bungeni na viongozi kama hawa wasioelewa kutenganisha maana ya ishus za private na ishus za public!
- I mean mambo kama haya yataishia kurudisha nyuma tu momentum ya ari ya wananchi waliyoionyesha kwenye huu uchaguzi kwamba wanataka mabadiliko, sasa kama CUF hawaelewi basi dawa ni kuachana nao tunachotaka ni upinzani wa kweli bungeni ili taifa liweze kunufaika na uwajibikaji utakaoletwa na Upinzani kweli bungeni hata kama ni mdogo, maana sasa itakwua nguvu ya hoja zaidi kuliko uwingi wa wabunge wa chama,
- CUF someni mabadiliko ya nyakati wananchi hawana tena muda wa kupoteza na hizi habari zisizo na anything good kwa taifa, zaidi tu ya kutafuta cheap popularity ambayo kama imeshindikana kupatikana kwenye kura, haiwezi kupatikana kwa kulumbana kwenye public na wapinzani wengine!, it stinks!
William.
Hapa the main point ni kwamba Kafri hawezi kuwa mbele lazima awe mkiani, kama alivyofanyiwa muasisi wa CUF, kwa hiyo hapa ni kwamba CUF hawawezi kuungana na kafiri wataungana na wale ambao hawajakata tamaa na akhera CCM, maana viongozi wa juu ni Waislaam na mwislaam humuunga mkono mwislaam,,,,,Chunguza uone ukweli ndiyo huoJamani kumbe CHADEMA wana maadui wengi ,CUF wanakeraa sana ,toka waunde serikali(waolewe) na CCM wana nyodo sana.Sijui mimba inawasumbua?? Khaa!!!!!!!!:angry:
Cuf = ccm.
The big issue here ni Udini tu, naamini kama chadema viongozi wangekuwa akina Abdallah, Mohammed wangekubali na si swala la muafaka hapa mkuu.Kama ni kweli haya ni maneno ya bwana Hamad basi ni kakurupuka na kakosa busara. Naanza kudoubt kama kweli ana stahili sifa zote alizo kuwa akimwagiwa kama kiongozi wa upinzani. Lakini kwa vile CUF sasa hivi wana muafaka (makubaliano) na CCM na kwa vile wamepewa baadhi ya vyeo kule visiwani tutegemee objectivity toka kwa baadhi ya viongozi wa CUF kupungua especially wale viongozi wakuu.
Kwanza Mh. Hamad ana bidi atambue kitu kimoja. Inabidi atambue kwamba kikatiba Chadema ina ruhusiwa kuunda uongozi wa upinzani bungeni bila kushirikisha chama chochote kingine. Kwa hiyo chama chochote kitakacho alikwa na Chadema kujiunga nacho ni kwa mapenzi ya Chadema wenyewe. Sasa Hamad ana chukulia kama ni haki.
Pili ukiangalia idadi ya wabunge vyama vingine vilivyo pata huoni hata maana ya kuwaingiza kwenye uongozi rasmi wa upinzani Bungeni. Chama kina mbunge mmoja au wawili kita badilisha nini haswa ukizingatia CCM ina more than 50%? Hao wabunge wa vyama vingine (ukiachilia CUF) wange kuwa wana hitajika kuvusha idadi ya upinzani kuvuka asilimia 50 ningeelewa ila kwa sasa kuli hitahika ushirikiano wa vyama vikuu viwili vya upinzani.
Tatu ni kwamba siyo lazima uwe kwenye shadow cabinet kuwa mpinzani na kuleta upinzani wa kweli bungeni. Hao wabunge wawili watatu waliobaki bado wana weza kuleta changamoto nje ya baraza la kivuli humo bungeni. Kama kweli wana taka sauti zao kusikika basi wata sikika tu!
Swala la kujiuliza ni je kwa nini Hamad ana nga'ngania Chadema washirikishe vyama vingine Bungeni lakini haja wahi kutamka (as far as I know) na kudai kwa nini CCM haishirikishi vyama vingine kwenye serikali yao (ukiachilia mbali SMZ)? Mimi nadhani Hamad ana tambua kwamba kuwa na muafaka na CCM ZNZ na kuwa kwenye kambi ya upinzani Bungeni SMT itakua contradictory kwa maana kwa upande mmoja wata kuwa part of the government na kwa upande mwingine wata kuwa part of the opposition.Nadhani Hamad na CUF wana tafuta tu visingizio vya kuto kuji husisha na upinzani wakiogopa kuvuruga muafaka.
The big issue here ni Udini tu, naamini kama chadema viongozi wangekuwa akina Abdallah, Mohammed wangekubali na si swala la muafaka hapa mkuu.
Muasisi wa CUF ni nani? na kwa nini alitolewa? wakapangwa Wale wasiokata tamaa na akhera. It implies the same mkuu wa CCM na Mkuu wa CUF ni waislaam hawawezi kuangushana. Lakini kwa Chadema wakuu ni kina nani?... We dont need to go to school to know thisHuwa sikimbiliagi kusema kitu fulani ni udini mkuu. Kuna mambo ukiya angalia juu juu utadhani ni udini ila it's deeper than that. Tukubali ukweli kwamba CUF kuwa sehemu ya serikali ya CCM Zanzibar kutaipa wakati mgumu CUF kushirikiana na vyama vya upinzani kwenye Bunge la Muungano. Wata wakosoaje?
Pia sababu nyingine ninayo weza kutoa ni labda wivu mkuu. CUF ndiyo walikua chama kikuu cha upinzani kwa muda mrefu na huyu bwana Hamad ndiyo aliye kuwa kiongozi wa upinzani kwenye Bunge la tisa. Kwa hiyo ina wezekana kuna friction fulani kati ya hivi vyama kwa kimoja kujiona ndicho chama kipya kuu (na CHadema ina haki ya kufikiria hivyo) na CUF kujalibu kujionyesha kwamba wao bado wana nguvu. Hapa ni tatizo la transition of oppositional power kutoka CUF kwennda Chadema. CUF hawataki kuachia na Chadema ina demand the respect it deserves.
Muasisi wa CUF ni nani? na kwa nini alitolewa? wakapangwa Wale wasiokata tamaa na akhera. It implies the same mkuu wa CCM na Mkuu wa CUF ni waislaam hawawezi kuangushana. Lakini kwa Chadema wakuu ni kina nani?... We dont need to go to school to know this