Hoja hapa ni kwamba unasubiri mtu awe Rais ndipo aanze kuonyesha msimamo? Magufuli hakuanza kujenga utambulisho wake wa kupambana na ubadhirifu siku alipokuwa Rais.
Alikuwa na historia ya misimamo na utendaji kabla ya kufika Ikulu. Hoja si kwamba Kafulila ni Rais, Waziri au Katibu Mkuu; hoja...
Kama Kafulila angeendelea kusimamia misimamo yake ileile ya Tegeta Escrow na IPTL, hakika leo angekuwa mbali sana kisiasa.
Kuwa ndani ya CCM hakumaanishi kuachana na misingi na misimamo iliyokujengea heshima kwa wananchi.
Mbona Magufuli aliweza kufanya hivyo akiwa ndani ya CCM? Basi, chama...
Sijaona kazi ya msingi anayoifanya Kafulila zaidi ya kusifia Samia na CCM. Kama kweli anataka kujenga imani kwa wananchi, arudi kwenye eneo alilojijengea jina: kupambana na ufisadi, ubadhirifu na matumizi mabaya ya fedha za umma. Huko ndiko wananchi wanahitaji kuona msimamo na matokeo yake.
lakini, Kama sheria ndiyo ilikuwa kikwazo, mbona haikurekebishwa mapema? Au Serikali za nyuma zilikuwa hazina uwezo wa kutatua changamoto za sheria yenyewe? Tusichanganye kutokuwa na uwezo wa kutekeleza na kukosekana kwa sheria. Na zaidi ya yote, kuwa na miradi 100 kwenye pipeline si sawa na...
Hiyo hoja ya kusema sheria ilikuwa kikwazo kabla ya 2023 ni kutafuta sababu ya kufunika ukweli. Sheria ya PPP ilitungwa mwaka 2010, na kama ilikuwa na mapungufu, Serikali ilikuwa na wajibu wa kuyabaini na kuyarekebisha. Sheria si jiwe lisilohamishika; zinafanyiwa marekebisho kadiri mazingira na...
Mfano wa sukari hauwezi peke yake kuwa ushahidi kwamba sekta binafsi ni “turufu ya usalama” kwa viongozi. Sekta binafsi ni muhimu, lakini nayo inahitaji usimamizi madhubuti wa Serikali ili ushindani uwe wa haki, bei zisipandishwe kiholela na maslahi ya wananchi yalindwe. Suluhisho si Serikali...
Ujinga,
Tusichanganye kutembelea stendi na kuleta maendeleo. Hayo ni majukumu ya kawaida ya usimamizi ambayo Halmashauri inapaswa kuyatekeleza kila siku. Kama usafi, usalama na miundombinu ni changamoto, swali ni kwa nini mifumo ya usimamizi imeshindwa kuzitatua mapema?
Wananchi hawahitaji...
Ziara ya kushtukiza si kipimo cha maendeleo wala ufanisi wa kiongozi. Wananchi hawahitaji viongozi wanaotembelea stendi na kusikiliza kero kila mara, wanahitaji suluhisho la kudumu. Kwa mfano, kama stendi haina vyoo safi, hakuna utaratibu mzuri wa magari, wafanyabiashara wanakosa maeneo rasmi na...
punguza uchawa kafulila hata hivyo ungeweza haya ikiwa wewe mwenyewe ungekuwa rais, Hoja inaonekana nzuri kisiasa, lakini kiuchumi ina mapungufu . Ukweli ni kwamba huwezi kushindana kwa kudumu na mtu mwenye ufanisi wa 70% ikiwa wewe uko 40% kwa kutegemea PPPs pekee. Ushindani wa soko hutegemea...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.