wakuu, kazi na dawa, maana mafisadi wanakula vichwa waweza jisahau majukumu ya nyumbani pia. katika pita pita zangu nimekumbana na jamaa na maswali yake mengi,
kisa?
hana imani na mama watoto wake, anadhani kuna mtu 'anamsaidia'.
anasema;
mke kaacha kusuka minyoosho, mabutu na kuchana afro, sasa anashinda saloon kutengeneza nyusi na hair extensions sijui weaving almuradi kila wikiendi hayupo nyumbani!
Mobile fone yake (mke) hataki tena mumewe aiguse!, tena kwa nyodo 'shemeji' kila akiingia nyumbani tu anaizima simu yake! mbaya zaidi kwa jamaa yangu, simu imewekwa Pin lock, just incase!
eti (mke) kabadili nguo za kazini, sasa anavaa suti za mini sketi badala ya 'za' suruali, na kazidisha manukato ya bei mbayaaaa...
sijathubutu kumuuliza mambo ya chumbani, maana 'inaelekea' kila dalili jamaa anahesabu boriti usiku!
Anyway, pamoja na kumliwaza kote kwamba mama watoto anatingisha tu kiberiti, jamaa hataki kuelewa, naona mwenzangu ana sink into mid life crisis, naona soon atapata depression!
Je kama ingelikuwa ni wewe, alama gani zaidi zingekuashiria kugeuka kwa upepo?
...yeshakukumba weye??? ...
Du! labda tuseme ni kipindi cha mpito, na jamaa ana imani ipo siku bi mkubwa atatulia. Swali linabaki usalama wa kiafya upo? Pamoja na hayo nampa pole...
Bado ana mng'ang'ania wa nini?Hajiamini kuwa anaweza kulea watoto mwenywe..ampe talaka aende zake..kama ni watoto anaweza kuwalea uko waliko hata kama i kwa mama yao...
Kuliko kuishi na huo msalaba,mwanadamu haishi mara mbili...ya nini kujitesa na mawazo na suddenly changes za maisha kwa mkewe?
Achana nae sio wako tena.
Maswali muhimu:-
Je huyo jamaa na huyo mkewe wameishi muda gani katika ndoa yao? Je akijifanyia evaluation anaona ni kitu gani kinakosekana kwake!? Yawezekana kabisa huyu jamaa akawa ndio chanzo cha mambo haya yote... ni bora ipatikane picha kamili ya kitu kinachoendelea kati ya hawa watu wawili!!
Naomba pia itambulike kwamba kuna mambo mengi yanayochangia uaminifu kupotea ktk ndoa ikiwa ni pamoja na:
- Kuboreka
- Kukosa imani na mwenza wako
- Kutokujiamini (Self insecurity) ambayo mara nyingi hupelekea mwenza kutaka kuonyesha uwezo wake kwa kulipiza kisasi
- Kwa wanawake kukosa mambo mapya katika maisha ya kila siku... sio vizuri kuwa na monotonous routines katika maisha > mtoe out, mpe surprises hata kama ni ndogondogo zinaleta mwamko ktk ndoa
Kwa hiyo suala hapa sio kulalamika ila fanya self evaluation an uone unafit vipi na unafanya nini katika mahusiano yenu!!
Ifanye ndoa yako iwe ya furaha kwa kutimiza wajibu wako kama mwanaume ktk ndoa!!
Marriage, such misery...
Ningekuwa mimi, ningeshamkodia majambazi wammalize muda mrefu, ili nioe mtu mwingine ambae hata nisumbua moyo wangu. kwanini aninyanyase na icho kidudu chake? salaaa leeee. kudadeki za kijotijoti.
Ningekuwa mimi, ningeshamkodia majambazi wammalize muda mrefu, ili nioe mtu mwingine ambae hata nisumbua moyo wangu. kwanini aninyanyase na icho kidudu chake? salaaa leeee. kudadeki za kijotijoti.
Ningekuwa mimi, ningeshamkodia majambazi wammalize muda mrefu, ili nioe mtu mwingine ambae hata nisumbua moyo wangu. kwanini aninyanyase na icho kidudu chake? salaaa leeee. kudadeki za kijotijoti.
..Na kuna vipenzi vya mke vingine ambayo labda ulikuwa nako then kakapotea kwa sababu tofati sasa vinata kuja kuwa vinakula lakini havitaki pale pale pa zamani hata kama pamesha milikiwa na mwingine..hivyo ndio tatizo.
Huyu mkuu maisha ni makuu yamemkuta kwa kweli,binadamu tunaishi mara moja ya nini kujitesa...ingawa ukienda kwa wazee utaambiwa kuwa vumilia kijana ndio ukubwa huo..mkeo kaa muongee ingawa inakuwa ngumu sana.
inshabahiana kweli na hayo maneno ya wazee, "vumilia kijana ndio ukubwa huo"!The happiness you get from being able to forgive someone is beyond any apology.
Ni tunda naulizia, lile lililonawiri,
Si langu nawaambia, la kwake bwana Bushiri,
Miye nimetamania, njama nikatafakuri,
Kula tunda kwa kuiba, kwanini huko kutamu?
Mwenyewe yuko kazini, shamba liliko ni mbali,
Zamu yake ni jioni, asubuhi yangu mali,
Nalila kiulani, pasipo ya mushkeli,
Kula tunda kwa kuiba, kwanini huko kutamu?
-Mzee MWKJJ
siku talaka inatoka haooo wanamkimbia anabakia yeye kusaga meno!Tulia mwenye kuhoji, Bwana Bushiri kapanda,
Tulia la mwenye mji, hakuliacha kuvunda,
Tulia yeye mpaji, kalitunza hilo tunda,
Tunda lile la jirani, hilo halina gharama!
Tulia mimi nakiri, sikuingia gharama,
Tulia akisafiri, najinoma huku nyuma,
Tulia alfajiri, hadi wanapoadhama,
Tunda lile la jirani, hilo halina gharama!
-Mzee MWKJJ
...kuna mengi mchongoma hujatuambia
1. je wana watoto? ni wangapi?
2. Ndoa hiyo ni ya muda gani?
3. Wana umri gani wahusika?
4. Mume anafanya kazi ya aina gani relative na kazi ya mke?
Ukijibu hayo labda utapata mwangaza kutoka kwa kina dada.
...