Uwekezaji wa Sh bilioni 157.8 katika ujenzi wa gati mpya umeongeza uwezo wa Bandari ya Mtwara kuhudumia shehena na kukuza biashara. Shehena imeongezeka kutoka tani 177,388 mwaka 2020/21 hadi tani milioni 2.58 mwaka 2024/25, huku bandari hiyo sasa ikiweza kuhudumia meli tatu kwa wakati mmoja...