Hiyo ndiyo TZ ,wanafukuza watoto wa wenzao, wao wako Ulaya na Marekani, tena wengi wao wamekwenda kwa vijisenti vya ufisadi. Mlalahoi hana haki nchi hii, nadhani watanzania wote tuandamane kukataa mabaya yote yanayotokea.
Menejimenti ya TANESCO haiwezi kukwepa lawama, mikataba mibovu waliiona na kila dhambi waliion ikiendelea, kwa kukaa kimya ina maana walishirikiana na ufisadi kwa njia moja au nyingine. Kama wangekua wasafi wangeachia ngazi. Wabunge nao walikua wapi siku zote kusema? mpaka maji yamwagike ndo...
Kuna web site inaitwa wananchi.go.tz, web site hii in picha kuubwa ya mheshimiwa mkubwa kabisa lakini pale hamna kitu, kwa sasa mimi nimeacha kabisa kuitembelea kwani ukiandika hoja miezi mitatu wanakujibu tutashughulikia hoja yako ila ukiwasifia majibu unayapata baada ya dakika 3. Kwa kweli...
Nimefurahishwa sana na habari uliyotuletea Kitila inaonyesha ni kiasi gani unaijali nchi yako hata kama uko mbali. Big up kwa wananchi waliofunga mgodi,naona watanzania wanaanza kuamka usingizini, hicho ndo tunachotaka. Ifike siku waziri afungiwe mlango nje ya ofisi yake maana viongozi wetu...
Huyo jamaa ajiuzulu ubunge au asijiuzulu sisi tunachotaka vijisenti vyetu virudi. Ila nawashauri watu wa jimbo lake waliomchagua sababu alikua na vijisenti wamkatae na wamzomee atakapokwenda kuongea nao, wasilete habari ya Monduli baada ya Lowassa kujiuzulu.
Kwa kweli ni aibu, wale waliokua wanaitwa mashushushu enzi za Nyerere siku hizi mabishoo wanatesa vijiweni, wengi wao watoto wa hao hao ,what do you expect. ingekua uwezo wangu ningewafuta wote na kuwaweka wapya na kuwafuatilia nyendo zao.
Jamani tuwasaidie Wanafunzi hawa,kuwalaumu inaruhusiwa ila baada ya lawana tutoe ushauri unaojenga.Mimi si mshabiki wa chama chochote cha siasa ila ni mshabiki wa maendeleo. Kama chama chochote kikiwaita wanafunzi kwa maslahi ya wanafunzi hao sidhani kama kuna ubaya kuhudhuria. Kwa hili la...
I think we should be very careful with chinese investors, See what they have done at sam nujma road and other projects, most of their products are of sub standard.My caution is we have to keep our eyes wide open when we are entering into contracts with Chinese.
Matumizi ya serikali ni makubwa sana lakini wafanyakazi wa kawaida hawana share kabisa zaidi ya vijisumni vya mishahara.Ukweli ni kwamba serikali inanunua vitu kwa zaidi ya asilimia 100 ya bei halisi ya hivyo vitu, huo ndiyo ukweli kama mimi muongo katafute listi ya bei za zabuni kwenye wizara...
Huyo jamaa ana kiburi na dharau kubwa, mimi daima huwa siwashangai watu kama hao mimi namshangaa aliyewachagua. Labda slogan ya maisha bora kwa kila mtanzania hatukuielewa vizuri,inabidi tuwatafute hawa watanzania na tuwajue ni kina nani labda ndo kina chenge?
Tatizo watanzania ni wapokeaji wa kila kitu, kiwen kibaya au kizuri, kikiwa kibaya tutakizungumzia kijiweni halafu aliyekifanya akipita na Vogue tunamsifia. hao ndiyo wa TZ bwana.Ila sasa naona wameanza kuamka ,watu sasa hawaogpi kutoa maoni ya mbele ya kadamnasi nadhani tusikate tamaa...
Jamani mambo haya mazito, kufungua kesi si mchezo eti,umesahau waziri mkubwa mwenyewe aliongea waziwazi kua wanawaogopa sasa kama serikali inawaogopa weye utaweza? Utaalamu wa kesi hizo anao mchungaji itabidi aombwe ushauri.Kwa mawazo yangu kushitaki haitasaidia kwani unaposhitaki unapaswa kutoa...
Hivi nani kawadanganya wabunge wako kwa maslahi yenu? hivi mnafikiri mahela yote waliyotumia kupata ubunge ilikua ni jitihada za kuwatumikia wananchi? lazima wazirudishe ndipo wawakumbuke wapiga kura na kabla hazijarudi sawasaw uchaguzi mwingine huoooo, maendeleo yatakuja kweli? iliyobaki...
JamiiForums uses cookies to help personalise content, tailor your experience and to keep you logged in if you register.
By continuing to use this site, you are consenting to our use of cookies.