Recent content by Dr Adam Francis

  1. Dr Adam Francis

    Kwenye mfumo wa majimbo Rais ni yule aliyeshinda mikoa mingi na sio idadi ya kura nyingi

    Ww ndio hujaelewa nilichokiandika. Hakuna usawa wa rasilimali na mapato katika mikoa yao. Changamoto ya kukosekana kwa usawa huo utapelekea kuwa na mikoa masikini na mikoa tajiri. Katika muundo unaoupendekeza, kuchukua rasilimali za mkoa ulioendelea unaojitegemea kupeleka kwenye mikoa masikini...
  2. Dr Adam Francis

    Kwenye mfumo wa majimbo Rais ni yule aliyeshinda mikoa mingi na sio idadi ya kura nyingi

    Changamoto ni kuwa mikoa yetu haina utajiri wa rasilimali na mapato unaofanana. Mkoa unapokua jimbo na unajiendesha wenyewe hauwezi kuwa tayari kutoa rasilimali zake kuendeleza mikoa mingine. Huo ndio mwanzo wa balkanization
  3. Dr Adam Francis

    Rais Samia afanya kikao na Vyama vya Siasa Ikulu Dar

    Mwanzo mzuri! Mwisho wa yote watanzania tunataka amani na utulivu ili tujenge nchi yetu.
  4. Dr Adam Francis

    Natamani hili suala la Lissu lifike mwisho, Watanzania tuijenge nchi yetu

    Tulifunzwa, mafahali wawili wagombanapo, zinazoumia ni nyasi. Hiki ndicho kinachoendelea nchini kwetu sasa. Kwahali ilipofikia sasa, kutafuta nani anamakosa haitatusaidia. Maana lipo wazi hakuna upande, kati ya CCM na CHADEMA ambao upo tayari kukiri na kuwajibika. Hii mivutano na vita za...
  5. Dr Adam Francis

    Somo kutoka uchaguzi wa Marekani; "Tume huru ya uchaguzi ndiyo njia pekee itakayowafanya viongozi wawaheshimu wananchi"

    Ni kweli comrade. Lakini tukiiboresha kwa kuipa uhuru zaidi, hauoni tutakuwa tumeikuza demokrasia yetu kwa hatua kubwa zaidi?
  6. Dr Adam Francis

    Somo kutoka uchaguzi wa Marekani; "Tume huru ya uchaguzi ndiyo njia pekee itakayowafanya viongozi wawaheshimu wananchi"

    Moja wapo ya hoja alizowahi kuzitoa Baba wa Taifa Mwl. Nyerere kama sababu za kwanini nchi yetu ielekee kwenye mfumo wa vyama vingi ilikuwa ni hatari ya chama kuonea watu kinaposhika hatamu. Tafakari hii haihitaji PhD kuing'amua. Katika mazingira ambayo viongozi wa chama na serikali wanayo...
  7. Dr Adam Francis

    Naiona CHADEMA ikisambaratika, nani alaumiwe?

    Sawa, sie yetu macho. Tuko pale tanawatazama mtaichezaje ngoma yenu.
  8. Dr Adam Francis

    Naiona CHADEMA ikisambaratika, nani alaumiwe?

    Sie tena? Ugomvi wenu wenyewe, mchawi anatokaje CCM?
  9. Dr Adam Francis

    Naiona CHADEMA ikisambaratika, nani alaumiwe?

    CCM inahusikaje kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe ya CHADEMA?
  10. Dr Adam Francis

    Naiona CHADEMA ikisambaratika, nani alaumiwe?

    Dola haziangushwi na maadui kutoka nje, historia inatufundisha kuwa Dola huuawa na vita zake za ndani kwanza hatimaye maadaui wanje humalizia kazi. Ndio maana waswahili husema mjenga nchi ni mwananchi, kadhalika mbomoa nchi ni mwananchi. Chama kikubwa kama CHADEMA kilichopitia misukosuko mingi...
  11. Dr Adam Francis

    Update: Siku ya 8 toka nimeacha pombe maendeleo ni mazuri sana

    Hongera sana kwa uamuzi mzuri! Tutakuunga mkono
  12. Dr Adam Francis

    Ushauri kwa wanasiasa vijana "Usiharibu Kwenu"

    Hoja nzuri sana comrade. Hongera sana.
  13. Dr Adam Francis

    Magereza wagoma kutekeleza amri ya mahakama ya kumruhusu Tundu Lissu kuwasiliana na mawakili wake

    Nchi yetu haijakamilika comrade. Its a work in progress. Pamoja na mafanikio mengi tulioyapata tangu uhuru hadi sasa, ni kweli kuwa bado tunachangamoto kadhaa haswa kwenye demokrasia yetu, haki za binadamu, uwajibikaji na utawala wa sheria. Mapungufu haya ni sehemu ya mchakato wa Taifa letu...
  14. Dr Adam Francis

    Ningekuwa Mwenyekiti wa TAHLISO, ndugu Kiliba, ningefuata nyayo za Makonda

    Huo ndio ukweli wa siasa za duniani kote, sio jambo linalohitaji fikra mpya.
  15. Dr Adam Francis

    Ningekuwa Mwenyekiti wa TAHLISO, ndugu Kiliba, ningefuata nyayo za Makonda

    Mm sijasema CCM itaanguka! Nimesema ikitokea CCM imeanguka, yeyote atakayeshika dola, tusitegemee asiitumie dola kutekeleza agenda zake
Back
Top Bottom