Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Omari Mzee aliahidi kuwa serikali italifanyia kazi suala hilo mapema iwezekanavyo.
Tanzania kuna makampuni mengi ya coca-cola, mimi nayajua matatu (coca-cola kwanza, Dar; Bonite bottlers, Moshi na African bottlers, Mbeya) sasa ni wapi hao au wote? inamaanisha hata mzalendo Mzee Mengi kampuni yake hailipi kodi? Naomba ufafanuzi tafadhali.
...inabidi tuungane tususe kunywa soda zao kuonyesha msisitizo ... kila mmoja wetu amwambie mwenzie ili tuwapige marufuku watoto, waume , wake ndugu jamaa na marafiki kunywa coca cola huenda ikasaidia kidogo
Hii Habari Imekaa Kama Udaku Vilee, Haielezi Ni Coca-cola Ipi, Na Huyo Mtu Anaenda Kwenye Kamati Ya Bunge Akiwa Hajui Analoongea Yaani Anataja Coca Tuu Makampuni Mengine Hayakumbuki! Mengi Anavyowabana Mafisadi Sasa Wameanza Kumharibia (sina Uhakika Katika Hilo Ila Inaonyesha Hivyo Kwa Sababu Habari Inataja Kampuni Moja Tuu
Ahsante.
Ndo maana nikasema Waziri asituambie eti atashughulikia hili suala. Vipi makampuni mengine? Yapo ambayo hayajui?
Kuhusu stori za kidaku daku, tatizo ni Media. Tanzania hatujui ni nini kinaendelea katika nchi yetu kwa sababu hatuna vyombo vya kutupasha habari juu ya nchi inavyoendeshwa, na ni vipi inavyotakiwa kuendeshwa. Na kwa sababu wananchi hatujui kinacho endelea, inakuwa vigumu sana kuchangia kuleta mabadiliko. Kazi ipo!
ufisadi tz ni kila sehemu.
hebu fikiria eti coca-cola hawalipi kodi! wakati huo huo wamachinga wanakabwa kufa mtu
Posted Date::6/4/2008
TRA yaorodhesha makampuni yasiyolipa kodi
Na Tausi Mbowe
MAMLAKA ya Mapato Tanzania (TRA), imewasilisha serikalini orodha ya makampuni makubwa sugu, ambayo yanakwepa kulipa kodi.
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya TRA, Dk Moselina Chijolinga aliwaambia wajumbe wa Kamati ya Bunge ya Fedha na Uchumi jana kuwa, mamlaka yake imeamua kupeleka orodha hiyo kwa serikali ili kuomba kampuni hizo zichukuliwe hatua.
''Tumeshapeleka serikalini orodha ya makampuni ambayo hayalipi kodi kabisa na yale yanayolipa kwa kulegalega kwa kuwa yanajulikana,'' alisema Dk Chijolinga.
Hoja hiyo iliamsha ari ya wajumbe wa kamati hiyo ambao ni wabunge, chini ya uenyekiti wake Dk Abdallah Kigoda, ambao waliuliza ni makampuni gani hayo ambayo yanakwepa kulipa kodi.
''Sijui kama sheria inanilinda katika hili, lakini tumeshapeleka barua serikalini inayoonyesha orodha ya makampuni yote sugu kulipa kodi,'' alisema Dk Chijoliga.
Wabunge hao walimtoa shaka Mwenyekiti huyo wa TRA na kumtaka kutaja majina hayo kwa kuwa katika Kamati za Bunge sheria inasema kuwa ana haki ya kutaja chochote.
Baada ya kuambiwa hivyo Mwenyekiti huyo aliidai kuwa kampuni ya Coca-Cola imekuwa hailipi kabisa kodi na baadhi ya makampuni ya simu za mkononi yanalipa kodi kwa kusuasua.
Hata hivyo, Dk Chijoliga alishindwa kutaja idadi kamili ya makampuni hayo mbele ya wabunge hao ambao wengi walionekana wazi kutaka kuzifahamu kampuni hizo.
Naibu Waziri wa Fedha na Uchumi, Omari Mzee aliahidi kuwa serikali italifanyia kazi suala hilo mapema iwezekanavyo.
Hii issue iko tatanishi kidogo..
Hivi ni kweli kwa kampuni ya kimataifa kama Coca-cola kutolipa kodi?
Kama ni kweli, basi duh tumeuwawa kifo cha mende...
Mkuu watu huwa siku hizi wanachukua kitu inaitwa FRANCHISE kwa maana unaweza ukaingia mkataba na Kampuni Mama na ukapewa nembo pamoja na Logo ukaendelea kufanya kazi kwa jinsi ninavyojua mimi sasa hawa wanaona they gat nothing to loose aibu inabaki kwa THE COCA COLA COMPANY USA.
Sasa hawa TRA watuambie ...wao kama Chombo tunachokitegemea kwenye kukusanya mapato walikuwa wapi muda wote huo kuyasema haya na ikiwezekana watuambie ni vigogo wangapi wanalinda maslahi ya Makampuni haya.